Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Pole na wewe pia. Kifo hakizoeleki.
Ansante

[emoji1545],tarehe ya leo tareh 25.... ni kumbukumbu ya kifo cha baba yangu[emoji24][emoji24][emoji24],

Naona kama vile bado yupo ndani ya nyumba[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Yaani kuna wakati napatwa na mitihani,najisemeaga tu angekuwepo baba[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Allah amrehemu
 
Mkuu pole sana.

Haielezeki na haivumiliki ila unatakiwa kuukubali ukweli kwamba hayupo tena.

Mimi alifia mikononi mwangu halafu ndio nilikua nimeanza kupanda mlima wa mafanikio angalau nianze kulipa fadhila zake ila ikashindikana.

Kinachoniumiza zaidi ni kwamba ali sacrifice maisha yake kwa mafanikio yangu ya ya watoto wake wengine kwa maana kwamba nilitafta hela nimpeleke India akakataa kwamba hata kama akienda akapata nafuu bado atakufa so nisiharibu hela, akakataa kabisa.

Akasema kama nina hela ya kumtibu, basi niitumie kusaidia ndugu zangu wengine (nina ndugu zangu wengine mambo yao hayakua sawa) akaniambia niwasaidie hao ila sio yeye.

Nikapambana nae Muhimbili lakini ikawa hivyo so akafariki mikononi.

Kwa sacrifice aliyofanya, ikabidi na mimi niamue jambo moja, nikaamua ku sacrifice kila kitu changu kwa miaka 4 kuwabust hao jamaa, yaani sikufanya maendeleo yangu binafsi yoyote kwa miaka 4 angalau wakae level. Kwa miaka 4 mapato yangu yote nimeffanya hivyo.

Anyway, nimetoka kumuota usiku huu halafu naamka nakutana na hii mada, mada kama hizi hua sipendi kuzisoma maana naishia kulia tu.

Mama yangu endelea kupumzika kwa amani, najua sacrifice yako kwenye maisha yangu haina mfano na sitakaa kuja kuilipa hata robo. Namini one day tutaonana tena.
Dah nimekuwa speechless 😢😢
 
Kwanza pole kabisa Mkuu! Mungu Yuko pamoja na wewe.
Utazoea tu! Sisi tulishazoea.
 
Ansante

[emoji1545],tarehe ya leo tareh 25.... ni kumbukumbu ya kifo cha baba yangu[emoji24][emoji24][emoji24],

Naona kama vile bado yupo ndani ya nyumba[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Yaani kuna wakati napatwa na mitihani,najisemeaga tu angekuwepo baba[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Allah amrehemu
Ni kweli mimi kila ikifika au ikikaribia tarehe 07.02 huwa najisikia vibaya nakosa amani naanza kujichunguza ni kitu gani hakipo sawa bàadaye nakumbuka ni siku ambayo mama yangu alifariki. Huwa nakumbuka matukio yote inauma kwa kweli.

Halafu ukute kuna watu walikunyanyasa, kukutenga, kukudhulum mali za mzazi/wazazi wako baada ya kufariki unatamani uende kwa Mungu na kumshtakia awarudishe wazazi wasolve hilo tatizo, lakini ndio hivyo tena haiwezekani.
 
Nilikuwa masomoni, nikapanga likizo ya December 2020 nikafanyie sapraizi.
Tarehe 22 Okt 2022 nikadanganywa kesho uende nyumbani mama mgomjwa.
Nikajiandaa zangu mmajira ya saa 5 usiku nakuta SMS.

“Pole sana kwa kuwa na kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mama. Mungu akutie nguvu mdogo wangu.”

Nililia kama mtoto, nilishindwa kulala usiku. Yaani ile nafika nyumbani kila nikiangalia picha za mama pale ukitani akiwa anatabasamu naishia kulia tu[emoji24]
 
Pole sana.mkuu.Hata mimi nikimkumbuka mama yangu huwa namuona akitabasamu siku zote. Baba naye alishatangulia mbele ya haki tena 2012 lakini picha yake haiji kama ya mama .
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Kama ww n mwanaume n kukaza roho mkuu ...huwez badili kitu..mm nmefiwa na mama angu mwezi wa 6 mwaka huu nilipata taarifa asubuh nikiwa tayari naenda kazin tena n mbali na hakuna dereva n ww mwenyew ...IMAGINE NLIPGA KAZ HADI JION NKARUD ZEN NIKAWAAMBIWA WAFANYAKAZI WENZANGU kwamba maza gone!!! Ukizaliwa mwanaume tambua hutakiwi kutia huruma n kukubaliana na tukio lolote. .na katika maisha jiandae kuskia habar yoyote mbaya au zur...OVER
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Pole sana mkuu!!!

Inasikitisha hasa hapo ambapo hata karne hajaigawa,jamani wenye wazazi wapendeni sana wazazi wenu tujue hawataishi mara mbili
 
Back
Top Bottom