Mliopo Dar, hali ya kibiashara ikoje sasa?

Mliopo Dar, hali ya kibiashara ikoje sasa?

Asante Mkuu ila la miezi 8 punguza kidogo
Kufa ni wajib ila pia cha moto kinakuja
Niko ndani week tu utafikiri mwezi mpaka siku nimezisahau
Ila kuna ajabu sana naiona huku wale walikuwa wanacheza kamari kwisha habari yao
Wauza pombe wote wamefunga biashara na kuna watu nawajua wanakunywa wanasema hawanywi tena na hela wana save kwa chakula [emoji23]
Kweli watu wengi wameeanza kuijua thamani ya hela na hali ikiendelea hivi hata thamani yake hatutaiona kabisa maana una chakula kimejaa nyumbani
Gari halili mafuta tena na mwisho hela unaiona kama karatasi tu hainunui hata toilet paper

Mkuu futa kauli ya miezi 8 tutawehuka humu
Acha nikaruke ruke garden


Sent from my iPhone using Tapatalk
Mie pia na shut down bar business
 
Nafanya biashara ya kuuza bidhaa za kampuni flani, juzi wamenipa taarifa kwamba stock yao inakaribia kukata, hivyo bidhaa yao haitakuwa sokoni kwa muda huu corona imefunga mipaka.

Sent using Fly in any Weather.
Dah hivi zile mishe hata za kiswazi swazi watu hawakimbizi tena. Mambo ya mishkaki ya paka,.kachori na supu ya pweza
 
Hili suala la level seat lina cost sana ukiachana na biashara. Tunatumia wastani wa masaa 5 barabarani kila siku.
 
mwanangu hali mbaya sana, mimi sijanunua mzigo tokea January vitu vimekata mtaji ndio unalika sahivi nafikiria daily hali ikirudi mtaji nitaurudishaje,, yani aisee kila kitu ovyo hata kitaa chips haziuziki wanafunzi wa vyuo wote wako home, yani wachina wamejua kutukost dunia nzima kisa popo(if it's true) ...stress kila saa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vibomba vya plastik vya kuwekea ktk ndoo vilikua vinauzwa 3000, daah sasa hivi 10k
Ndoo za plastiki zimepanda bei, na zimekuwa dili. Biashara njema kwa waziuzazo. Vibomba vya plastiki vya kuweka kwenye ndoo, navyo si haba. Sanitaiza. Na bidhaa zote ziendanazo na wakati uliopo, soko lake zuri kwa wachuuzi.

Levo siti imesababisha fursa ya kuchukua leseni za muda mfupi LATRA kwa wanaotaka kujiunga kutatua tatizo la usafiri. Bodaboda na Bajaji ruksa CBD. Hili ni soko zuri lengine.
 
Hili suala la level seat lina cost sana ukiachana na biashara. Tunatumia wastani wa masaa 5 barabarani kila siku.
Sasa chagueni kati ya kupata Covid-19 au kukaa level sit😁
 
Hii ni kwa Wakulungwa na wanaharakati na wabishi mliopo Bongo DSM.

Naomba kujuzwa hali ya biashara ikoje kwa sasa kwa scales zote yani biashara kubwa na ndogo ndogo za kitaa?

Mkuu ila kwa ufahamu wangu kama mwanazuoni ni kama hata kabla ya hili janga “Uchumi at micro level ulikua hauna perfomance nzuri” ingawa tulikua tunaambiwa “wia on traki”[emoji38]
 
Back
Top Bottom