Mliowahi kupigana darasani leteni ushuhuda wenu hapa

Mliowahi kupigana darasani leteni ushuhuda wenu hapa

Hilo pambano gani la masaa mawili aisee au mlikuwa mnakabana sana 😅! Nakozi za maana haziwezi kumaliza dakika 40 lazma mmoja aombe yaishe.

Hio ilikuwa inaitwa “parling” au kuzipanga “mtu mbike!” Maeneo ya Morogoro Golf Club pale ndio ilikuwa eneo la maangamizi.
😂😂 Mkuu ilikua hakuna anaekubali, yaani kifupi tulitoshana nguvu kabisa kabisa. Kuna muda mashambilizi yanakua kwangu na muda mwingine kwake ila kila mtu alikua anayatoa.

Aisee kupigana ni kazi jama ile siku tulichoka mnoo. Ila mapambano yangu mengine hata dk 5 nyingi nishamchapa mpinzani.
 
Uuwiii!! Sijawahi pigana na miaka hiyo Shule zetu za Kayumba siku ya kufunga shule ndo ya watu kuondoa hasira zao kama mlikosana.

Mi nilikuwa ile mida shule inafungwa kengele ikipigwa tukienda mstarini mbio kwa Kaka ili tukimaliza niondoke naye. [emoji3]
[emoji38][emoji38]
Ungejaribu zichapa japo ck 1 uje tusimulia bana[emoji23][emoji23]
 
Nilizichapa na Ticha wa sayansi uvumilivu ulinishinda alikua anapiga vidole vyetu kwa rula. Nilimngata meno nikiwa nalia nikakimbilia juu ya madawati. Akija huku nahamia upande mwingine hakuna aliyenigusa maana niliku nishashika bikali.

Huyu ticha ni best yangu sana tukikutana nampa heshima yake.. na tunapiga stori vizuri tu.
...Bro Himid alinipiga ngumi ya sikio darasani nikaanguka chini nikalia weeee hapo nikaamka nikachukua bikali nikamfuata..Niliizamisha bikali yote mgongoni. Toka siku hiyo hakunigusa na nibest yangu sana
Na wewe heshima yako lazima iendelee kuwepo kwa huyo Ticha
 
Kuna jamaa nilikuwa namuonea sana ndio alikuwa fala wangu.

Siku hiyo akaamua kunitest hahahaha.
Maana nilikuwa maneno mengi mikwara kibao huku mweupe kabisa!!

Jamaa aliniotea roba moja halafu madenti wengine wakawa wanashangilia kwamba asiniachie hadi nikojoe!

Kiukweli siku hiyo nilimuona ziraili kbs..
Ilibidi nikojoe tuu maana sio kabali ile.
Hata angetaka ninye ningekunya!!

Hapo heshima ikawepo..
Akaletwa chalii mwingine tena alikuwa na kaumbo kadogo halafu mi bonge la mtu.

Nikaanza bullying kama kawaida.
Yule dogo akatonywa na wambea kwamba mi mweupe mikwara tuu..

Dogo akaniamulia siku hiyo akanishika mapumbuu acha maneno kabisaaa!!
Yaani kumpiga nilishindwa nikabaki nimetulia tuu.mkono mmoja kanibana mapumbuu mwingine ananipiga ngumi na makofi!!
Kalikuwa kafupi yaani kunipiga kofi hadi karuke juu km masai ndo kanipate.hahahaha
 
Aisee darasa la 7 nakumbuka nilipigana na mwalimu, alikuwa kijana kijana halafu anapenda sifa sasa siku hiyo kaingia kakuta watu wanapiga kelele, mimi naye ndio naingia ndani nilikuwa nimepitiliza mapumziko maana kipindi hicho walimu hawafundishi tena, tunasubiria mtihani wa taifa.

Sasa mwalimu akaniwakia na kutaka kunichapa eti mimi ndio kilaza kabisa hata kufuata kengele siwezi, ile karusha fimbo anichape mkononi nikaidaka sijui ni ujinga gani ukaniingia nikaona huyu jamaa mbona namuweza nikaanza purukushani naye darasani nikamzidi nguvu sijui aliona aibu nikamgaragaza chini nikakimbia[emoji2089][emoji2089][emoji2089].

Ilikuwa katikati ya wiki sasa kurudi shule kesho yake aisee walimu walinikomesha nilipelekwa ofisini kuna wamama hao walinishikilia mikono wengine walikuwa wanachapa bakora nafikiri nilipigwa kwa muda zaidi ya saa 2 na walimu wa shule nzima, yaani wengine walikuwa wanachapa wanaenda kunywa chai wakirudi wanasema hili bado lipo wanachapa, nililia nikaachwa nikae kabisa katikati ya ofisi anayekuja anacharaza viboko anaondoka, nilikoma aisee
Noma sana, ila ukweli ni kwamba ulileta heshima
 
Shule zetu za vidumu na mfagio mambo haya ya ngumi yalikuwa Kawaida sana kutokea.

