Mliopata utashi wa kufuata dini tofauti na za kurithishwa na wazazi wenu, mliwezaje?

Mliopata utashi wa kufuata dini tofauti na za kurithishwa na wazazi wenu, mliwezaje?

Mgosi Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2023
Posts
499
Reaction score
604
Hapa kazini nimekutana na binti Wa kisabato.Nimekua nae karibu sana na ananiheshimu sana kikazi lakin pia kimahusiano ya kawaida.

Ni binti mwenye maadili ya hali ya juu, kutokana na mazoea nikaamua nimchimbe alikujaje kua msabato kwan nilijua amezaliwa kwene familia ya kisabato haswaa.

Cha kushangaza kaniambia kwao hata si wasabato ni yeye tu kwene familia yake. Mama ake ni muislam na baba ake ni mkatoliki. Hivo yeye katika kukua alikulia kwene makuzi ya dini hizo lakini alipokuja kujitambua katika uchambuzi wa neno la mungu akaja kuona usabato ndio unaomfaa na unaendana na kile anachoamini ndani.
nimeshangaa pia ni mifano nadra sana.

Je, nyie mlioweza kukataa kurithi dini na kufuata utashi wenu katika dini mnawezaje ? maana huu ujasiri ni nadra kuukuta sehemu
 
FB_IMG_1722416875685.jpg
 
Ukiwa na wazazi ambao ni waelewa na wanakupa uhuru wa kuchagua ukipendacho ni rahisi sana kuchagua njia unayoipenda.

Ila kama umetoka nyumbani hapo upo huru zaidi kuchagua njia unayotaka
 
Ukiwa na wazazi ambao ni waelewa na wanakupa uhuru wa kuchagua ukipendacho ni rahisi sana kuchagua njia unayoipenda
Ila kama umetoka nyumbani hapo upo huru zaidi kuchagua njia unayotaka
Ni ngumu sana mtu kutoka dini ya wazazi wake
 
Ni matokeo ya malezi yasiyozingatia sana ibada na mafundisho ya imani. Baba muislam, mama mkatoliki...unaweza kuona tayari familia haina unity kwenye swala la imani..
 
Ni matokeo ya malezi yasiyozingatia sana ibada na mafundisho ya imani. Baba muislam, mama mkatoliki...unaweza kuona tayari familia haina unity kwenye swala la imani..
Wapo pia waliolelewa malezi mamoja ila wakabadili
 
Wazazi waislamu ndio wanakuwaga watata.

Maana dini yao inawafundisha wamtenge na wamchinje mtu anaehama uislamu.

Wazazi wakristo hawana shida. Mtoto Sali popote unapotaka. Maana ukristo hauna sheria ngumu
 
Wazazi waislamu ndio wanakuwaga watata.

Maana dini yao inawafundisha wamtenge na wamchinje mtu anaehama uislamu.

Wazazi wakristo hawana shida. Mtoto Sali popote unapotaka
aisee🤬
 
Mi nilikua muislam lakini nikabadili kua shahidi wa yehova.

Wazazi wamejifanya kunitenga saizi mwaka watatu wanaanza kujirudi.

Hamna kinachoshindikana ukiamua
 
Wazazi waislamu ndio wanakuwaga watata.

Maana dini yao inawafundisha wamtenge na wamchinje mtu anaehama uislamu.

Wazazi wakristo hawana shida. Mtoto Sali popote unapotaka. Maana ukristo hauna sheria ngumu
Wanatishia tu,,,
nchi hii nani akuchinje labda huko saudia au iran
 
Back
Top Bottom