GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kuna muda huwa nawashangaa sana kama siyo mno Watanzania kwamba ni kwanini hawataki Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ' Zawadi ' ya Rais ambaye ana ' maono ' makubwa sana ya Kimaendeleo kama aliyonayo Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.
Kwa wale Ndugu zangu ambao mmekuwa mkipiga Kelele juu ya Ununuaji wake wa Ndege ili kuweza kuzidisha Kasi ya Utalii nchini nadhani kwa hili alilolifanya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta sasa mtakuwa na la Kujifunza na ikibidi bado hamjachelewa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais JPM au Kutengua ' Kauli ' zenu kwani kiukweli Rais JPM yupo sahihi kwa 100% na hizi Ndege anazozinunua zitaongeza mno Ukuaji wa Uchumi na hasa Sekta nzima ya Utalii kwa nchi ya Tanzania.
Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza.
Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema kwamba uzinduzi huu wa hii Safari ya moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani ( USA ) kutaongeza maradufu ' mapato ' katika Sekta nzima ya Utalii ya nchini Kenya na pia Uchumi wa nchi yake utakuwa kwa haraka kwakuwa Kenya imekuwa na ' Vivutio ' vingi ambavyo Wamarekani wengi hupenda kuvitembelea mara kwa mara.
Bado nitasema na leo nasema tena bila ' Unafiki ' kwamba kama kuna ' Zawadi ' ambayo Mwenyezi Mungu ametupa Watanzania basi ni kwa kutupatia Rais mwenye maono ya kweli, yenye tija na uhakika wa Kimaendeleo kwa nchi hii Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.
Hakuna Rais ninayempenda na kumkubali kama JPM na Mwenyezi Mungu ambariki sana azidi kutuletea Maendeleo Watanzania.
Source: Daily Monitor
Nawasilisha.