Nimeshuhudia mechi nyingi sana za ngumi,mechi inaandaliwa mapema,njiani wakati wa kurudi ndio muda wenyewe.

Mimi nilikuwa si mtu wa vurugu japo nishawahi piga mtu katika harakati za kujinasua,,alinivamia anipige kwa chuki zake tu..
Nikamtandika.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mechi inapangwa mapema hivyo[emoji1787][emoji1787]

Yaani ukiikosa kuicheki hiyo burudani umejitakia mwenyew
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Eti jezi ya Simba [emoji38]

Kuna muda mwalimu alikamata washangiliaji wote wa ngumi..
Kumbe alichelewa kutoka aiseeee...tuliruka kichura siyo Cha nchi hii..halafu mwalimu Mwenyewe ni bimkubwa .

Nilirudi nyumbani Sina hali,akasema kesho urudie tena kubaki kushabikia ngumi.
Hahahahhahahah
 
Kuna dogo mmoja alikuwa anaitwa Hery barton mjuaji sana nakumbuka alizichapa na mchizi mmoja anaitwa Daniel Msuya! Sikuhio mapema sana kabla ya assembly saa 12 asubuhi.

Aisee zile ngumi zilikuwa level za kimataifa yani! Hamna kushikana hapo ni nako 2 nako yani ikipenya unaskia shavu limeitika fyo.toooh. Pale ndio tulipata taste ya kina Tyson kabisa huku hery barton akila nakoz za kwenda maana Daniel alikua na utulivu sana kwenye kuzipachika.
Naona mkuu uliinjoy mitanange mikali
 
Nakumbuka wakat nipo darasa la nne nilikuwa napenda ugomvi sana yaan mm mda wote nimejiandaa kimapambano niko na t shirt na kivaa ndan ya shart kwa jili ya mapambano.

Sasa siku hiyoo nikaingia mkenge kwa lijaama tulikuwa tuna lita taralila limerudia darasa alaf lirefu ebwana eeh liliniangusha chini likanipiga ngumi za pua kwa mara ya kwanza natolewa damu
Yaan mpk narudi home nafikiria lile jamaa ikabidi nikakae nyuma ya nyumba maumivu ya poe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu ulikuwa unajiandaa kwa mechi muda wowote[emoji1787][emoji1787]
Ulitisha sana
 
Nakumbuka wakat nipo darasa la nne nilikuwa napenda ugomvi sana yaan mm mda wote nimejiandaa kimapambano niko na t shirt na kivaa ndan ya shart kwa jili ya mapambano.

Sasa siku hiyoo nikaingia mkenge kwa lijaama tulikuwa tuna lita taralila limerudia darasa alaf lirefu ebwana eeh liliniangusha chini likanipiga ngumi za pua kwa mara ya kwanza natolewa damu
Yaan mpk narudi home nafikiria lile jamaa ikabidi nikakae nyuma ya nyumba maumivu ya poe
Hahahahahah kipindi tunasoma na mtoto wa Juma Ngasongwa waziri wa viwanda back in that time. Salim alikuwa machachari sana ila kumbe mdomo mwingi ngumi hajui bana sasa kumbe wana walikuwa wanamuogopa bure kabla hatujau std 7 si akawa anamzingua dogo mmoja anaitwa Zamdeen. Dogo siku ya graduation akaja na kakaake anaitwa Aladeen babu. Sasa siku hio Zamdeen akamchezesha Salim ili ampambanishe na braza wake! Kilichotokea siku ya graduation Salim alikula vitasa vya chap chap alilia kama mtoto *****!😅😅😅
 
Kuna jamaa nilikuwa namuonea sana ndio alikuwa fala wangu.

Siku hiyo akaamua kunitest hahahaha.
Maana nilikuwa maneno mengi mikwara kibao huku mweupe kabisa!!

Jamaa aliniotea roba moja halafu madenti wengine wakawa wanashangilia kwamba asiniachie hadi nikojoe!

Kiukweli siku hiyo nilimuona ziraili kbs..
Ilibidi nikojoe tuu maana sio kabali ile.
Hata angetaka ninye ningekunya!!

Hapo heshima ikawepo..
Akaletwa chalii mwingine tena alikuwa na kaumbo kadogo halafu mi bonge la mtu.

Nikaanza bullying kama kawaida.
Yule dogo akatonywa na wambea kwamba mi mweupe mikwara tuu..

Dogo akaniamulia siku hiyo akanishika mapumbuu acha maneno kabisaaa!!
Yaani kumpiga nilishindwa nikabaki nimetulia tuu.mkono mmoja kanibana mapumbuu mwingine ananipiga ngumi na makofi!!
Kalikuwa kafupi yaani kunipiga kofi hadi karuke juu km masai ndo kanipate.hahahaha
[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23]
Mkuu ukaona isiwe tabu, ukawamwagia kojo
 
Back
Top Bottom