Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

Watu 7000 wajiandikisha au wamekata ticket kuwemo kwenye safari hiyo ya kwanza? Yaani Kenya hata wangerusha dreamliner zote nane kwenda JFK bado haziwezi beba watu 7000

Another CERTIFIED IDIOT!
 
Another CERTIFIED IDIOT!
Agreed, maana ni ngumu kuelewa maana ya safari ya Kwanza .najua KQ watakuwa wakifanya daily flights to JFK and so abiria 7000 maana yake KQ JKIA to JFK flight is full booked mwezi mzima
 
Tununua Ndege bila leseni ya IATA ni tatizo, zitaendelea kupaki tu!
 
Tununua Ndege bila leseni ya IATA ni tatizo, zitaendelea kupaki tu!

' Tununua ' ndiyo Kiswahili cha wapi hiki? Sasa kama Kiswahili tu ambacho ni chepesi kinakusumbua hivi je mambo mazito kama haya yanayohitaji upeo mkubwa / akili kubwa utayaweza kweli?
 
Akili zako zitakua sio nzuri labda una kasoro, Kenya ina uchumi mkubwa Mara 3 ya Tz?? Aisee! Hebu Lete proof
 
Akili zako zitakua sio nzuri labda una kasoro, Kenya ina uchumi mkubwa Mara 3 ya Tz?? Aisee! Hebu Lete proof

Mbona naona kama vile haya maneno uliyoyaandika hapa yanakuhusu Wewe mwenyewe Mkuu japo Wewe unadhani umemwambia huyo ' Member ' mwingine?
 
Maneno meengi, alafu yote hovyo
 

Mbona naona kama vile haya maneno uliyoyaandika hapa yanakuhusu Wewe mwenyewe Mkuu japo Wewe unadhani umemwambia huyo ' Member ' mwingine?
Basi nyote akili zenu ni 0% uchumi wa Kenya ni 85Billion Dollars GDP na Tanzania ni 56 Billion Dollars GDP hiyo mara 3 inatokea wapi? Kenya mwaka Jana kwenye tourism imeingiza 1.2 billion Dollars Tanzania imeingiza 2.3 Billion Dollars na Utalii ulikua kwa asilimia 12 na Kenya ulikua kwa asilimia 20% sasa huyo anachopotosha ujinga hapo ni Nini? Eti Kenya imekita mizizi kwenye utalii wakati mwaka Jana Status ya Region Tourism hub imekuja Tanzania badala ya kumpiku Mkenya. Upuuzi mtupu
 

Sasa usingechokozwa ' Kitaalam ' huu ukweli na haya maujuzi yote yaliyosheheni ' data ' ungeyatolea wapi ili Watanzania wenzako wajue? Hapana ' chezea ' GENTAMYCINE Wewe na siku zote nikilitaka langu huwa linakuwa na kwa majibu yako haya nadhani kwa 95% umenipa kile nilichokuwa nikitaka Kujiridhisha nacho.
 
Wewe ni miongoni mwa watu wa hovyo humu ndani kuwahi kutokea, sipaswi kutumia maneno makali kama ulivyotumia wewe, lakini niruhusu nikuite mbumbu na mjinga sana, Kenya na Tanzania nani anaongoza katika kuvutia na kupata pesa nyingi za utalii?.

Kwa taharifa yako Tanzania imechaguliwa mara tatu mfululizo kuwa nchi inayoongoza kwa vivutioa vya utalii hapa Africa, tunashindana na South Africa na Botswana tu ktk ukandaa huu, kumbuka hizo nchi mbili utalii upo mikononi mwa wazungu waliwekeza sana tangu enzi za ukoloni
 
Tumia busara ya kiafrica inayosema, Mwenye hekima huijaza akili yake kwanza kabla ya kufungua domo lake. Hivi ni nchi gani inayoanza biasha ya usafiri inayoweza kuanza na direct international route bila kuwajaribu wafanyakazi pamoja na ndege zake kwa kufanya domestic routes kwanza?.
Kenya inapata hasara kila mwaka na wanashindwa kulipa mikopo iliyokopwa na KQ hadi rais anaingilia kati na kulazimisha Bank kubadili madeni wanayoidai KQ kuwa share kwa lazima, huo umbali unaodai KQ ni shirika kubwa unatumia vigezo gani? au unatumia miaka mingi ya kufanya biashara?
 
Wewe umechangia vizuri sana ninakupongeza sana kwa hilo. Kaka tatizo kubwa tulilonalo sisi waafrica wengi ni kuangalia upande mmoja zaidi wakati wa mikosoa au kuunga mkono hoja, kwa mfano nilitegemea wewe inayesema kipaumbele kiwe kilimo, nilitegemea useme nini ambacho alipaswa rais akifanye katika kilimo ili uone kweli serikali imetoa kipaumbele ktk kilimo.

