Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

chilumendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,079
Reaction score
3,550
Wadau niombe msaada kihusu mada tajwa hapo juu. Nimekuwa napambana na ujenzi wa kibanda changu cha ndoto yangu kwa kipindi cha miaka mitano hivi.

Ilivyofika mwaka jana wakati wanapiga plasta nilikuta kitu kisichocha kawaida katika mchanga, nilimkuta sungura aliyechinjwa akiwa amefukiwa kwenye mchanga.

Tukio hilo nililipuzia nikamtupa huyo sungura kwa kumfukia kwenye shimo.

Mwezi huu tena baada kusimama ujenzi kwa muda mrefu nilianza kujenga fensi cha kushangaza kwenye msingi uliochimbwa tulikuta ngozi ya kondoo ikiwa imefukiwa napo nilipuzia

Kilichosababisha kuandika thread hii ni tukio la leo tumekuta kisu kilicho na damu pamoja na manyoya ya ndege kisu kikiwa na damu.

Niombe wadau walioexperience changamoto hiyo mlifanyeje. Lakini nini maana ya mauzauza hayo? Nini kinatafutwa

Kuhusu kiwanja niliuziwa na kijana mmoja ambaye naye alinunua kwa mmiliki, ambapo huyo kijana naye anaishi karibu na jengo langu ingawa miye sijahamia
 
Mimi hili hekalu langu nilikabidhiwa ndani ya miezi miwili tu baada ya kuwapa kampuni tenda ya ujenzi😎😎😎
09876543000.jpg
 
Unajenga mkoa gani, wilaya gan nk. Lakini watu wengi wakipata vipesa kidogo unaanza dharau sana kusalimia majirani, ubabe usio na msingi, kujiona umeyapatia maisha ndio wanaanza kukufanyia visa na mikasa ili ukome. Rekebisha na majirani wape hi, wasalimie saidia unapoweza then fanya mambo yako utaona fresh sanaa.
 
Mmmh miye ninaishi mbali na ujenzi unapofanyika, na ni mara chache sana kuwepo wakati ujenzi unafanyika yupo dogo ndiyo anasimamia
 
Kama mpaka leo upo hai na ujenzi wako unaendelea kadri ya unavyojimudu basi elewa haya yote ni mapicha picha tu.

Binadamu tuna kawaida za kutishana na kukatishana tamaa hasa kwenye mambo ya maendeleo.

As long as hujaguswa mwili wako wala kuathiriwa afya yako endelea na ujenzi wako. Hao wanakutisha tu, hakuna mwenye madhara. Ingekuwa mambo yenye nguvu basi usingefikia hapo ulipofikia. Msikilize Mch. Richard kwenye hiyo link hapo chini.

Kama mpaka leo upo hai na ujenzi wako unaendela kadri unavyojimudu basi elewa haya yote ni mazingaombwe tu.
Binadamu tu kawaida za kutishana na kukatishana tamaa hasa kwenye mambo ya maendeleo.
As long as hujaguswa mwili wako wala kuathiriwa afya yako endelea na ujenzi wako. Hao wanakutisha tu, hakuna mwenye madhara.
Asante mdau kwa ushauri
 
Mmmh miye ninaishi mbali na ujenzi unapofanyika, na ni mara chache sana kuwepo wakati ujenzi unafanyika yupo dogo ndiyo anasimamia
Sawa ila ukiwa unaenda weka unafki kwa majirani kidogo, unajua sisi weusi nuksi sana, yaani unapiga hatua kimaendeleo majirani wanavimba hasira so kuepusha wape hi kidogo, jifanye unawasikiliza ushauri wao nk yaani fast mauza uza yanaisha
 
Hizi nyumba hizi zina mambo, na mara nyingi wanakuaga ni watu wa jirani na hapo wanaofanya mauza uza

Mimi nlivonunua kibanda hichi balozi hakupenda sababu tuliuziana kwa kufata sheria, basi nlivoanza kukarabati ikawa anakuja kubeba udogo, yaan kila mafundi wakija na yeye lazima atie timu kubeba udongo.

Nikawa najiuliza uyu mtu anakuja kubeba udongo wa nini isitoshe udongo wenyewe ni mfinyanzi kabisa wakutengenezea vyungu na ilihali dar hatutengenezi vyungu.

Baada ya miezi miwili ukuta ukadondoka akawa anapita kusema mbovu kwa watu....nlichomfanya haji kunisahau maiaha yangu yote mwaka wa 4 huu nikipita njia hii na yeye anapita njia nyingine yaan ananikimbia
 
Sawa ila ukiwa unaenda weka unafki kwa majirani kidogo, unajua sisi weusi nuksi sana, yaani unapiga hatua kimaendeleo majirani wanavimba hasira so kuepusha wape hi kidogo, jifanye unawasikiliza ushauri wao nk yaani fast mauza uza yanaisha
Watu wabaya ni wabaya tu.Hata ukiamua kujipendekeza kwake atataka kukuumiza tu.Ukiumia kwake ni kicheko.Kujinyenyekeza au kuwa karibu nao sidhani kama ni jibu la haraka.
 
Usitumie uganga mana ni kampuni moja. Hata Kama ungenunua nyumba usipojua yaliyofanyika na Kama huna ujuzi na upuuzi mweusi itakutesa.
Wenzio washamaliza hapo wako pembeni wanasubiri kilio toka kwako.
Me niliwahi church kukomboa mji wangu.
 
Mmmh hatari
 
Ukipuuzia hakuna baya lolote utapata, ukiwaza na kuchukuliwa serious tegemea mabalaa mbele. Uchawi dawa yake ni kupuuzia. Ndio maana unashauriwa ukisikia usiku wachawi wanawanga au kucheza juu ya bati, toka nje kaa jifanye huna habari tena vuta na kiti kabisa chukua simu peruzi mtandaoni.

Wachawi wanapenda kutiliwa maanani, ukiwapuuzia hawana tena issue
 
Back
Top Bottom