Wewe umechangia vizuri sana ninakupongeza sana kwa hilo. Kaka tatizo kubwa tulilonalo sisi waafrica wengi ni kuangalia upande mmoja zaidi wakati wa mikosoa au kuunga mkono hoja, kwa mfano nilitegemea wewe inayesema kipaumbele kiwe kilimo, nilitegemea useme nini ambacho alipaswa rais akifanye katika kilimo ili uone kweli serikali imetoa kipaumbele ktk kilimo.
Ununuzi wa ndege ni kitu cha mara moja sana, ukiwa na pesa unaweza kununua na ikaonekana kwa muda mfupi, ila kilimo hata kama una pesa, bado unahitaji mambo mengi ili kilimo kiweze kuonyesha mafanikio chanya, kwa hiyo muda, utaalamu na miundombinu vinahitajika sana.
Kwa mfano, hadi sasa serikali imetumia chini ya $600 kununua ndege zote 7, hii ni chini ya 25% ya bajeti ya Wizara ya kilimo, ukipngeza na pesa za wahisani wanaochangia kilimo na uvuvi, kwa sasa wizara ya kilimo na uvivi ina zaidi ya $3B hazijatumika, Bank ya Kilimo imepewa pesa nyingi ili iwakopeshe wakulima lakini wamezikalia, juzi Magufuli alisema kama mkurugenzi mtendaji wa hiyo Bank ameshindwa kazi afukuzwe, Serika imetoa pesa nyingi sana kwa TIB ili kukopesha watanzania wanaotaka kuzalisha ktk kilimo, uvuvi na ufigaji, nenda TIB upate maelezo ya kina. Sasa unataka serikali ijiingize moja kwa moja ktk kilimo au ulitaka ifanye nini ili uone kwamba kweli kilimo ni kipaumbele cha serikali?.