Ununuzi wa ndege ni kitu cha mara moja sana, ukiwa na pesa unaweza kununua na ikaonekana kwa muda mfupi, ila kilimo hata kama una pesa, bado unahitaji mambo mengi ili kilimo kiweze kuonyesha mafanikio chanya, kwa hiyo muda, utaalamu na miundombinu vinahitajika sana.

Kwa mfano, hadi sasa serikali imetumia chini ya $600 kununua ndege zote 7, hii ni chini ya 25% ya bajeti ya Wizara ya kilimo, ukipngeza na pesa za wahisani wanaochangia kilimo na uvuvi, kwa sasa wizara ya kilimo na uvivi ina zaidi ya $3B hazijatumika, Bank ya Kilimo imepewa pesa nyingi ili iwakopeshe wakulima lakini wamezikalia, juzi Magufuli alisema kama mkurugenzi mtendaji wa hiyo Bank ameshindwa kazi afukuzwe, Serika imetoa pesa nyingi sana kwa TIB ili kukopesha watanzania wanaotaka kuzalisha ktk kilimo, uvuvi na ufigaji, nenda TIB upate maelezo ya kina. Sasa unataka serikali ijiingize moja kwa moja ktk kilimo au ulitaka ifanye nini ili uone kwamba kweli kilimo ni kipaumbele cha serikali?.
 
Tanzania ni taifa la wendawazimu kabisa,halafu kuna mtu anauza mchicha kijijini halafu anafurahia kununuliwa ndege,wakati hana hata cent ya kwenda Dar .
Mkuu acha kupanda hayo mandege ya mitumba ni hatari.
Wewe ndiye unaeongoza kwa uwendawazimu, huna unalojua zaidi ya kupiga kelele hovyo, wewe unadhani unaweza kushindana na dunia nzima ambapo ripoti za mashirika yote ya kimataifa zinaipongeza Tanzania ukiacha kipengele cha freedom expression
 

Nakupongeza kwa mchango huu maridhawa. Tujikite kwenye kilimo maana mimi ni mkulima. Naona umetaja kiwango ambacho kiko kwenye kilimo, na unasema kuna bank kama TIB ziko hela. Je unajua mlolongo wa kuzipata hizo hela au unaongea nadharia? Naona wewe unaongea nadharia wakati mimi nimekutana na hali hiyo kwa uhalisia wake. Kwa jambo usilolijua ni vyema kukaa kimya tu. Je unajua bei ya pembejeo kama mbolea, ubora wa mbegu, viuatilifu nk? Je unajua bei tunayokutana nayo sokoni kulinganisha na gharama ya hicho kilimo? Hivi unajua niko mahali ambapo tracktor inabidi nilikodishe kutoka kilomita zaidi ya 50? Kibaya zaidi wakati unataka kukodisha, huko lilipo ni changamoto hata kulipata. Sisi kama wakulima tulitarajia zile 50m@kijiji tungezipata wangalau kwenye tarafa yetu tungepata tractor mbili ili tuondokane na hiyo dhahama, kwa bahati mbaya hilo limekuwa ahadi kama ahadi nyingine hewa tulizowahi kukutana nazo. Nikushauri ndugu yangu, hebu jikite kwenye jambo unalilifahamu kuliko kuleta utetezi wa kisiasa kwenye hili suala la kilimo. Angalie signature yangu utajua kwamba ninajua ninaloongea kwenye kilimo.
 
Kaka umeleta mada ili tuchangie sio kuleta vitisho, mimi ni mkulima wa miaka mingi sana inawezekana kukuzidi wewe, lete hoja zijibiwe hapana kuleta vitisho.

Nimekuuliza ulitaka serikali ifanye nini katika kilimo, badala ya kutoa ushauri wewe unakazania kuniuliza maswali ya kipuuzi kwamba inajua bei ya pembejeo au kuhusu mlolongo wa kuzipata hizo pesa za TIB, sasa ulitaka ukifika tu Bank wakurushie hizo pesa?, mikopo yote lazima iwe na masharti ili kuhakikisha kweli mtu anayetaka hizo pesa atazitumia kwa malengo husika.

Sharti kubwa la kukopeshwa pesa za TIB ni lazima uwe umeshaanza kilimo cha mazao ambayo yapo katika orodha yao, shamba liwe na hati na iwe katika kanda husika, watakuja kulikagua na kuangalia kama umetimiza vigezo vya kukopeshwa, sasa unataka nini zaidi, mimi nilienda na nilikopeshwa, japo sio kwa kiwango nilichoyaka.

Kuhusu 50M, huna lolote wewe ni miongoni mwa matapeli tu, kwasababu umesikia kuna pesa basi akili yako imechanganyikiwa, sema ukweli ni kitu gani cha maendeleo kinaweza kufanyika ktk vijiji vyetu kwa mtaji wa 50M, kama sio kukopeshana ktk vikundi vidogo vidogo vya mama ntilie, hivi yale mabilioni ya Jakaya yaliyotolewa yalitumikaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…