Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

Ibada za kutakasa ardhi/makazi
 
Shamba la wafu
 
Wengi tumejenga, tunaishi kwenye mapito ya wachawi na wanga
 
Tiba zenye madhara
 
Wadau niombe msaada kihusu mada tajwa hapo juu. Nimekuwa napambana na ujenzi wa kibanda changu cha ndoto yangu kwa kipindi cha miaka mitano hivi.

Ilivyofika mwaka jana wakati wanapiga plasta nilikuta kitu kisichocha kawaida katika mchanga, nilimkuta sungura aliyechinjwa akiwa amefukiwa kwenye mchanga.

Tukio hilo nililipuzia nikamtupa huyo sungura kwa kumfukia kwenye shimo.

Mwezi huu tena baada kusimama ujenzi kwa muda mrefu nilianza kujenga fensi cha kushangaza kwenye msingi uliochimbwa tulikuta ngozi ya kondoo ikiwa imefukiwa napo nilipuzia

Kilichosababisha kuandika thread hii ni tukio la leo tumekuta kisu kilicho na damu pamoja na manyoya ya ndege kisu kikiwa na damu.

Niombe wadau walioexperience changamoto hiyo mlifanyeje. Lakini nini maana ya mauzauza hayo? Nini kinatafutwa

Kuhusu kiwanja niliuziwa na kijana mmoja ambaye naye alinunua kwa mmiliki, ambapo huyo kijana naye anaishi karibu na jengo langu ingawa miye sijahamia
Huo mtaa una wachawi wanakutisha usijenge komaa utamaliza ujenzi.Mimi wakati mafundi wanapiga plasta waliona snake[emoji216] akitoka ukutani kwenye plasta wakatoka nduki lkn nilimaliza ujenzi
 
Hiyo ni message inatumwa kwako Mkuu, ila inaonekana wanakushindwa, sasa shikia IMANI ulonayo kwa usawasawa, zidisha.
Hakuna mtu atachinja Sungura na kufanya hayo mengine yote kwa nia ya kukutisha, huyo/hao wanamaanisha Mkuu, ni muhimu kupeleleza kumjua muhusika ni nani na anataka nini kuna watu hawaachagi kufatilia, ukahamia akaendelea kubadilisha akajifanya jirani mwema kumbe nia anaijua yeye. USIPUUZE.
Asante nitafanyia kazi ushauri wako
 
Huo mtaa una wachawi wanakutisha usijenge komaa utamaliza ujenzi.Mimi wakati mafundi wanapiga plasta waliona snake[emoji216] akitoka ukutani kwenye plasta wakatoka nduki lkn nilimaliza ujenzi
Haha snake tena
 
Ni rahisi tu kama una imani kwa Yesu. Fanya hivi: chukua maji kwenye chupa, sali ukisema, kuanzia sasa haya si maji tena bali ni DAMU YA YESU kwa Jina la Yesu. Wao si walimwaga damu ya wanyama? Basi wewe mwaga Damu ya Yesu mahali hapo huku ukisema; Damu ya Yesu inanena mema matupu juu yangu, rudia mara nyingi. Weka imani kwa Yesu, kazi imekwisha, endelea na ujenzi na fanya hivyo mara kwa mara.
Asante sana kwa muongozo huu
 
Wadau niombe msaada kihusu mada tajwa hapo juu. Nimekuwa napambana na ujenzi wa kibanda changu cha ndoto yangu kwa kipindi cha miaka mitano hivi.

Ilivyofika mwaka jana wakati wanapiga plasta nilikuta kitu kisichocha kawaida katika mchanga, nilimkuta sungura aliyechinjwa akiwa amefukiwa kwenye mchanga.

Tukio hilo nililipuzia nikamtupa huyo sungura kwa kumfukia kwenye shimo.

Mwezi huu tena baada kusimama ujenzi kwa muda mrefu nilianza kujenga fensi cha kushangaza kwenye msingi uliochimbwa tulikuta ngozi ya kondoo ikiwa imefukiwa napo nilipuzia

Kilichosababisha kuandika thread hii ni tukio la leo tumekuta kisu kilicho na damu pamoja na manyoya ya ndege kisu kikiwa na damu.

Niombe wadau walioexperience changamoto hiyo mlifanyeje. Lakini nini maana ya mauzauza hayo? Nini kinatafutwa

Kuhusu kiwanja niliuziwa na kijana mmoja ambaye naye alinunua kwa mmiliki, ambapo huyo kijana naye anaishi karibu na jengo langu ingawa miye sijahamia
Nyumba ya ma angu mdg ilianzaga mauzauza kama hayo kabla aijaisha.......ilivoisha usiku watu wakilala wanatekenywa badae ikaja kutokea majoka mawili makubwa............alafu yakapotelea ndani.......wakaleta watu wa maombi usiku tukasikia kishindo nje asubui kukuta rundo la furushi limekaa irizi tukazimwagia mafuta ya taa tukachoma zikagoma kuwaka Mchungaji akaomba tena ndo zikawaka........hyo nyumba nishawai kupapaswa na limtu usiku nlitoka na neti hadi kweny taa na Kuna siku nmelala nkaanza kuvutwa ukutani na mazombie wacha nipige kelele kumbe watu hawanisikii..... nlitoka nduki hua naenda mchana jion nageuza kwangu............ wachawi ndo hua wanaanza hivohivo ukijifanya kupuuzia ukimaliza kujenga hyo nyumba ndo utajua mazombie tz yapi mengi ushauri wangu fanya maombi yani fanya maombi toa na sadaka
 
Achana nao hao wajinga wanakutisha ili ukijaa wakutapeli,

Mimi nilikuta mavitu ya ajabu ajabu hivyo hivyo nikawa nawaambia vijana wayatupe siku moja mtu akaja akadai amesikia tetesi nakuta mambo ya ajabu basi anipeleke kwa mtaalam nikazindike nikamuuliza kwani ujenzi hauendi au unaenda? kuna mtu kaumia au wote wazima basi sina huo muda, akaondoka zake na ikawa mwanzo na mwisho kuona huo upuuzi hadi tumemaliza,

Juzi kati tena kuna mtu alikua anauza nyumba yake, dalali akadai hawezi kuiuza wameifunga anatakiwa apeleke mtaalam aifungue, akatafuta dalali mwengine na nyumba iliuzika bila wasi.
 
