10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.
Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.
Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,
ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno
Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.