Mliopata utashi wa kufuata dini tofauti na za kurithishwa na wazazi wenu, mliwezaje?

Mliopata utashi wa kufuata dini tofauti na za kurithishwa na wazazi wenu, mliwezaje?

Hapa kazini nimekutana na binti Wa kisabato.Nimekua nae karibu sana na ananiheshimu sana kikazi lakin pia kimahusiano ya kawaida.

Ni binti mwenye maadili ya hali ya juu, kutokana na mazoea nikaamua nimchimbe alikujaje kua msabato kwan nilijua amezaliwa kwene familia ya kisabato haswaa.

Cha kushangaza kaniambia kwao hata si wasabato ni yeye tu kwene familia yake.
Mama ake ni muislam na baba ake ni mkatoliki.Hivo yeye katika kukua alikulia kwene makuzi ya dini hizo lakini alipokuja kujitambua katika uchambuzi wa neno la mungu akaja kuona usabato ndio unaomfaa na unaendana na kile anachoamini ndani.
nimeshangaa pia ni mifano nadra sana.

Je Nyie mlioweza kukataa kurithi dini na kufuata utashi wenu katika dini mnawezaje ? maana huu ujasiri ni nadra kuukuta sehemu
Mimi ni mmoja wapo mkuu,baba yangu na mama yangu ni warutheli,kwa Sasa ni Msabato.
 
Mimi kwetu waislam lakini tangu nijue uislam kwa undani niliona hauendani namm vile navoamini.
Nimeamua niwaachie uislam wao saizi nimebaki ally wa jina
 
Tuendelee kuzikataa dini, hasa za kuja na mambo yake yooote.

Dini ni utumwa,
Dini ni unyonyaji kiuchumi,
Dini inadumaza uwezo wa kufikiri.
Dini ni chanzo Cha hofu na sonona.
Epuka dini, ishi kwa amani.
 
Nilikuwa muislam nimebadili kuwa msabatho mwanzo wazazi walikuwa wagumu saivi wametulia ninaishi nawo vizuri sasa naanza kumfundisha mama mafundisho na nina uhakika atakuwa msabato soon yesu nisaidie
 
Dini bhana zimekuja kutuchanganya.

Ni bora tamaduni zetu zina manufaa ndizo vema zidumu na zisibadilishwe.

Dini wewe badilisha muda wowote pasipo kuzingatia kumfurahisha yeyote zaidi ya nafsi yako.
 
Wazazi waislamu ndio wanakuwaga watata.

Maana dini yao inawafundisha wamtenge na wamchinje mtu anaehama uislamu.

Wazazi wakristo hawana shida. Mtoto Sali popote unapotaka. Maana ukristo hauna sheria ngumu
Mh!!

Acha uongo yaani nyie mpaka makanisa hamuingiliani , wanachokataa waislamu mtoto akibadili dini basi atavaa vichupi .

Tuna dada yetu ni mkristo maana aliolewa na mkristo , sasa anavaa nusu uchi ndio wazazi wake wanakataa asiingie kwao mpaka avae vizuri ila sio diini .
 
Vijana ingieni msome kule Quora kuna wasomi nguli sana , wapo dini zote mpaka Atheists kule unapata maswali magumu na ukweli ..
 
Back
Top Bottom