Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuhusu mali wala usiseme,wanafanyaga vile wanajua wataishi milele,Ni kweli mimi kila ikifika au ikikaribia tarehe 07.02 huwa najisikia vibaya nakosa amani naanza kujichunguza ni kitu gani hakipo sawa bàadaye nakumbuka ni siku ambayo mama yangu alifariki. Huwa nakumbuka matukio yote inauma kwa kweli.
Halafu ukute kuna watu walikunyanyasa, kukutenga, kukudhulum mali za mzazi/wazazi wako baada ya kufariki unatamani uende kwa Mungu na kumshtakia awarudishe wazazi wasolve hilo tatizo, lakini ndio hivyo tena haiwezekani.
Shangaa wewe[emoji23]Braza uliweza vip kufanya kaz huku umepewa taarifa kuwa mam ako kafariii duh uliwezaje mkuu hpn mkuu ukipazwa pale pale ujeuze uende kujiandaa na safari tayar kurud nyumbn ukaomboleze
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Aisee baba/mama siku moja[emoji24][emoji24]Tarehe 1.5.2020
Ilikuwa ijumaa majira ya saa moja asubuhi baba yangu alifariki. Siku hiyo tulikuwa na safari. Akiwa chumbani kwake anajiandaa nami niko nje naweka sawa gari kwa ajili ya safari. Baada ya kumaliza nilimgongea chumbani kwake ili kama yuko tayari tuweze kutoka, sikuamini nilicho kikuta aiseee. Namkuta mzee amelala kitandani huku tayari akiwa amefariki [emoji2357]
Siku hiyo hiyo, majira ya saa tatu usiku mama naye alifariki. Hii ni kufuatia mshituko alio upata. Ilikuwa ni siku ngumu sana maishani mwangu. Hakika jambo la uchungu halisahauliki [emoji26]
Jikaze mkuu, tuwaombee wazazi wetu kwa Mwenyezimungu maisha yao huko walipo yawe mazuri zaidi, nasi mwenyezimungu atujaalie mwisho mwema.
Kabisa mkuu, Kuna wengine tunaogopa hata kucomment, baba yangu alifariki nikiwa Nina miezi sita tu.Dah sasa ambao mama zetu walitangulia tukiwa na 3yrs tukoment wapi jmni
ukiona lako zito ujue kwa jirani ni zito zaidi
Pole sana nduguTarehe 1.5.2020
Ilikuwa ijumaa majira ya saa moja asubuhi baba yangu alifariki. Siku hiyo tulikuwa na safari. Akiwa chumbani kwake anajiandaa nami niko nje naweka sawa gari kwa ajili ya safari. Baada ya kumaliza nilimgongea chumbani kwake ili kama yuko tayari tuweze kutoka, sikuamini nilicho kikuta aiseee. Namkuta mzee amelala kitandani huku tayari akiwa amefariki [emoji2357]
Siku hiyo hiyo, majira ya saa tatu usiku mama naye alifariki. Hii ni kufuatia mshituko alio upata. Ilikuwa ni siku ngumu sana maishani mwangu. Hakika jambo la uchungu halisahauliki [emoji26]
Jikaze mkuu, tuwaombee wazazi wetu kwa Mwenyezimungu maisha yao huko walipo yawe mazuri zaidi, nasi mwenyezimungu atujaalie mwisho mwema.
Nawazaga pia nikikutana mada kama hizi. Wakati mwingine najipa matumaini huenda nikatangulia nikawaacha.Pole mkuu asee[emoji24]
Sipati picha mzazi kuondoka sijui ntakuwaje...wenye wazazi wote wawili tuzidi kumshukuru Muumba[emoji120][emoji120]
Acha kbs , binafsi nilipita Kwa shida mno , muombe Mungu azidi kukuimarisha tu.Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.
Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Kabisa.Kuhusu mali wala usiseme,wanafanyaga vile wanajua wataishi milele,
Pole sana aisee ni kipindi kigumu sanaWandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.
Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole Sana.yalinikuta.hayo,nilikuwa Nalia kila siku kwa Maana Mimi ndo nilikuwa namuuguza,masaa ya kumpa dawa nilikuwa nayajua Mimi.Kila inapofika siku ya xmass Ni msiba Tena,yaani Nalia Mimi,Nalia Sana.Chakula Cha siku hiyo huwa Ni kichungu Sana kwangu.Yaani huwa sipendi siku ya xmass.Nimeshindwa kumove on kwa kweli kuhusu xmass yaani Ni kilio kila mwaka.Yote Tisa kumi kuifuta namba ya simu ya MAREHEMU mama,ilikuwa Ni mtihani kwangu.yaaani nimelia saaaana.Usijali mkuu,Mungu mwema,atakuvusha tu.Ndugu zangu wapendwa habari za muda mrefu tena.
Ninajitahidi kuzoea hali ya kutokuwa na mama ila bado siamin kama ndo mazima.... Inauma lkn hakuna namna.
Mama tulimzika na matanga tayri.
Kuna kauli nilizokutana nazo kwa kipindi hiki nazikumbuka sana naomba niweke hapa.
Dadammoja ambaye yeye ni Yatima na amekuwa vizuri mikononi mwa ndugu wengine na sasa yupo JWTZ alinipigia simu na kuniambia: SHUKURU WEWE MZAZI AMEKUKUZA HADI HAPO ILA WENGINE WANAPOTEZA WAZAZI MAPEMA ZAIDI.
hii kauli iliniingia kichwani.
Binamu yangu mmoja aliniambia.
Nimekuja msibani sio kwa ajili ya baba yenu(kwake ni mjomba) wala ninyi (sisi sasa) ila ni sababu za mama yenu (marehemu) the way alivyoishi na sisi....ana heshima kubwa. Kuna vitu alitengeneza ambavyo vina msaada mkubwa kwetu na sisi tuendeleze.
Pia SWALA MSIBA LISAHAU MAPEMA MAANA KUNA MAISHA BAADA YA MSIBA.
Wa tatu ni broo mmoja ambye hata simjui.
Mama yako yupo sehemu salama zaidi ya hapa duniani hakuna haja ya kusikitika.
Hizi ni chache zinazo run kichwani muda wote ila ni nyingi sana ninazo kumbuka .
Nathamini kila mchango wa mwana JF kwan nimepitia kila comment na zimenifariji sana sana.