Mlioko kwenye ndoa zaidi ya miaka 5

Mlioko kwenye ndoa zaidi ya miaka 5

Jaman mlioko ndoan ndan ya miaka 5 nakuendelea mmewezaje??
Yan mmewezaje kuishi wawil mpaka miaka hiyo

Yaan mi miaka 2 tu nataman dunia igeuke kichwa chini miguu juu
Yan ukimuona mwenzio unapata hasira gafla
Akisafir unataman asirudi du!!!
Mmewezaje jaman nipen mbinu
Du! Pole sana. Inawezekana pale kila mmoja atakapotambua thamani ya mwenzie. Vinginevyo ni kuishi kwa mazoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikubali ndoa ikushinde mapema hivyo, komaa utavuka tu.
 
Ila mwanamke mwenzangu ulikubali vipi kuolewa na mwanaume hakupendi ndio shida unayopata sasa hivi

Mimi acha nikupe pole tu nimefatilia thread zako za nyuma dalili zote ulishaziona kwa huyu mwanaume toka mnaanzisha mahusiano na ukaolewa naye tu moshi unafuka sasa ndani
Kuna muda umri ukufika unatongozwa na wanaume za watu tu hakuna hata wa kukwambia nikuoe
Sasa hali Kama iyo ukikutana na mtu hata kwa bahati mbaya yuko single akajaribisha tu nikuoe wewe unaingia mwil mzima
 
Tatizo mnaingia kwenye ndoa kama step tu ta maisha. Eti muda umefika.

Haya sasa unakiharakisha na kifo maana ndo step iliyobaki.
 
Kwa uzoefu wangu mdogo...ndoa ikivuka miaka mitatu ya kwanza, itadumu muda mrefu kama sio daima. Miaka miwili hadi mitatu ya kwanza huwa ni challenging kwa ndoa nyingi sana. Miezi ya mwanzo ya ndoa ni kama heaven fulani hivi..then reality checks in after na ndio hapo ili muwe aligned kuna migogoro mingi na kutofautiana sana. Ikipita miaka miwili mnakuwa tayari mmeshakuwa mnazungumza lugha moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani mlioko ndoani ndani ya miaka 5 nakuendelea mmewezaje?

Yaani mmewezaje kuishi wawili mpaka miaka hiyo

Yaani mimi miaka 2 tu natamani dunia igeuke kichwa chini miguu juu.Yaani ukimuona mwenzio unapata hasira gafla.

Akisafiri unatamani asirudi dah!

Mmewezaje jamani nipeni mbinu
Hapa ndio ulipomkaribisha pepo...
 
Back
Top Bottom