Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Nimeona watu wanasema tu inatosha inatosha bila kutoa mchanganua wa hiyo laki 3 utaitumia vipi?
-Mtoa mada amesema una mke na watoto utawezaje kuibalance hiyo laki 3 na kutosha kabisa?
-Mie natoa direction mpeni mchanganua wa kutumia hiyo laki 3 eg

-Apange vyumba vya Tsh ngapi?
-Mchana ale asubuhi na mchana ale nini akiwa kazini? Nauli?
-Kodi ya meza aache Tsh ngapi na wawe wanaitumia vipi kwa mlo wa asubuhi,mchana(mkewe) na Usiku(famillia)
-Watoto wanasoma chai asubuhi na hela ya kununua mihogo,aisikilimu akiwa shuleni(mtoto hawezi kukaa na njaa mpaka saa tisa ndio aje kula nyumbani)
-Matumizi ya umeme,maji,sabuni(kufua ,kuogea).

Mchanganuo wangu:-
-Awe ananua vitu kwa jumla eg kiroba cha unga cha kilo 5(7,500/=),Mchele kilo 10 wa 1800(18,000),Nyanya kisado (5000),Vitunguu kisado(elfu 6),Mafuta ya taa(elfu 20),mafuta ya kupikia(lita 5 elfu 15),Kiroba cha mkaa(kilo 25 , Tsh 15000)
Hapo Jumla ni 80,000/=

-Baada ya hapo awe anaacha elfu 4 tu ya mboga kila siku kwa Mwezi jumla ni 120,000/=

-Na yeye bajeti yake kwa mwezi awe anatumia elfu 3 kwa siku ,chai atumie za kwenye dispensa ofisini awe ananunua tu chapati mbili za 500 au 600 na mchana msosi wa buku jero na nauli 800 kwahiyo bajeti yake itakuwa elfu 60,000/= kwa mwezi(20 working days)

-Hiyo 40 iwe ni gharama za umeme na maji na vitu vigogo vidogo.
Kodi anatoa wapi mkuu? Hela ya dharura mtomto kuumwa?
 
Mimi take home yangu ni 510 baada ya makato 230 ni savings na inayosalia ni bajeti yangu na familia mwezi mzima inatoboa na pesa kiduchu ya kusaidia ndugu inapatikana na michepuko juu ila wife ana ka genge njaa hapendi kukaa iddle kanasaudia mboga sabuni bills ndogo ndogo na maisha yanasonga ko hiyo pesa inatosha sana tuu
Hicho ndo kinachokuokoa cha mke kujishughulisha
 
acheni kuzunguka kwa huo mshahara lazima upate tabu sana kuweza kumudu maisha na kufanya maendeleo bila kufisadi
na hapa ndipo sera za serikali zinpokuwa mbovu unaruhusuje kim a cha chini kwa mfumuko huu wa bei na karne hii
kiwe 300k au chini ya hapo?
 
Hicho ndo kinachokuokoa cha mke kujishughulisha
Hakuna cha kuniokoa hapo mke akiwa ananyonyesha anakutegemea mda wote swala hapa ni kujitune kuendana na bit ya maisha,genge lenyewe hata 60,000 haifiki kwa mwezi ndo utasema inaitegemea? Afu kumbuka pesa ya mke huwa ni yake sema sie wengine wake zetu sio wa kupenda kujiremba saana wanaridhika na maisha ya kiasi na mimi binafsi sitaki mwanamke wa kuegesha makalio tuu home lazima atafute hata mia na pia bajeti za urembo huwa sinaga hizo anakomaa mwenyewe
 
Jamani kiuhalisia huo mshahara ni mdogo ,mimi hapa nilipo nalipwa 200k take home sijaoa na sina mtoto ila cha moto nakiona,ila nitafanyaje sasa ndoivo tumemaliza chuo ajira hakuna tupo mtaani jobless, Nimejitahidi kutunza walau nipate hata mtaji ila ndoivo majukumu mengi hususan sisi tuliotoka kwenye familia za kimaskin,wazazi nao wanataka huwasaidie,madogo wanataka,shangazi,mjomba n.k

Dah ila maisha hayapo fair kabsa,yan napitia comments za wadau naona kuna watu wanalipwa hadi 2m nao pia wanalalamika? Mimi nikipata hata 500k naamini nitafanya jambo kwa kwel.
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Huwa naachiwa elfu hamsini kwa ajili ya chakula nakaa nayo week 2 inatosha na inabaki.hii inaitwa home economics na ni mwanamke mwerevu peke ake anaweza
 
Hata sio ku-fake mzee,

Tu-assume una mke na mtoto mmoja

Chai tu kwa nyumbani kwa hiyo familia watatumia 3000 kima cha chini kabisa,

Wewe pia chai huko kazini kwako assumption 1000 au 1500

Haya mchana familia inakula kiasi gani na wewe unakula nini?

Usiku vipi?

Hapo hujaweka usafiri hata kama ni wa daladala

Hujaweka vocha

Bado hujanywa maji

Mzeee hiyo pesa mjini mtihani
Hiyo chai ya 3000 ni chai ya aina gani
 
Wanaosema wanaweza mudu maisha kwa tshs 300k au chini ya hapo na wana familia wangetoa mchanganuo ili uzi huu uweze toa elimu kwa wengine jinsi ya kubajeti.
Familia ya watu wanne;
Asubuhi
Chai 4@ 200 = 800
Maandazi 12@ 100 =1200
Jumla 2000

Mchana
Sembe 1kg 2000
Veg 300
Viungo 1000
Maharage 1/4 700
Nishati mkaa 1000
Jumla 5000

Usiku 4000

Sijaweka
usafiri kwenda kurudi kazini
Vocha
Kodi kama kapanga
Nguo
Kingamuzi
Maji
Sabuni
Dawa ya meno
N.k
 
Hiyo ni hela ndogo sana kwa maisha ya mjini labda kijijini ambako atalima chakula chake cha mwaka mzima,solar power,usafiri ni baiskeli,maji ya kujichimbia mbugani ,hakuna bia hapo wala sigara,
Tusijazane upepo
 
Back
Top Bottom