Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Take home 300,000/=

Means kwa siku matumizi yao yasizidi 10,000/= mtafutaji pamoja na familia yake...

It's a hustle kwa kweli... wanakuaga na maisha magumu sana, kila kitu kwao anasa...

Mgeni akija wananuna...


Cc: mahondaw
Shidaa...
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Kabla ya kukujibu, jibu kwanza hili, kupokea huo mshahara unakuwa kwenye nyumba ya kupanga? nyumba hiyo iko Kariakoo au Tegeta au Goba au wapi jibu kwanza ndio utapata ufafanuzi nafahamu kwa mjini nyumba tu yenyewe ya kupanga vyumba viwili na sebule itakupa taabu sana maana una watoto
 
Uwe na mwanamke anayefanya kazi na yeye labda ndo iyo pesa ndo itatosha vijana wengi waliochangia uzi huu inaonekana wapo kwa wazazi hiyo pesa haitoshi kabisa hiyo ni hela ya kodi,na bili za maji na umeme chenji inayobakia ni nauli tu na vocha
 
ndio maana nikauliza
 
Yani mimi tu peke yangu bila family haitoshi kabisa,

Labda nipige dash asubuhi na mchana.

Hiyo 10,000 ni kama nauli na vocha tu.

Ila life liko tofauti sana aisee,kuna watu wanajua ku budget hiyo mtu hadi anasave kabisa.
wa bukoba huyu
 
Uwe na mwanamke anayefanya kazi na yeye labda ndo iyo pesa ndo itatosha vijana wengi waliochangia uzi huu inaonekana wapo kwa wazazi hiyo pesa haitoshi kabisa hiyo ni hela ya kodi,na bili za maji na umeme chenji inayobakia ni nauli tu na vocha
wengi wanachukulia utani
 
Pesa haijawah kumtosha mtu hata wanaolipwa mamilions Bado hawaridhiki.

Kikubwa ishi kulingana na kipato chako. Kuanzia kwenye malazi ,chakula na mavazi.

Mfano uswazi Kuna vyumba mpk 20000 kwa mwezi. Chakula mitaa hiyo siyo gharama. Ila km unataka kubanana town lazma jasho likutoke kwa pesa hiyo.
 
Mimi nimewahi kufanya kazi mahala fulani (part time) maeneo ya ubungo, nikipokea hiyo laki 3 napanga kabisa kuwa nitakunywa bia za 6,000 tu nipoze koo, ili niamke na 290,000. Matokeo yake naamka na 250.
Ndani ya wiki 2 sina hata 100 ya nauli, naanza kwenda kazini kwa kutumia chanzo kingine cha mapato.
Kwa kweli kama mtu hana chanzo kingine cha mapato na anategemea mshahara wa laki 3 kuendeshe maisha, nampa salute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…