Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Mama angu mlezi alifariki April 10 2019, toka kipindi hicho hua namuota sana. Mara nyingi nilikua namuota tupo kwenye nyumba niliyokulia namuona anapika. Mwezi uliopita nilimuota kafariki wakamleta kanisani akiwa kavishwa sanda. Niliokopa sana.

She was muislim, nimeulizia kwa wenye uelewa wa dini hii wananishauri nikamfamyie kisomo hiyo hali inaweza kuisha. Naplan kufanya hivyo siku moja, Hopefully Mungu ataniwezesha
Yes fanya hivyo,
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole sana Mungu akutie nguvu
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Mkuu pole sana.

Haielezeki na haivumiliki ila unatakiwa kuukubali ukweli kwamba hayupo tena.

Mimi alifia mikononi mwangu halafu ndio nilikua nimeanza kupanda mlima wa mafanikio angalau nianze kulipa fadhila zake ila ikashindikana.

Kinachoniumiza zaidi ni kwamba ali sacrifice maisha yake kwa mafanikio yangu ya ya watoto wake wengine kwa maana kwamba nilitafta hela nimpeleke India akakataa kwamba hata kama akienda akapata nafuu bado atakufa so nisiharibu hela, akakataa kabisa.

Akasema kama nina hela ya kumtibu, basi niitumie kusaidia ndugu zangu wengine (nina ndugu zangu wengine mambo yao hayakua sawa) akaniambia niwasaidie hao ila sio yeye.

Nikapambana nae Muhimbili lakini ikawa hivyo so akafariki mikononi.

Kwa sacrifice aliyofanya, ikabidi na mimi niamue jambo moja, nikaamua ku sacrifice kila kitu changu kwa miaka 4 kuwabust hao jamaa, yaani sikufanya maendeleo yangu binafsi yoyote kwa miaka 4 angalau wakae level. Kwa miaka 4 mapato yangu yote nimeffanya hivyo.

Anyway, nimetoka kumuota usiku huu halafu naamka nakutana na hii mada, mada kama hizi hua sipendi kuzisoma maana naishia kulia tu.

Mama yangu endelea kupumzika kwa amani, najua sacrifice yako kwenye maisha yangu haina mfano na sitakaa kuja kuilipa hata robo. Namini one day tutaonana tena.
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole sana mkuu.

Kumbuka kufiwa ni kukomaa pia.

Kifo ni maumbile, unapoishi na kuweka akiba kichwani suala la kufiwa na watu wako wa karibu halitakusumbua sana likutokeapo.

Aheri usahau kufa mwenyewe kuliko kusahau kufiwa, ama ukadhani kuwa, kifo ni maalumu kwa ajili ya wakubwa wanaokuzidi umri ama watu flan flani tu, maana kunakufiwa na wanao wadogo pia. Jambo hilo ni lazima ulikumbuke.

Ninakupa pole sana, ninaelewa aina gani ya uchungu ulio nao kwa kuondokewa na mama yako kipenzi.
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole sana ni hali ngumu sana asikwambie mtu ila yaache machozi yatoke usiyazuie.. Machozi ni tiba
Machozi hupunguza uchungu
Machozi huonesha kujali
Machozi huonesha upendo
Usiyazuie yaache yatoke.. Usipomlilia sasa utamlilia lini!?[emoji24]
 
Pole mkuu asee[emoji24]

Sipati picha mzazi kuondoka sijui ntakuwaje...wenye wazazi wote wawili tuzidi kumshukuru Muumba[emoji120][emoji120]
Hata mimi nilihisi nina haki bado ya kuwa na wazazi wote lkn haikuwa hivyo
 
Pole sana ni hali ngumu sana asikwambie mtu ila yaache machozi yatoke usiyazuie.. Machozi ni tiba
Machozi hupunguza uchungu
Machozi huonesha kujali
Machozi huonesha upendo
Usiyazuie yaache yatoke.. Usipomlilia sasa utamlilia lini!?[emoji24]
Mimi nilishindwa kulia baadae uchungu nusura unipe uchizi.
Machozi ni dawa
 
Poleni sana

Sisi wenye wazazi, tuwaheshimu, hatuwezi ona umuhimu wao hadi siku tukiwahitaji na hawapo kabisa
 
Mimi nilishindwa kulia baadae uchungu nusura unipe uchizi.
Machozi ni dawa
Ninapokumbuka kile kipindi kile basi tuu[emoji25][emoji24] ilikuwa mwezi wa tatu siku chache mbele kabla ya birthday yake[emoji24] tuko kikaoni simu nimeweka silent mode .. Halafu ikaingia msg...[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24].. Mom was no more[emoji25]
 
Ndugu yangu maumivu ya kufiwa na mzazi hayana FARAJA yanj asikudanganye mtu kwamba kuna mtu au kitu kitakufariji uyaepuke. Ni maumivu ambayo lazima uyapitie kwa ukali ule ule bila huruma. Yatapungua kulingana na wakati unavyoenda, yani miaka imavyozidi kusonga yanapungua taratibu ma sio kuisha.

Pole sana
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Duh kweli chini ya 50 inahuzunisha sana.
 
Back
Top Bottom