Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Unaishi mkoa gani? Tuanzie hapo
Mimi nalipwa 1m kwa mwezi, ukijumlisha na vizinga vya hapa na pale , sina mume wala mtoto ila hiyo pesa haijawahi kutosha.
Chukua mkopo kama unaruhusiwa uanzishe kabiashara hata ka kufuga kuku au kuuza mkaa uwe unapata daily income
 
Nina Dogo ofisini anapata take home 200000,, kila siku Ana kunywa supu ya kuku asbh,mchana chakula cha 3000 na maji , ingawa hana family ila sielewagi,,
Ha ha ha ha haaaaaaa, mtoto wa mjini huyooooo
 


Point..na watu naona wanajfariji kweli kweli!
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.

Kuna anayepokea take home 1.3m na bado maisha yanamshinda.
Issue siyo unapokea ngapi mkuu issue ni unapangiliaje maisha yako na unajiongezaje nje ya mshahara.
Hata ukilipwa take home ya 2m kama hujiongezi na hupangilii mambo utashangaa kila mwezi unakuwa mtu wa madeni tu
 
unaweza kuoa jinamizi hela yeyote haitoshi
 
Take home yangu ni 229,000/ but Nina nyumba japo ya kawaida tu,mke na watoto wanakula na nyumbani kwa wazazi natoa huduma,hii kitu ni mipango tu mkuu,huwezi amini huwa nasevu na akaunti yangu haipungui million kwa tahadhari
hebu orodhesha mnakulaga nini? na gharama nyingine za lazima kama vile usafiri nk
 
Kubwa sana hiyo kuna watu wanaondoka na laki na maisha yanasonga
wacha zako hizo 😬😬weka picha ileee ya kiburungutu cha mshahara wako navimia mbili juu kwenye barabendi😂 tuthaminishe uhalisia wa unachotetea
 
mimi nina take home 1.1m but bado naona maisha magumu hao wa 3 ata sielew asee
Mimi take home yangu ni 510 baada ya makato 230 ni savings na inayosalia ni bajeti yangu na familia mwezi mzima inatoboa na pesa kiduchu ya kusaidia ndugu inapatikana na michepuko juu ila wife ana ka genge njaa hapendi kukaa iddle kanasaudia mboga sabuni bills ndogo ndogo na maisha yanasonga ko hiyo pesa inatosha sana tuu
 
Take home 300,000/=

Means kwa siku matumizi yao yasizidi 10,000/= mtafutaji pamoja na familia yake...

It's a hustle kwa kweli... wanakuaga na maisha magumu sana, kila kitu kwao anasa...

Mgeni akija wananuna...


Cc: mahondaw
Sio kweli inategemea na mkoa sasa kama huku rukwa 2000 unapata migebuka 6 unaanzaje kufukuza mgeni? Hiyo pesa nyingi sana na uhakika wa kula nyama au samaki daily labda kwenu Dar au Arusha au Dodoma ila huku kwetu it is more than enough,mchele supa 1700/1800 wakati Njombe au Dar 2400/2500 huoni utofauti hapo?
Huku mkoani ukiwa na mil.6,000,000 unajenga nyumba ya vyumba 3,sebule,jiko na public toilet na unaezeka msauzi kabisaa,,ukiwa na 10 mln hapo nyumba imekamilika kila kitu sasa utalinganisha vipi na Dar ambayo gharama ya ufundi tuu ni sawa na gharama ya kiwanja?
 
Iko hivi 150,000 mtafutaji na 120,000 nyumbani 30,000 tahadhari mambo ya kuvaa ni bajeti zinapatikana pembeni kama genge au posho
 
Gari gani hilo kinatumia mafuta ya 15,000 kila siku mkuu?
 
Hiyo chai 3000 inategemea na mazingira .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…