Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mi kipato changu kikubwa mara nyingi tu zaidi ya hicho ila home hatunywi chai ya 3000 mi na wife, duh
 
Yani mimi tu peke yangu bila family haitoshi kabisa,

Labda nipige dash asubuhi na mchana.

Hiyo 10,000 ni kama nauli na vocha tu.

Ila life liko tofauti sana aisee,kuna watu wanajua ku budget hiyo mtu hadi anasave kabisa.
vocha zina faida gani kwako?
 
Mwana nimekukubali sana
 
Ila kodi ya nyumba umeisahau
 
Ila kodi ya nyumba umeisahau
Hapo asqueze kwenye gharama za mboga na anunua dagaa robo 2000 ambayo inaweza ikasave kwenye mboga,na pia mboga bamia na nyanya chungu ,mboga za majani atasave anaweza akapata kodi hata ya 60,000/=
 
Haya maisha tunayajua tusio mipesa.

Pamoja na yote mkuu, lazima ujifunzd ku-save kabla ya ku-spend. Jiwekee kanuni kwanza kuwa wewe kila mwezi una-save mfano 10K, 20K au 50K kwenye fixed account, halafu inayobaki ndio unatumia kwa mahitaji yako na familia.

Enzi za utoto nilikuwa nawashangaa sana wazee wanaovaa viatu lakuchumpa, wengine soli imeisha upande na hajali, wengine shati limepauka analo tu, wengine suruali inakiraka hajali, usafiri baiskeli, simu kitabani, wakati anafanya kazi na anapata pesa. Lakini kadri umri ulivyoongezeka nikaanza kuelewa kuwa, lazima tujifunze kuyapa kipaumbele mambo ya msingi, mfano kununua kiwanja au kujenga kabisa, kulipa ada za watoto, kutoa sadaka, kumsitiri mke na watoto, mashamba nk.
 
Kuna hotuba moja ya enzi za "Fagio la Chuma" za utawala wa rais Ali Hassan Mwinyi, alielezea jinsi maisha ya ndugu yake mmoja, aliyekuwa mfanyakazi wa serikali, yalivyomfundisha somo kuhusu maisha ya watumishi wa serikali.

Yule ndugu yake rais Mwinyi alikuwa mfanyakazi wa serikali, kuna mambo fulani yaliharibika chini yake, akawekwa kwenye uchunguzi. Sasa katika uchunguzi huo, alitakiwa asiwe kazini. Lakini mshahara analipwa kama kawaida mpaka uchunguzi ukamilike.

Sasa yule bwana akamuendea ndugu yake, rais Mwinyi. Akamlalamikia, akasema ameonewa, akamsihi rais Mwinyi amfanyie mpango arudishwe kazini.

Rais Mwinyi akamuuliza, lakini wewe si unafanyiwa uchunguzi tu, na mshahara wako unalipwa wote kama zamani?

Yule ndugu yake Mwinyi akasema ndiyo, mshahara nalipwa, lakini Ami ujue watu hatuishi kwa mshahara tu mjini hapa. Nikiwa kazini kuna mbinu nyingi za kuongeza kipato. Nikiwa simo kazini sina ujanja naishia kwenye mshahara tu.

Kwa maneno mengine, alikuwa ana uwezo wa kupata fedha nyingi za rushwa akiwa kazini, kwa hivyo, mshahara mdogo haukuwa tatizo.

Rais Mwinyi alieleza kisa hiki kuonesha tatizo la rushwa serikalini.
 
Mtoa Post ukimfatilia utakuta ndo kapata kazi kapewa milioni 1 anaona ndo mshahara mkubwa.
 
bado hujapiga bajeti ya watoto shuleni,tufanye and watoto wawili mmoja anasoma while ya msingi na mwingine anasoma shule ya awali ambayo Kila mwezi lazima awe analipa ada,inawezaje kumtosheleza kwa laki tatu?
 
Issue ni kupangilia matumizi yako ya pesa, kuacha matumizi yasiyo na msingi na kufanya yale matumizi ya lazima bas! na kama itatokezea itabaki basi save kwenye account.
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Mi napata 588,150 after deduction na sijaoa lakini haunitoshi kabisaa...wiki ya kwanza tu ya mwezi unakuwa umeisha...sasa hawa wa 300,000 sijui wanafanyaje kweli nimeamini kila mtu na akili zake.
 
Mshahara wangu 300,000 kwa maisha ya kupanga nitakwama kodi tu ila mipango inakuwaga hivi:
120,000 nampa mke wangu Happy abajetie mboga na maji kwa mwezi mzima
80,000 nabajetia umeme, matunda na nauli za Kanisani pamoja na Sadaka
100,000 nanunua unga, mchele, maharage, sabuni na vocha vocha
Hela ya kodi ya nyumba tunaipata kwenye biashara yetu. Nadhani tukijjenga tutapunguza gharama.
 
Mimi nishaishi Dar kinondoni nnaenda kuparangana K. Koo nnapata buku tatu, tano na siku ingine unapiga deshi na nlikua nnaishi, saahizi nimepata nnakaa nyumba kodi tu kwa mwezi laki 3, umeme sio chini ya 50, maji sio chini ya 20, hapo bado familia hajala vizuri wala kufua, na maisha yanasonga fresh tu, issue ya kipato inategemea na mipango na kupanga badget kulingana na ulichonacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…