Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Aisee,bila akili ya ziada unaweza kufa maskini yaani.Lakini hyo ndo take home ya ndugu zetu walimu wa shule za misingi.sijui wanaishije,
 

Nadhani tunatofautiana maisha, mimi japo mshahara wangu ni zaidi ya hapo ila matumizi ya nyumbani hayazidi 7,000 labda siku moja moja tu niamue,huwa nikitoka kazini napita sokoni nanunua mihogo au viazi vya buku vikichemshwa vinatosha kabisa.
 
Nadhani tunatofautiana maisha, mimi japo mshahara wangu ni zaidi ya hapo ila matumizi ya nyumbani hayazidi 7,000 labda siku moja moja tu niamue,huwa nikitoka kazini napita sokoni nanunua mihogo au viazi vya buku vikichemshwa vinatosha kabisa.
Kweli mkuu huo ndio uhalisia ukiacha 7000 maisha yanaenda poa tu
 
Nimeona watu wanasema tu inatosha inatosha bila kutoa mchanganua wa hiyo laki 3 utaitumia vipi?
-Mtoa mada amesema una mke na watoto utawezaje kuibalance hiyo laki 3 na kutosha kabisa?
-Mie natoa direction mpeni mchanganua wa kutumia hiyo laki 3 eg

-Apange vyumba vya Tsh ngapi?
-Mchana ale asubuhi na mchana ale nini akiwa kazini? Nauli?
-Kodi ya meza aache Tsh ngapi na wawe wanaitumia vipi kwa mlo wa asubuhi,mchana(mkewe) na Usiku(famillia)
-Watoto wanasoma chai asubuhi na hela ya kununua mihogo,aisikilimu akiwa shuleni(mtoto hawezi kukaa na njaa mpaka saa tisa ndio aje kula nyumbani)
-Matumizi ya umeme,maji,sabuni(kufua ,kuogea).

Mchanganuo wangu:-
-Awe ananua vitu kwa jumla eg kiroba cha unga cha kilo 5(7,500/=),Mchele kilo 10 wa 1800(18,000),Nyanya kisado (5000),Vitunguu kisado(elfu 6),Mafuta ya taa(elfu 20),mafuta ya kupikia(lita 5 elfu 15),Kiroba cha mkaa(kilo 25 , Tsh 15000)
Hapo Jumla ni 80,000/=

-Baada ya hapo awe anaacha elfu 4 tu ya mboga kila siku kwa Mwezi jumla ni 120,000/=

-Na yeye bajeti yake kwa mwezi awe anatumia elfu 3 kwa siku ,chai atumie za kwenye dispensa ofisini awe ananunua tu chapati mbili za 500 au 600 na mchana msosi wa buku jero na nauli 800 kwahiyo bajeti yake itakuwa elfu 60,000/= kwa mwezi(20 working days)

-Hiyo 40 iwe ni gharama za umeme na maji na vitu vigogo vidogo.
 
Chai ya familia unakunywaje ya elfu 3 mkuu wkt mnajua uwezo wenu mdogo?

Viazi vitamu/mihogo ya 1000 mkiichemsha kwa familia ya watu 3 mnakula mpk mnaacha kwa kushiba na chai yenu ya rangi fresh kabisaa,tena wewe unayeenda kazini ukisha kunywa zako hio chai hapo home ukienda kazini hakuna kunywa chai tena huko ofisini.

Mkichoka mihogo/viazi kuna sehemu vitumbua/maandazi vinauzwa sh.100, sasa mpk mmalize hio buku 3 kwa asubuhi si mchezo.

Familia za zamani mmama ananunua unga wa ngano anakanda zake fresh kabisaa then anatengeneza zake maandazi ya familia kunywea chai asubuhi wiki nzima.

Maji ya kunywa huko kazini ni lazima ununue sio?Unadhani haya ma bag ya vijana yanabeba nini humo?Watu wanabeba mpk maji ya kunywa ya chupa waliyotoka nayo home mzee.

Unajua miaka ya 1998 huko serikalini watumishi kada za chini kama manesi mshahara ulikua Tsh.37,000(elfu thalathini na saba tu) kwa mwezi na waliishi na familia fresh tu.Hio Tsh 37,000 kwa sababu za inflation ni sawa na anayelipwa hio Tsh.300,000 kwa zama hizi.

Hio hela sio kubwa na inahitajika kufanya maarifa ya kuongeza kipato cha ziada lkn kibongo bongo watu wanaishi tu.



 
Asante kwa mchanganuo. Ila umeacha kipengele muhimu cha kodi ya nyumba. Au ni mchanganuo kwa mtu aliyejenga tayari?
 
kiasi gani inatosha.....?
 
Kama una mke anayejua maisha, anayejua kuvumilia mnaweza kutusua vizuri tu,ila pata mke mwenye makuu, hapo hata kwa muujiza ni ngumu
 
wakati naanza kazi yangu ya kwanza kwenye ajira nilikuwa nalipwa TZS 600K take home wakati dereva aliyekuwa ananiendesha alikuwa analipwa 250k .

Nilikuwa namuuliza huyu dereva anawezaje kuishi kwa mshahara huo kwa mwezi , wakati yeye alikuwa na mke mmoja na watoto wanne , halafu alikuwa na mchepuko una watoto wawili, mke wake alikuwa anaishi naye kwenye banda alilokuwa amejenga huko malamba mawili mbezi DSM.

Aliniambia yeye matumizi yasiyo ya lazima hafanyi wakati mimi mzee hiyo 600K hata mwezi hauishi nalikuwa napumulia mashine hapo sina mke wala mtoto.

Ila nilikuja kukaa sawa baadae baada ya kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa yangu kila inapoingia mwisho wa mwezi.

Hivyo mkuu 300K ni nyingi sana ukiiwekea nidhamu kwenye matumizi ya msingi na utaishi bila stress ingawa mikopo ya hapa na pale itakuwa haikauki kwa maisha ya kawaida.
 
duh hahahahaha atakuwa anaiba wese huyo
 
Jambo kubwa si kuangalia unachokipata na kupanga maisha .. Utapata msongo wa mawazo bure.. Nafikiri, anachotaka muuliza swali au kumsaidia yoyote aliyopo katika kiwango chochote, namna bora ya kumudu maisha... Hela yoyote unayopata ni mbegu.. Si ya kula yote, hivyo huwezi kula yote na kujiuliza namudu vipi?? Cha kufanya ni kuangalia jinsi unaweza kipato cha ziada au kuanzisha kitu cha kuongeza pato. Uko mahali pazuri, angalau una laki tatu kila mwezi.. Sasa panga mpango na ukishirikiana na mke, muweze kuchagua kitu cha kufanya.. Cha kuwaongezea pato...Biashara zipo nyingi, angalia tu mtaani kwako,kuna watu wana biashara nyingi tu... Lakini mtaji ni mdogo tu... Hawa watu na wao wanamudu maisha kwa biashara hizo ndogo ndogo...Na wewe unaweza kufanya.

Cha msingi uwe na nia, usijali maneno au kauli za watu, almradi unafanya biashara halali, utatoka .. Mtumainie Mungu wako, yeye aliye muanifu atakukamilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…