Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

I lost my dad 2017
I lost my mom 2019
Na Wala hawakuwa wazee
Ni muda tu utakuponya ukae sawa.
Here I am stronger than ever nipo nachapa gwaride because they left a strong daugh

Wapo hai ila usijisifu na kuwakejeli ambao hawana wazaz rafiki
Nitakuwa mjinga wa mwisho duniani kama nitakejeli kwanza naanzaje kufanya hivyo katika umri wangu wa miaka 39
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Mungu akutie nguvu,yeye tu aweza kukufariji,binafsi sijui hat nilivukaje,Mungu alinisaidia
 
Mama yangu alikufa 1992 alituacha 4 nilipata uchungu nikiwa mtoto mpaka sasa nimekua mama wa watoto 3 ila hapa ninaandika huku nalia. Kwani baada ya hapo nilipotoa changamoto nyingi sana kwani mimi ndio nilikua mkubwa. Kuna maisha fulani huwezi kueleza kwa mtu. Ila sasa nimekua mfanyabiashara mkubwa na wadogo zangu wako vizuri najionea fahari na wadogo zangu kwani ndio tuliofarijiana kwa kipindi chote.
Mama pumzika kwa amani alikufa akiwa na miaka 30
 
Wazazi walioaga dunia

Mithali 6:20-22

[20]Fanya kile baba yako akuambiacho, mwanangu, wala usisahau kamwe yale ambayo mama yako alikufundisha.

[21]Yaweke maneno yao kwako siku zote, yakiwa yamefungwa moyoni mwako.

[22]Mafundisho yao yatakuongozeni msafiripo, yatakulindeni usiku, na yatakushauri mchana.

Pole mkuu, I know how it feel, but with time your wound will heal.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
siku mdogo wangu alivyofariki ilinitia huzuni na simanzi sana😭😭.....maadui zangu walitaka kuutumia huo msiba kunimaliza kabisa....kwa sababu kama nisingekaza ningeathirika kisaikorojia ila hilo nililitambua mapemaaa....nilisimama imara kama nilivyosimama imara kipindi cha mwendazake...mwendazake alikuwa amepania kutupoteza kabisa kwenye ramani sisi wasomi watoto wa wakulima tusiokuwa na connection....alitaka wengi wetu tuishie kufanya kazi za hovyoo....alitaka nyuso zetu zipoteze nuru kwa sababu ya kukosa matumaini ya maisha yetu ya baadae.......lakini mungu aliamua kusimama nasisi😢😢😢😢 .....wasomi wote tusiokuwa na connection tupo imara mpaka leo mikono juuuuuuuuuuuuuuuuuu.......mwamba wa miamba wote mikono juuuuu....😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Faraja pekee ni kusali sana. I have lost a mother too, miaka 6 imepita ila kumove on haiwezekani sababu kila ukipata issue ambazo yeye alikua msaada au mshauri lazima itakusumbua. Kwahyo jambo la kukushauri ni kusali na kukubali tu kuwa mama hauko naye tena. Ila hauwezi kumove on. POLE SANA na Apumzike kwa Amani
 
Binafsi mama yangu ndio alikuwa tegemeo langu kwe2 mambo ya kujikwamua kusaka elimu, wala hakuumwa aliniaga anasafiri akirudi tutaongea vizuri, dah ndio ikawa ntolee iyo.. Miaka 7 sasa bado sijamsahau ni ngumu sana kusahau. Tumshukuru mungu kwa yote.
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Ebwan hili usiombe likukute... il muhimu nenda kanisani dua na sala utapata faraja maana mtuhani huu mgumu sana
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Utalia milele kwenye maisha.... tena hapo mbona hujalia... haijawahi kuzoeleka.

Ila Bora hata wewe umeweza kupost kabla ya mazishi. Wengine hata nguvu za kupost hazikuwepo.... tulikuwa kama wajinga....yani kwa kifupi zaidi ya kupiga na kupokea simu mengine hayakuwezekana.
Pole kwa Kifo cha mama....
 
Pole. Lakini hayo ndo maisha yetu wanadamu, tunakufa/tutakufa lazima. Uwe unasoma Biblia pia na usitafute faraja kwa watu saaana maana nao watakufa. Soma 1Wathethalonike 4:13-18
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Simple tu nilikuwa form six nilihandle situation bila wasi
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Moshi uko mtoto kaua Mama yake.
 
Mimi nilimpoteza mama mwaka 2020, nikampoteza mtoto mwaka 2021, mwaka huo huo 2021 mwezi uliofuata nikampoteza baba...haya mambo nikumuachia Mwenyezi Mungu tu na katika kipindi hicho kila jambo unaloliwaza kumbuka kwamba Mungu yupo na unazidi kumuomba yeye akupe uvumilivu na akuvushe salama...pia amini wazazi wapo mahali salama na siku Moja tutaonana katika heriiii ....

Pole sana kwa magumu unayopitia na Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.
Pole sana.Mapito juu ya mapito.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Pole sana mkuu wangu. Ila kama ukijihisi kulia lia tu wala usijikaze. It helps much.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Back
Top Bottom