Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Usiwalazimishe wakuelewe waache na ujinga wao pia hao wasichana wanaowakataa walimu achana nao, mtu sahihi huja kwa wakati sahihi pasi kuangalia kipato,dini,rangi au jamii Fulani! Ila ukipata mwalimu anaejitambua hasa wa kike utaenjoy maisha ya ndoa Kama uko Edeni! Yote kwa yote walimu Ni walezi wazuri mno hasa wanaojitambua!
 
Life style inawafanya walimu waonekane njaa kali. Utakuta mwalimu anaishi maisha ya kawaida sana hatakama analipwa vizuri na ukienda taasisi za mikopo utawakuta wamejazana.

Hii ni sawa sawa na wafanyakazi wa migodini hasa technicians na wale unskilled, mtu analipwa 2m+ lakini ukiona maisha yake utadhani analipwa laki2. Ndomana mtaani utasikia "haya ya mgodini" yanadharaulika na kuonekana wana njaa kwenye mikopo sasa ndo usiseme. Japokuwa kwa sasa kuna waliobadilika lakini bado wengi wanaishi maisha choka sana.

Hebu angalia mfanyakazi wa bank hatakama analipwa 1m lakini yuko smart kuanzia kuvaa, chakula hadi makazi.
 
Mwalimu mwenye degree Basic yake ni 771,000/=..? Kwan Askar Jesh au Polisi mwenye degree nae analipwa sh ngap nliwahi sikia wao wana mishahara miwili na katikat ya mwez wanalipwa

kama ni hivyo basi ni kweli wanazidiwa.

mdogo wangu wa mwisho ni polisi ana degree analipwa 860k
 
Walimu kinachowabeba,
Wana akili ya maisha Sana,
Wanapata kidg,ila Wana uwezo wa kufanya maendeleo

Kuna afisa maliasili mmoja Huwa nakunywa nae pombe Hadi za laki 8, ila Hana hata kibanda Cha kujistiri na Yuko kwenye late 50s
Yulea afisa Baba yake ana nyumba saba na Mashamba, huyo baba yake mzee tumemzika juzi juzi tu! sasa afisa misitu akajenge na nyumba za Baba yake na mashamba yao utakaa weye??

usimuone vile ukamuiga kwao wako njema!! na yeye ndo mkubwa wadogo zake woote wana mijengo ya hatare!
 
Ngoja nitunze hii comment

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Walimu walilazimika kuomba ukarani wa sensa sababu shule zote zimefungwa kupisha zoezi hilo, sasa ulitaka wakae nyumbani wakati mtu angeweza kujaribu bahati yake akapata vi laki viwili vitatu vya ukarani!?
Ugumu ea maisha tu mkuu hakuna sababu nyingine. Hizo ulizoandika ni porojo za kujifariji.
 
Neno
 

kama ni hivyo basi ni kweli wanazidiwa.

mdogo wangu wa mwisho ni polisi ana degree analipwa 860k
hii ni posho kwenye baadhi ya mashirika ya umma
 
Kwahiyo kuiba nako kumewekwa kwenye chanzo cha mapato? Dah. Tuna safari ndefu sana kifikra🙆‍♂️🤭🤭🤭🤭😳😳😳
 
Watanzania tumefikia mahali ambapo tunahesebu kipato kwa kuchanganya na pesa za hongo. Siyo kila kazi ina mianya hiyo, na ni makosa kusema kipato cha mtu kiko chini kwa sababu hapokei hongo. Hii imekuwa ni sehemu ya utamaduni wetu Watanzania, ambapo wezi na wala rushwa wanasifiwa kwa kujenga na wale wanaofanya kazi kwa kutumia haki kuonekana failures mbele ya jamii. Hayo yamenipata saana, lakini hayakuweza kuniyingisha kubadili maadali yangu ya kazi. Nimweza kufanikiwa bila kuchukuwa hata senti tano ya mtu au kupokea malipo ya aina yopyote ikiwa ni pamoja na ngono. You can succeed without ufisadi wa aina yoyote, I am testimony to that.
 
Wanabakia na laki na nusu kwa mwezi baada ya mikopo, pili hawana kamba za kuvuta
Shule pengine ina walimu 30 hakuna hata mmoja anayemiliki kadi ya ATM, zote ziko kwenye taasisi za mikopo
 
Weka takwimu sio maneno matupu. Polisi anamzidi sh? Mwalimu?
 
Mara ya mwisho kusikia mwl ameenda Dodoma kuna kikao ni lini? mara ya mwisho kusikia mwl yuko kwenye kikao na hicho kikao kina posho ilikuwa lini? Pesa wanayopata hizo kada nyingine ni pesa halali iliyopitishwa na serikali, ukitaka umaskini kwako uendelee mwambie mwanao awe mwalimu.
 
Hapo ndio nagundua kwa nini walimu huwa hawazeeki haraka, dhulma wizi na kunung'unikiwa na watu humfanya mtu kusinyaa mapema
 
Umemaliza
 
Acha kelele huoni mshahara ya diploma zote za afya, diploma zote za afya zinaanza na TGHS B ambayo ni kama 800,000, degree ya udaktar wanaanza tghs.E 1,500,000
Degree ya ufamasia wanaanza na TGHS-D 1,250,000
Na degree zingine zote zilizobaki afya Wanaanza na TGHS C 1,000,000
Ukisema walimu wanaizidi kada zote serikalini kwa 5000 waombe radhi watu wa afya




 
Kama mpaka muda huu mpwayungu village hajachangia chochote kwenye uzi wako, basi atakuwa hajakutendea haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…