Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

Kaka umeleta mada ili tuchangie sio kuleta vitisho, mimi ni mkulima wa miaka mingi sana inawezekana kukuzidi wewe, lete hoja zijibiwe hapana kuleta vitisho.

Nimekuuliza ulitaka serikali ifanye nini katika kilimo, badala ya kutoa ushauri wewe unakazania kuniuliza maswali ya kipuuzi kwamba inajua bei ya pembejeo au kuhusu mlolongo wa kuzipata hizo pesa za TIB, sasa ulitaka ukifika tu Bank wakurushie hizo pesa?, mikopo yote lazima iwe na masharti ili kuhakikisha kweli mtu anayetaka hizo pesa atazitumia kwa malengo husika.

Sharti kubwa la kukopeshwa pesa za TIB ni lazima uwe umeshaanza kilimo cha mazao ambayo yapo katika orodha yao, shamba liwe na hati na iwe katika kanda husika, watakuja kulikagua na kuangalia kama umetimiza vigezo vya kukopeshwa, sasa unataka nini zaidi, mimi nilienda na nilikopeshwa, japo sio kwa kiwango nilichoyaka.

Kuhusu 50M, huna lolote wewe ni miongoni mwa matapeli tu, kwasababu umesikia kuna pesa basi akili yako imechanganyikiwa, sema ukweli ni kitu gani cha maendeleo kinaweza kufanyika ktk vijiji vyetu kwa mtaji wa 50M, kama sio kukopeshana ktk vikundi vidogo vidogo vya mama ntilie, hivi yale mabilioni ya Jakaya yaliyotolewa yalitumikaje?

Wwe sio mkulima ni muuza face hapo Dar. Sioni kama una jipya bali unauza maneno hapa jukwaani. Hayo masharti wewe hayawezi kukuhusu maana dada yako kaelewa na manager wa bank.
 
Wwe sio mkulima ni muuza face hapo Dar. Sioni kama una jipya bali unauza maneno hapa jukwaani. Hayo masharti wewe hayawezi kukuhusu maana dada yako kaelewa na manager wa bank.
Wewe ni tapeli tu huna hoja zaidi ya kulalamika bila kutoa ushauri wa nini kifanyike, wewe endelea kulalamika na kusugua makalio vijiweni matokeo utayaona
 
Mkuu GENTAMYCINE hongera kwa uzi na ninakupongeza sana kwa utetezi wako kwa JPM. Naheshimu michango yako kwani huwa sio mnafiki na huwa unanyoosha bila kupindisha hata Mavunde hilo analijua.

Tuje kwenye mada yako, nionavyo kuna upotoshaji wa wazi kwenye wanaomkosoa JPM kwa kuwekwa kwenye kundi la kumpinga japo sio kosa hata akipingwa, upotoshaji huu unafanyika kwa makusudi ama pasipo au kwa kufuata mkumbo. Tuko sisi tuliosema na tutaendea kusema na kukosoa bila kuyumbayumba kwani tunachosimamia tunakiamini. Tulisema ndege ni jambo jema, lakini kwa hali za walio wengi hapa nchini ambao ni wakulima ni vyema kipaombele kingekuwa kwenye kilimo. Mimi ama wanaoamini kwamba kilimo kilipsawa kuwa kipaombele kisha ndege baadae, ni kwamba tungeleta maendeleo ya watu kwanza, kisha maendeleo ya vitu. Iwapo ingetokea kwamba tuliokosoa kununua ndege kwanza tungeenda kuilipua hapo sawa, lakini tumetumia haki yetu ya kukosoa na kusema kipi kilipaswa kuwa kipaombele kosa letu liko wapi?

Inaonekana ww na mashabiki wake na hata yeye mwenyewe mnakwepa hoja zetu za ukosoaji kwa kichaka cha kupingwa, na hamtumii neno ukosoaji bali huwa mnasema kumpinga rais ili mpate public sympathy. Na kwa bahati nzuri hilo neno ya kwamba rais anapingwa kwa kila jambo linaenea vizuri bila wananchi kupata upande wa pili maana sasa hivi kinachosikika kwenye media ni atakacho rais. Huku kwenye mitandao pakee ndio kumebaki na mijadala huru kama hivi. Msipotoshe japo mna haki ya kumtetea mpendavyo na sisi tuna haki ya kumkosoa tupendavyo kwani ndio demokrasia as long as hakuna anayekwenda kuharibu hiyo miundo mbinu.
Ebu nikuulize swali, ukisha peleka fedha hizo kwa wakulima kisha unafanya nini, unakaa kibwege tu. Kesho utawapelekea nini. Ndege, meli, reli, barabara, utalii, kilimo, uvuvi, ufugaji ,madini, viwanda, n.k. vyote hivi ni nyenzo za kukusanyia fedha ili ukizipata ndipo sasa unaweza kutekeleza vipaumbele vyako kikiwemo kilimo, Elimu, maji na huduma zingine za jamii. Usipofanya hivyo basi wewe utakuwa MTU Wa kutegemea mikopo tu kutoka nje ambapo Matokeo yake tunajua ni kuiweka nchi yako rehani.
 
Tatzo sio ndege bali ni sheria ya manunuzi, bunge lilihusishwa mkuu?

Bunge lilishawahi kukufanyia nini licha ya kula pesa yako kwenye vikao na majimboni hawafiki wanafiki wakubwa. Tukiwa na rais kama JPM hatuitaji wabunge wanafki ambao walitumia billions of TZS Kuandika katiba hewa wakafie mbali!!!! Au ww babako mi mbunge unataka vikao ili mpate posho???
 
Bunge lilishawahi kukufanyia nini licha ya kula pesa yako kwenye vikao na majimboni hawafiki wanafiki wakubwa. Tukiwa na rais kama JPM hatuitaji wabunge wanafki ambao walitumia billions of TZS Kuandika katiba hewa wakafie mbali!!!! Au ww babako mi mbunge unataka vikao ili mpate posho???
Unajua maana ya Bunge mkuu? Wabunge ni wawakilishi wa wananchi ikiwemo wewe mwenyewe! Na ndo mawaziri wa Serikali yetu Unaposema wabunge ni wanafiki ina maana unamaanisha wananchi wote ni wanafiki pamoja na wewe! Na kama unasema Rais pekee anatosha basi tufute bunge na abaki mwenyewe tu
 
Back
Top Bottom