Ok kwa mimi point zangu ni kuwa;
Mazingira ya kufanyia kazi ni duni kulingana na kada nyingine
Mshahara duni na mazingira duni ya kazi ya ualimu sio sawa kumtia mtu gharama za kwenda kurudi mikoani na wilayani kutafuta mshahara wa 400k
Ukiangalia ufaulu wa miaka hii ni wazi kuwa wanafunzi wanafaulu kupita matarajio na ndio maana wasio na ajira mtaani ni wengi sana hii ina maana walioajiriwa bila interview hawana mapungufu yoyote ambayo yangefanya kuwe na ulazima wa usaili ili kuchuja ubora
Kama ni kutafuta usawa au kuwapambanisha eti kwakuwa wanaohitaji ni wengi bado usawa huo hautakuwepo utake usitake rushwa lazima itatembea
Kigezo cha kupima competency ya mwalimu kwa mtihani wa kuchagua ni uwongo bora hata interview ya kufundisha sio multiple choice
Kuhusu izo kada nyingine wapigwe tu interview kwanza wanafanya kazi mijini na mtonyo wa kutosha lakini pia sio zote kwahiyo hata hizo ambazo mishahara na mazingira ni duni zenyewe kufanya interview za multiple choice ni kupotea rasilimali tu
Nyingine watajazia wengine
Mkuu nimeangalia sababu ulizozitoa kwa upande wangu nimeona hazima mashiko, Kwa sababu kila sababu uliyoitoa na Kada zingine zinapitia pia
Sababu ya kusema kuwa saizi watoto wanafaulu sana wala haina mahusiano na uwezo wa walimu, wote tunajua hili limetokana na SIASA za awamu ya 5 kutaka sifa kwenye kila kitu
Kuna watoto wengi tu na wengine wanatoka kwenye familia zetu, wanafaulu ilhali hawajui kusoma wala kuandika, na wala lawama hatuzipeleki kwa walimu bali wanasiasa
Mbali na walimu Kuna Maafisa Mifugo,kilimo,ustawi wa Jamii,watendaji nk, hawa wote wanatakiwa katika mazingira magumu lakini pia ata mshahara yao ni midogo pia
Lengo la interview kwenye kila sehemu waga linakuwa zuri, miongoni mwa sababu za kufanya interview ni pamoja na
1. UWAZI, kufanya usahili ili upate Jambo Fulani ni vizuri Kwa sababu kunaonesha uwazi katika upatikanaji wa mtu huyo badala ya kumteua tu kitu ambacho waga kinatoa hisia za uonevu
2. KIPIMO, kama mavyuoni walikuwa wanafanya mitihani ili kuonesha uwezo na uteyari wao basi bila Shaka wanastahili kufanya usahili pia ili iwe kipimo cha uwezo wao na uteyari wao wa kwenda kuitumikia hiyo nafasi
3. UWEZO, kama nafasi za kazi zipo 50 mkakutana mnaoigombania mpo 150, Kwa lugha nyepesi watakaopata ni kuwa wamekuwa Bora kuliko wale 100 waliokosa
4.UTHUBUTU, kama ulipigania kazi Kwa kupoteza pesa,kupoteza muda na kupata usumbufu wa kufanya mitihani na hatimae kuipata ni wazi kuwa ulikuwa unahitaji hiyo kazi hivo lazima utafanya kazi Kwa moyo
5.UWAJIBIKAJI, angalau mtu akisotea nafasi ya kazi kunakuwa na % za kuamini kwamba atakuwa muwajibikaji kwa sababu aliisotea hiyo nafasi, tofauti na mtu ambae amepata tu kama sandakalawe
6.THAMANI, kufanya usahili kunaipa thamani hiyo nafasi ambayo watu wamekutana kuipigania
7.UTAYALI, mtu ambae atakubali kufanya usahili ni wazi kuwa ana utayali wa kufanya hiyo kazi,kwenda popote atakapopangiwa,kupata mshahara wowote ule na hivo kupunguza malalamiko ambayo almost kila mtumishi wa TZ anayapitia
Kwahiyo tukumbuke kuwa walimu na wahudumu wa Afya nawao walikuwa wanafunzi kama wanafunzi wa Kada zingine, hakuna uspecial wowote ule ispokuwa mwanzo ilitumika busara ya kuvutia wanafunzi kuchagua kusomea hizo Kada
Kwa hiyo nawao wapo ambao hawana uwezo wa kufundisha vizuri kama ilivo kwenye Kada zingine, hivo tulidhike tu na ukweli kwamba kwa sasa interview haikwepeki