Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
China inakabiliana na mlipuko mpya wa virusi vya human metapneumovirus (HMPV), vinavyoenea kwa kasi katika majimbo ya kaskazini, hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 14, ikiwa ni miaka mitano baada ya janga la Covid-19.
Ripoti na machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanadokeza kuwa virusi hivyo vinasambaa kwa kasi huku wengine wakidai hospitali na sehemu za kuchomea maiti zimezidiwa.
HMPV husababisha dalili zinazofanana na mafua, huku nyingine zikiwa sawa na zile za Covid-19. Maafisa wa afya wanafuatilia kwa karibu hali hiyo wakati virusi hivyo vikiendelea kuenea.
Dalili za HMPV, kama ilivyobainishwa na CDC, ni pamoja na: kikohozi na mafua makali au Pua iliyoziba, homa, maumivu ya koo, kupumua kwa shida na Uchovu wa mwili.
==