Nashangaa kuona vijana wa CHADEMA na ACT wakihangaika kujadili suala ambalo katika demokrasia halina mjadala.
Magufuli akiwa mgombea wa CCM amekuwa akiwapigia debe wagombea wa CCM na kuwanadi na kusema bayana kuwa mkiniletea flani hapa maendeleo yatakuja msiponiletea huyu hiiiiiiiiiiii shauri yenu!!!
Vijana wanaochipukia katika siasa wanapaniki kusikia hivyo na kuanza kuweka tafsiri za kishamba kuwa Rais anabagua.
Huo ni ushamba wa kisiasa, Rais Magufuli yuko kwenye demokrasia ya siasa anapigania nafasi yake na anawapigania wanachama wa Chama chake lazima awanadi na kuwaombea kura hawezi kumnadi mgombea wa upinzani itakuwa kituko.
Licha ya yeye kuwa Rais lakini yuko katika majukwaa ya siasa kama ambavyo viongozi wengine wa CHADEMA na ACT na wengineo pia wako kwenye majukwaa ya siasa na hawawezi kamwe kumpigia debe mgombea wa CCM hata kama amepita bila kupingwa.
Lakini turudi kiuhalisia, kwa nini Mgombea wa CCM anasema maendeleo hayana Chama lakini chagueni CCM? Nimeeleza hapo kuwa hizo ni sababu za convenience ya kiutendaji kwani:
1. Hatuoni jinsi wapinzani wanapoingia mabaraza ya madiwani wanavyokwamisha sera na mipango ya Serikali iliyoki madarakani?;
2. Kwani hatuoni jinsi Bungeni wabunge wa upinzani kwa misimamo ya kupangiwa kutoka nje au kupangiwa na vyama vyao kwa miaka mitano wamekataa kupitisha bajeti na hivyo kama usingekuwa wingi wa CCM nchi ingeingia kwenye mgogoro mkubwa kijamii??
3. Mara ngapi tunaona wapinzani wakipinga kila kinachofanywa na Serikali hata kama kizuri kwa umma? Hawa unawapigiaje debe kwa mfano? Yani unampigia debe mtu ambaye akichaguliwa anaponda ujenzi wa shule, vyuo, hospitali, barabara, madaraja atakwambia ni maendeleo ya vitu sio watu!!! Huyu wa nini?
Hapa ndipo unamuona Rais Magufuli falsafa hake ya "nileteeni diwani wa CCM na Mbunge wa CCM" nikafanye nao kazi.
Kauli hizo za kutaka watendaji watakaosimamia Ilani ya CCM chama kinachokwenda kushinda mchana kweupe, haimaanishi na haijawahi kumaanisha kuwa eneo alipo diwani wa upinzani au mbunge wa upinzani maendeleo hayaendi, la hasha, CCM anaharakisha tu maendeleo, kwani:
1. Ule uwanja wa ndege wa Kigoma hadi Zitto anatua na ndege safi wakati viwanja vingine vya ndege vya mikoa kama Simiyu, Tanga, Ruvuma na kwingineko umejengwa jimbo la mtu wa CCM?
2. Interchange ya Ubungo pale imejengwa jimbo la CCM? Na barabara ya njia nane Ubungo hadi Kimara hadi Kibaha ni jimbo la CCM?
3. Kajenga hospitali 71, vituo vya afya Kata 478 na zahanati zaidi ya 1000 hivi viko majimbo ya CCM pekee???
4. Amekamilisha meli ile Ziwa Victoria MV NEW VICTORIA wanapanda CCM tu?
Yako mengi lakini naseeeemaaaaa hata mimi, kwa kuangalia utendaji wa kinafiki usiosimama kwenye falsafa bayana ya maendeleo ya Taifa, naseemaaa maendeleo hayana chama ila chama kinachoweza kukubakikishia maendeleo ya kweli na ya maana na ambacho hakitaelekezwa na wazungu bali mahitaji ya Mtanzania ni CCM, CCM, CCM.
Asanteni sana.