Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Kwa upande wangu mikopo imenitoa sana pengine nisingefika hapa leo au ninge subir sana lkn ttzo limekuja awamu hii ya JPM mikopo imekua poison biashara zimeyumba sana nme maliza mkopo kwa sasa sikopi tena till further notice
 
Habari za mda huu wanajamvi!

Sina shaka maana na jua kwa rehema za MUNGU mmeamka salama na baadhi tiari mpo makazini kuijenga nchi yetu.

Kwa wale ambao hawapo poa kiafya na kiakili Mungu awatie nguvu na afya mpate kurejea mapema vitani

Kama kichwa cha thread kinavyosema, mliowai kukopa mikopo mikubwa bank na baadae kuirejesha na kutokukopa tena mlitumia mbinu gani?

Binafsi ni mhanga wa hili janga kwa zaidi ya miaka5.
Nilikopa ili kuupa nguvu mtaji wangu uliokua mdogo mwanzoni sikupata tabu kurejesha..tatizo ni kwamba kila mwaka najikuta nashawishika kuongeza ukubwa wa mkopo

Na kwakua dhamana yangu inaruhusu basi ata jamaa wa bank huongeza ushawishi wa kukuongezea
Shida ni kwamba tangu mwaka jana nimeanza kula msoto usiowakawaida.

Mkopo nliokua nao nilirejesha kwa tabu sana,nliapa nikimaliza sintakopa tena,kumbe nlikua najidanganya tu.

Yaan baada ya kumaliza nilikaa bila mkopo kwa miezi miwili tu nikarudi tena kujisalimisha waniokoe.

Hapa nilipo nipo kwenye tabu na mateso ya marejesho yani biashara inavyokua ngumu ndio kabisa naiona siku ya rejesho kama siku ya ukumu.
Imebidi nisimamishe shughuli zingine ili niweze kuinusuru dhamana yangu.

Ukweli ni kwamba mpaka sasa sijakutana na mtu binafsi aliejingiza kwenye mikopo akatoka huko salama,nimeona matajiri wengi wenye mitaji mikubwa lakini mtego wa kujinasua kwenye banio la mabenk limewashinda.

Wengi wao hadi mauti yanawakuta na kuacha benk ikiwadai tena madeni yasiolipika kiraisi.

Vijana wengi wameaga mashindano baada ya kushindwa kurejesha mikopo na dhamana zao kupigwa mnada.

Je wewe uliefanikiwa uliwezaje?
Na nini kinachofanya sisi tushindwe?

Hapa hatuwaongelei wale wanaokopa kwa kutumia salaryslip zao.

Onyo: Wale mliozoea kutoa povu kavulieni nguo hapa sio mahala pake.

Karibuni.
Mkuu, wengi watakwambia hakuna mtu anayeweza kuendelea bila mikopo, lakini mimi kwa Uwazi nakwambia hakuna mtu anaweza kuendelea kama atalipa Mikopo yote na kubaki bila mkopo, wengi tunaowaona wakiwa na biashara kubwa wana mikopo na muda wao wa liondoka duniani unapofika huacha madeni kwa warithi wao, mara nyingi mali walizoacha hupigwa mnada kufidia madeni. Aidha, kama warithi wakikubali kuendelea na biashara, na o huendelea na hali hiyo hiyo ya kudaiwa. Ndivyo ilivyo hata kwa nchi inapokopa kutoka Benki ya Dunia au Washirika wa Maendeleo, Serikali iliyokopo inapotoka madarakani, huichia Serikali inayoingia ili iendelee na madeni husika. Kwa hiyo usiogope kukopa, endelea tu wakati wako wa kuondoka duniani ukifika, familia yako italipa deni au mali utakazokuwa umeacha, sitapigwa mnada kufidia.
 
Kwa upande wangu mikopo imenitoa sana pengine nisingefika hapa leo au ninge subir sana lkn ttzo limekuja awamu hii ya JPM mikopo imekua poison biashara zimeyumba sana nme maliza mkopo kwa sasa sikopi tena till further notice
Ukiona hivyo, ujue ulikuwa hufanyi biashara halali.
 
ningekua nafanya biashara haramu ningekopesheka?
Biashara haramu ina maana pana: kukwepa kodi, kuuza vitu vya magendo, kuuza vitu fake, kutolipa leseni na vibali vya biashara na mengine ya aina hiyo. Kwa mawazo yangu, utakuwa ulikuwa unafanya mojawapo ya hizo biashara, kama sio kweli unathani ni kwa nini unalalamika kuwa awamu hii biashara yako haiendi vizuri ? Wote waliokuwa wanababaisha kwenye biashara, sasa hivi ni vilio kwa kwenda mbele.
 