Wadau niombe msaada kihusu mada tajwa hapo juu. Nimekuwa napambana na ujenzi wa kibanda changu cha ndoto yangu kwa kipindi cha miaka mitano hivi.

Ilivyofika mwaka jana wakati wanapiga plasta nilikuta kitu kisichocha kawaida katika mchanga, nilimkuta sungura aliyechinjwa akiwa amefukiwa kwenye mchanga.

Tukio hilo nililipuzia nikamtupa huyo sungura kwa kumfukia kwenye shimo.

Mwezi huu tena baada kusimama ujenzi kwa muda mrefu nilianza kujenga fensi cha kushangaza kwenye msingi uliochimbwa tulikuta ngozi ya kondoo ikiwa imefukiwa napo nilipuzia

Kilichosababisha kuandika thread hii ni tukio la leo tumekuta kisu kilicho na damu pamoja na manyoya ya ndege kisu kikiwa na damu.

Niombe wadau walioexperience changamoto hiyo mlifanyeje. Lakini nini maana ya mauzauza hayo? Nini kinatafutwa

Kuhusu kiwanja niliuziwa na kijana mmoja ambaye naye alinunua kwa mmiliki, ambapo huyo kijana naye anaishi karibu na jengo langu ingawa miye sijahamia
Usiwe mwoga mkuu.
Kama imani yako iko sawasawa hakuna lolote la kukudhuru.

Wewe mwamini na kumwomba Mungu, anayetulinda siku zote.

Inaelekea hapo wewe una jirani anataka kukutisha ukimbie umwachie ardhi.

Mimi nimekutana na paka ameingia ndani ya nyumba yangu, alinisumbua wiki tatu ansingilia nisipopajua.
Liliponichosha nikaliua.
Siku chache baadaye kukawa na msiba jirani, hata hivyo sikuunganisha huo msiba na lipaka.
Vyovyote vile sikusumbuliwa tena.

Mungu anatulinda katika mengi.
 
Mimi site kwangu Tegeta, walikuwa wanavunja nazi pia wanakunya na kuacha vimimika kwenye chupa zenye maandishi ya kiarabu ya rangi nyekundu.

Nilimtafuta jamaa yangu, tukaenda kununua kondoo tukaja nae site akiwa amefungwa kitambaa cheusi shingoni tukamfunga kwenye mti mbele ya site.

Usiku saa sita tukachimba shimo kondoo tukambana korodani akapiga kelele sana,
Tulipohisi majirani wamesikia zile kelele.
Tukachukua majani tukafukia ktk shimo.

Kondoo tukamtia kwenye buti ya gari tukaondoka, kesho yake tukamchinja tukamchoma, na supu ya kutosha,
Waliogopa hata mafundi wakisahau vifaa asubuhi wanavikuta,

Toka siku hiyo sijaona upuuzi tena,
 
Habari Mkuu... Nimesoma changamoto yako kiukweli hayo mambo yapo na wengi humu watapuuza ila kuna vitu ambavyo watu wengi tunavipuuza tunaponunua aidha Ardhi, au Gari au Kitu chochote ambacho kimepita kwenye mikono au macho ya wamiliki tofauti??

Siku zote Ukinunua ardhi kutoka kwa mtu ambaye siyo Mimlki wa ardhi hiyo tafadhari ikomboe hiyo ardhi iwe ndani ya na ikubali kupokea Jina lako kama Mrithi wa halali.. Kumbekeni ardhi inaweza kuwa na fungamano na mambo ya urithi ambayo ukiinunua yale mambo yataendelea kutokukutambuwa bali yanamtambuwa mumilik wa aawali aliyekuwa analihudumia..

Jamani hakuna Mila yoyote duniani isiyokuwa na Mila na Desturi zake. Hata hao mnaowasema kuwa ni wazungu wana mila zao.

Ushauri wangu kwenye hilo.. Mtafuta mimiliki wa awali siyo huyu kijana aliyekuuzia. Nenda Muite mahala Mwambie mimi ndiye nileyenunua ardhi yako uliyokuwa umemuuzia fulani ila naona kama ujenzi unasuasua naomba uniruhusu hii ardhi iwe ndani ya Ukoo wa Jina langu.. Hakika atakwambia maneno mengi na ataifungua hiyo ardhi na hautakuta hayo mauza uza yoyote.

Haujawahi kusiki Mtu ananunua mifugo kama muuzaji siyo Mumiliki halali wa huo mfugo huyo mfugo utatoroka na kurudi uliko kulia... Mifano halisi Mbwa na Ng'ombe........
Hayo ni Machache tu.

Mfano wangu Nilinunua eneo sehemu ambayo ni very potential huku Dodoma (wagogo na Warangi Mnawajua) tena kwa bei nafuu sana.
Nilimtafuta mmiliki wa ardhi wa awali nikamwambie anikabidhi ardhi yake kutoka kwenye ukoo wake na ardhi iwe ndani ya uumiliki wangu alicheka sana akasema wewe mjanja sana mwenzio ameshindwa kuliendeleza nikasema najua hizi mali zina maagano kwa hiyo lazima maagano yavunjwe
 
Back
Top Bottom