Nimeona watu wanasema tu inatosha inatosha bila kutoa mchanganua wa hiyo laki 3 utaitumia vipi?
-Mtoa mada amesema una mke na watoto utawezaje kuibalance hiyo laki 3 na kutosha kabisa?
-Mie natoa direction mpeni mchanganua wa kutumia hiyo laki 3 eg
-Apange vyumba vya Tsh ngapi?
-Mchana ale asubuhi na mchana ale nini akiwa kazini? Nauli?
-Kodi ya meza aache Tsh ngapi na wawe wanaitumia vipi kwa mlo wa asubuhi,mchana(mkewe) na Usiku(famillia)
-Watoto wanasoma chai asubuhi na hela ya kununua mihogo,aisikilimu akiwa shuleni(mtoto hawezi kukaa na njaa mpaka saa tisa ndio aje kula nyumbani)
-Matumizi ya umeme,maji,sabuni(kufua ,kuogea).
Mchanganuo wangu:-
-Awe ananua vitu kwa jumla eg kiroba cha unga cha kilo 5(7,500/=),Mchele kilo 10 wa 1800(18,000),Nyanya kisado (5000),Vitunguu kisado(elfu 6),Mafuta ya taa(elfu 20),mafuta ya kupikia(lita 5 elfu 15),Kiroba cha mkaa(kilo 25 , Tsh 15000)
Hapo Jumla ni 80,000/=
-Baada ya hapo awe anaacha elfu 4 tu ya mboga kila siku kwa Mwezi jumla ni 120,000/=
-Na yeye bajeti yake kwa mwezi awe anatumia elfu 3 kwa siku ,chai atumie za kwenye dispensa ofisini awe ananunua tu chapati mbili za 500 au 600 na mchana msosi wa buku jero na nauli 800 kwahiyo bajeti yake itakuwa elfu 60,000/= kwa mwezi(20 working days)
-Hiyo 40 iwe ni gharama za umeme na maji na vitu vigogo vidogo.