Mlioko serikalini msijione 'Special' sana. Mambo wakati mwingine hubadilika kwa kasi usiyoitarajia

Kuna wale unawakuta wanakunja utadhani umeingia police kuhojiwa na sielewi wanafanya hivo ili iwe nini!

Mtu uko ofis fulani kuhudumia watu, halafu unajifanya kana kwamba wewe ni asikari, unakunja sura na kuwa mkali tu kama mbwa mbwekaji, tukueleweje sasa, si uache kazi au uwe police tujue moja?
 
Kuna mtumishi mmoja wa umma ana glass yake bar...
Asubuhi ofisini anaacha koti juu ya kiti....halafu huyoo bar...lete supu lete mchupa...kama unahitaji huduma unamfuata bar....mnamalizana....mpaka muhuri anakuwa nao bar..maaaamae🤯
Anakuwa ameshaagiza vyombo na supu kabisa ili ukienda kupata huduma ya kusainiwa form au kugonga mhuri unamlipia wakati huna mbele wala nyuma
 
🤣🤣 Namjua mtu cheochake Afisa elimu daraja la ll akikatwa bodi yamikopo anabakiwa na laktatu na anaishi na familia na ndugu
Labda kijijini lakini mjini hakuna rangi hutoona. Halafu kuna vile umefika halmashauri una shida fulani wanaanza kukuzungusha mara nenda pale ukienda pale unaambiwa nenda kule ukienda kule unaambiwa rudi nyuma kidogo ingia kushoto ukiingia kushoto anakuambia nenda mbele kidogo ingia kulia mlango namba 2 ukiingia namba 2 unakutana na kidada kimechoka halafu sura ngumu halafu anachati. Ukimsalimia anaitika bila kuinua kichwa huku bado yuko kwenye simu. Unamueleza shida yako anakwambia muhusika hayupo na haijulikani atakuwepo lini na wewe umetoka mbali zaidi ya Km 100 na umetumia nauli kibao. Pumbav zenu!
 
Naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…