Nimesoma mawazo ya watu wote ukweli ni kwamba mikopo sio mizuri kabisa Mimi mpaka Sasa nadaiwa bank kila nikikalibia kumaliza nasema sito kopa Tena ila nikimaliza tu narudia kukopa Tena kwahiyo mikopo ni mateso
 
Mkopo ni kama some sort of addiction, mtu akishaanza kuacha kazi sana. Matajiri wengi almost 90% wana run biashara kwa mikopo tena mikubwa sana ambayo sometimes hailipiki. 2004 mzee wangu akiwa nazo alikuwa na marafiki kma kina gachuma, lameck airo,patel na wengine nilijifunza wengi huendesha biashara kwa mikopo.

The difference ni kwamba wenzetu cjui wanafanyeje kuishi na madeni miaka yote mpk wanakufa na vizazi vinaendeleza madeni. Mpk leo i dont what went wrong mzee alikuwa na mtaji wa 800 milion back 2000 ilikuwa pesa kubwa tu kufikia 2005,alikuwa n 500 milioni fixed Account crdb,mpk benki ikamzawadia land cruiser mpya coz alikuwa akiweka pesa hatoi!

Wakawa wanamfuata mzee kukopa yaani anabembelezwa kabisa kukopa, hapo ndipo tatizo lilipoanza. To make the story short cjui kilitokea nn kufikia 2009 ,mzee alifilisiwa vibaya sana hawana hata chembe ya huruma walifilisi hadi kijiko. Infact tulitolewa kwenye nyumba na nguo zetu tu mpk leo mzee hayuko sawa,ana presha, kisukari ,magonjwa ya moyo yaani utadhani yeye ni benki ya magonjwa ! Hao watu watamu ukiwa unalipa ukiyumba utajuta kuzaliwa, i learned sitakuja nikope hata mia benki better litle with peace of mind
pole sana,lakini usiape kutokupoa mzee aliteleza tu...wew utafanikiwa
 
Biashara haramu ina maana pana: kukwepa kodi, kuuza vitu vya magendo, kuuza vitu fake, kutolipa leseni na vibali vya biashara na mengine ya aina hiyo. Kwa mawazo yangu, utakuwa ulikuwa unafanya mojawapo ya hizo biashara, kama sio kweli unathani ni kwa nini unalalamika kuwa awamu hii biashara yako haiendi vizuri ? Wote waliokuwa wanababaisha kwenye biashara, sasa hivi ni vilio kwa kwenda mbele.
bila shaka wewe ni kula kulala huelewi lolote kuhusu uchumi na biashara" naomba niku ulize kwnn katika biashara pesa ina itwa currency? uchumi wa hii nchi sasa haupo stable eti ,ndio mnavyo danganywa na wanasiasa eti wanaolalamika ni wapiga deal
 
Narudia tena, wote manolalamika kuwa Awamu hii hakuna pesa, mlikuwa wapiga deal, pesa zimerudi kwa watu waliokuwa wanazipata kihalali, ridhika na hicho unachopata, ndicho kilitakiwa kuwa halali yako tangu Awamu zilizotangulia.
 
utakua kwenye hili kundi
tapatalk_1540552832237.jpeg
 
Biashara haramu ina maana pana: kukwepa kodi, kuuza vitu vya magendo, kuuza vitu fake, kutolipa leseni na vibali vya biashara na mengine ya aina hiyo. Kwa mawazo yangu, utakuwa ulikuwa unafanya mojawapo ya hizo biashara, kama sio kweli unathani ni kwa nini unalalamika kuwa awamu hii biashara yako haiendi vizuri ? Wote waliokuwa wanababaisha kwenye biashara, sasa hivi ni vilio kwa kwenda mbele.
Stop the stupidity mkuu......sio kila ambaye biashara yake imeyumba kipind hiki walikua kwenye black market.....hujakaa kuwaza kwamba maybe wateja aliojua nao ndo wamebanwa na income yao imepungua so uwezo wa kuwa dispose hyo income kwenye biashara ya jamaa umepungua that why biashara yake inayumba. Pia ukiangalia idad ya vyeti feki wat if kama alikua na wateja wa kutosha hapo na kwa sasa hao wote hawana kazi.... Dont jump into conclusion
 
