Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Kwanza pole sana Mkuu, na nikwambie kitu hakuna namaanisha hakuna kitu unaweza ambiwa au hata watu wakucomfort vp kikaweza japo kupunguza maumivu ya kuondokewa na mama hakipo. Mimi nina miaka mitatu mama yangu amefariki ila kila nikiingia chumbani kwake najikuta machozi yanadondoka yenyewe nikiwa hata bar nikisikia nyimbo yoyote inayomhusu mama mimi ni kilio siwezi kujizuia kwenye hili hata kidogo. Ni Mungu mwenyewe ndio akawe mfariji wako ila Mama anauma aisee acha kabisa.
 
Machozi yamenitoka mnoo, ama kweli hakuna upendo mkuu Duniani kama wa mama, Mungu aendelee kuwapa pumziko la milele zetu wote waliotangulia mbele ya haki.
Mungu aendelee kuwapa afya njema na baraka zitokazo kwake mama zetu walio hai maana hatuna chochote Cha kuwalipa ili kufidia Yale waliyowahi kututendea na maumivu mazito waliyokwisha kupitia kwaajili yetu

Sent from my CPH2239 using JamiiForums mobile app
 
Pole Sana,

Huwa nawazaga leo nipo ma mama na najisemea ndiyo kila kitu kwangu,vipi siku naambiwa mama yako hatunae tena,yaani ni fumbo,

Mama ananiambiaga yaani nawaza nikifa sijui nitakuacha ktk hali gani mwanangu,yaani nakuwazia wewe kuliko hata wadogo zako,
 
Mmmmmmh anajiendekeza?

Haujui tu,yakupasa[emoji40]
 
Reactions: Ok9
Kudeka muhimu kaka.
Katika kuandika huku nimegundua mengi sana
 
Tushapoa maumivu ila sometimes unagombana na mtu anamtukana mama yako aliekufa tena saa nyingine mkeo Kabisa anamtukana mama yako.Mke Wangu ana wazazi wake wote wawili lkn tukigombana anawatukana wazazi Wangu waliokufa bila woga
 
Mkuu kifo hakizoeleki na ngumu Sana mtu wa karibu yako akakutoka na utachukuwa mda Sana kumsahau na hata ukimsahau Kuna siku unaweza ukaanza kulia mwenyewe
 
Reactions: Ok9
Tushapoa maumivu ila sometimes unagombana na mtu anamtukana mama yako aliekufa tena saa nyingine mkeo Kabisa anamtukana mama yako.Mke Wangu ana wazazi wake wote wawili lkn tukigombana anawatukana wazazi Wangu waliokufa bila woga
Mh na bado ni mkeo?
 
Mimi nimefiwa na baba yangu miaka kama miwili imepita[emoji24][emoji24] na bado akili yangu haija kubali kwamba ameniacha!
Huwa nalia kila ninapo mkumbuka na kwenye ndoto zangu huwa ninamuona ni mzima kabisa tuna endelea na maisha mazuri tulio kuwa nayo!
Yaani we acha tu ni uchungu wa hali ya juu [emoji30]
Namwomba Mwenye Enzi Mungu anipe nguvu na amani moyoni mwangu!
Nami nakuombea na wewe amani ya Mwenye Enzi Mungu iwe nawe milele walahi!
 
Kwanza nikupe Pole Sana mimi nimepita changamoto hiyo alianza Baba, baada ya mwaka akafuata mama kisha dogo aiee niliishi Jehanamu nikiwa dunian lkn Neema ya Mungu ilinipitisha salama.

Mwombe tu Mungu akusaidie ni maumivu Sana.

Pole sana!
 
Maumivu ya kufiwa na mama hayaelezeki....kuna muda unafika unatamani mamaako awe hai umueleze matatizo akusikilize akubembeleze lakini wapi....mimi wangu alifariki 2004 lakini maumivu yake hadi leo hayaelezeki

Mtumeee!
Kwa kweli Mwenye Enzi Mungu akusaidie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…