Mkuu pole sana.
Haielezeki na haivumiliki ila unatakiwa kuukubali ukweli kwamba hayupo tena.
Mimi alifia mikononi mwangu halafu ndio nilikua nimeanza kupanda mlima wa mafanikio angalau nianze kulipa fadhila zake ila ikashindikana.
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba ali sacrifice maisha yake kwa mafanikio yangu ya ya watoto wake wengine kwa maana kwamba nilitafta hela nimpeleke India akakataa kwamba hata kama akienda akapata nafuu bado atakufa so nisiharibu hela, akakataa kabisa.
Akasema kama nina hela ya kumtibu, basi niitumie kusaidia ndugu zangu wengine (nina ndugu zangu wengine mambo yao hayakua sawa) akaniambia niwasaidie hao ila sio yeye.
Nikapambana nae Muhimbili lakini ikawa hivyo so akafariki mikononi.
Kwa sacrifice aliyofanya, ikabidi na mimi niamue jambo moja, nikaamua ku sacrifice kila kitu changu kwa miaka 4 kuwabust hao jamaa, yaani sikufanya maendeleo yangu binafsi yoyote kwa miaka 4 angalau wakae level. Kwa miaka 4 mapato yangu yote nimeffanya hivyo.
Anyway, nimetoka kumuota usiku huu halafu naamka nakutana na hii mada, mada kama hizi hua sipendi kuzisoma maana naishia kulia tu.
Mama yangu endelea kupumzika kwa amani, najua sacrifice yako kwenye maisha yangu haina mfano na sitakaa kuja kuilipa hata robo. Namini one day tutaonana tena.