Mkuu, heshimu mawazo ya watu wengine kama ambavyo na ya kwako yanaheshimiwa. Hatuwezi wote kufikria kitu kimoja. Aidha, humu JF ni tuko kwenye Mdahalo, sithani kama ingekuwa Mdahalo wa wazi yaani mimi na wewe tunaonana, ungeweza kuniambia niache "stupidity" kwa jambo wazi kama hili. Ni kweli inafahamika kuwa kutokana na mabadiliko ya aiana ya maisha ambayo watu wamekuwa wakiishi, wamebanwa na income yao imepungua so uwezo wa kuwa dispose hyo income kwenye biashara umepungua ndo maana baadhi ya watu wanalalamika kuwa biashara zao zinayumba. Vilel vile, kuondoa watumishi wenye vyeti feki kumepunguza idadi ya wateja katika biashara. Hoja yangu sio wafanya biashara kuendelea kulalamika, wanapaswa kujipanga kuendeleza biashara yao kwa aina hiyo ya kipato maana ndicho kipato halali. Hii ni kwa sababu kipindi cha nyuma watu walikuwa wanapata pesa amabazo hawana uchungu nazo, vivyo hivyo na matumuzi yalikuwa ya ovyo ndo maana wafanya biashara nao walikuwa wanaona wanapata pesa nyingi lakini zilikuwa chafu. Pia, hata hao wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo, watu pekee waliokuwa wanalipa kodi halali ni wafanyakazi wa Sekta ya Umma. Shikirisha ubongo wako, wacha Mhe. Rais aweke mazingira mazuri ambayo baadaye kila mtu atafaidi matunda ya uhuru.
 
Gari , nyumba , biashara ada ya shule ni mikopo halafu unajiita tajiri , huwezi inuliwa na benki ukabaki salama.
Mkuu, hayo ndo Wadau hawataki kusikia, nimejaribu kueleza hapo juu wamenijia juu. Ongeza na mikopo ya Elimu ya Juu. Mfano mzuri wa jinsi ambavyo mikopo haiwezi kumtoa mtu, ni jinsi nchi za Kiafrika zinavyokopa, lakini zinaendelea kuwa masikini.
 
Mada nzuri nimeipenda. Nimeona wengi wanaipinga mikopo kwa hoja nzuri tu ila hamjatupa njia mbadala ya kupata mitaji ya kuanzisha biashara au ya kukuza biashara. Kwa mtu mwenye kipato cha million moja kwa mwezi anawezaje kupata mil 10 ili aweze kuanzisha au kukuza biashara. Maana akiamua kudunduliza 200,000 kila mwezi itamchukua takribani miaka minne ili aweze kupata hiyo mil 10. Tunaomba ushauri wenu wazoefu wa mambo ya mikopo
 
Nan kakudanganya mikopo haiwezi kukutoa? ungeuliza uka elekezwa acha ujuaji ttzo nyie fresh from school mna ujuaji mwingi alfu hauna maana yoyote
 
Nan kakudanganya mikopo haiwezi kukutoa? ungeuliza uka elekezwa acha ujuaji ttzo nyie fresh from school mna ujuaji mwingi alfu hauna maana yoyote
Kukopa hela ukanunua/ukajenga nyumba au ukanunua gari, au ukalipia mtoto karo haina shida, tatizo ni kukopa ili uongeze mtaji kwenye biashara, halafu uache kukopa katika maisha yako yote kwa ajili ya hiyo biashara. Jaribu uone, kama hiyo biashara itaendelea. Unathani wafanyabiashara wakubwa hawana mikopo ? Thubutu, wana mikopo mikubwa sana ambayo hailipiki katika maisha yao yote, wakiondoka wanaacha kwa warithi wao. Vivyo hivyo kwa mataifa nayo yanaendelea kukopa. Awamu moja ikiondoka inaacha madeni kwa awamu inayofuata.
 
Mada nzuri nimeipenda. Nimeona wengi wanaipinga mikopo kwa hoja nzuri tu ila hamjatupa njia mbadala ya kupata mitaji ya kuanzisha biashara au ya kukuza biashara. Kwa mtu mwenye kipato cha million moja kwa mwezi anawezaje kupata mil 10 ili aweze kuanzisha au kukuza biashara. Maana akiamua kudunduliza 200,000 kila mwezi itamchukua takribani miaka minne ili aweze kupata hiyo mil 10. Tunaomba ushauri wenu wazoefu wa mambo ya mikopo
Auze Asset yake kama vile shamba au mifugo.
 
Back
Top Bottom