LGE2024 Mlowo: Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo

LGE2024 Mlowo: Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Jeshi la Polisi limemzuia mwenyekiti wa Chama cha CHADMA, Taifa, Freeman Mbowe kuzungumza na wananchi wa Mbozi, Mkoani Songwe, na kuwatawanya kwa mabomu wananchi waliokusanyika kumsikiliza mwenyekiti.

Kwa mujibu wa Ratiba eneo hilo lilikuwa na mkutano wa Chama cha ACT wazalendo mchana wa leo Novemba 22, 2024.

Viongozi wa Chadema wakazungumza na Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na kukubaliana kuwa muda wa asubuhi mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe azungumze na wananchi wa Mlowo.

Pia soma: LGE2024 - Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe

Screenshot 2024-11-22 132641.png
 
Baada ya siku 2 tu za kampeni, tayari watawala washapata Picha kamili kwamba Mwisho wa CCM UMEFIKA RASMI, Sasa wameamua kuingiza Polisi na mitutu mitaani.

Tulishaonya Tangu mapema humu kwamba CCM haipo, imebaki polisi na watekaji tu.

Screenshot_2024-11-22-13-14-33-1.png
Screenshot_2024-11-22-13-14-21-1.png
Screenshot_2024-11-22-13-15-02-1.png

Nguvu za kuokoa Wahanga wa ghorofa la Kariakoo hakuna, ila ya kuumiza Raia imejaa!

Poor Polisi!
 
Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1 (1).png
    Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1 (1).png
    420.8 KB · Views: 4
  • 20240907_095744 (1).jpg
    20240907_095744 (1).jpg
    116.1 KB · Views: 5
  • IMG-20200726-WA0000.jpg
    IMG-20200726-WA0000.jpg
    43.7 KB · Views: 4
Yote kazi ya Mkwelima KIFUA KIPANA..
Natabiri hatari kubwa mwakani.
 
CDM nawafananisha na vijana wa zamani, kwenye mpira wa kitaa.

Kuna mashabiki wao wanafunga safari kwa sababu moja tu, mpira ukiisha watafute ugomvi na wahuni wa upande wa pili watandikane ngumi, bakora hiyo ndio furaha yao.

Kesho yake ukiwaona wana nundu wamekula kichapo huko balaa, ila mechi nyingine wapo hawakosi.

Ndio CDM campaign zimeanza jana tu tayari wana ugomvi na jeshi la polisi, yaani wao bila ya vurumai siasa zao hazinogi.
 
Chadema wanapenda attention ya media. Ratiba ni ya ACT, chadema anaongea na ACT na kukubaliana kabla ya mkutano wa ACT kuanza mwenyekiti wa Chadema aongee na wananchi, childish. Unafanya mabadiliko bila kutaarifu vyombo vilivyokabidhiwa ratiba kusimamia amani kwenye mikutano?? Walitakiwa kuomba kibali kwa wenye mamlaka ya kusimamia amani ya mikutano kuwa tumekubaliana na ACT kuwa tutaanza sisi kisha wataendelea.

Wameenda kiholela na wenye mamlaka ya kusimamia usalama hawakuwa na taarifa wakadhani wanataka kuleta chokochoko. Wenye mamlaka wapo sahihi, wasubuli siku yao na wafuate utaratibu na ratiba iliyowekwa ambayo wanaijua ila wanataka muda wote waonekane wanaonewa ili waonewe huruma
 
Wakuu

Jeshi la Polisi limemzuia mwenyekiti wa Chama cha CHADMA, Taifa, Freeman Mbowe kuzungumza na wananchi wa Mbozi, Mkoani Songwe, na kuwatawanya kwa mabomu wananchi waliokusanyika kumsikiliza mwenyekiti.

Kwa mujibu wa Ratiba eneo hilo lilikuwa na mkutano wa Chama cha ACT wazalendo mchana wa leo Novemba 22, 2024.

Viongozi wa Chadema wakazungumza na Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na kukubaliana kuwa muda wa asubuhi mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe azungumze na wananchi wa Mlowo.
Mbowe achia chamq watu wamekuchoka. Angaliq alama zq nyakati. Mwachie Lisu
 
Back
Top Bottom