Mme wako akifa Utaweza kuimudu familia?

Mme wako akifa Utaweza kuimudu familia?

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Nina swali kwa ndugu zetu wanawake je utaweza kuimudu familia ikiwa mumeo hayupo kwa namna yoyote Ile?

Au kwa Wanaume unauhakika kuwa Kama Leo au kesho ukifa au ukipata ulemavu wa kudumu mke wako ataweza kuimudu familia au itaangukia katika umaskini wakutupwa?

Kama jibu Ni hapana umejipanga kuchukua Hatua gani.

Nawasilisha , Hakuna ajuaye kesho.
 
Riziki itapatikana tu kwani hutokea na tumeyaona haya

Mwanzo ni mgumu ila huwa wanayakubali na maisha yanaenda

Mke anaweza kuolewa tena na maisha yakasonga

Kwa mwanaume pia ni hivyo anaweza kuoa wa kumlelea watoto na hata akamzalia wengine

Maisha ni fumbo huwezi kujua ya kesho
 
Nina swali kwa ndugu zetu wanawake je utaweza kuimudu familia ikiwa mumeo hayupo kwa namna yoyote Ile? Au kwa Wanaume unauhakika kuwa Kama Leo au kesho ukifa au ukipata ulemavu wa kudumu mke wako ataweza kuimudu familia au itaangukia katika umaskini wakutupwa? Kama jibu Ni hapana umejipanga kuchukua Hatua gani.

Nawasilisha , Hakuna ajuaye kesho.
Hata nikidondoka leo, waifu atapambania watoto wake tu, kuna wanawake wanapambania watoto wao ili hali baba wa hao watoto wako hai, hao wanawake wanaitwa Singo mamazi, kwahiyo mwanaume akifa maisha yanaenda tu kama mwanamke sio mzembe
 
Mkuu maisha hayana kanuni kama za sayansi kwamba wote mkiifuata Kwa usahihi mtafika sehemu Moja. Ndiyo maana vyuo vikuu Duniani vyote havina kozi za maisha na kutunuku wahitimu degree za maisha. Hivyo chochote unachopanga na kukitekeleza ktk maisha kinabaki kuwa ni trial and error tu.
 
Maisha yataendelea bila uwepo wako, ni kama tu hujawahi kuwepo.... ishi ukijua ni zamu yako tu.
 
Hapa cc wazee wakataa ndoa ,ngoja tubaki kusoma Maoni ya wake zenuu
 
Nina swali kwa ndugu zetu wanawake je utaweza kuimudu familia ikiwa mumeo hayupo kwa namna yoyote Ile? Au kwa Wanaume unauhakika kuwa Kama Leo au kesho ukifa au ukipata ulemavu wa kudumu mke wako ataweza kuimudu familia au itaangukia katika umaskini wakutupwa? Kama jibu Ni hapana umejipanga kuchukua Hatua gani.

Nawasilisha , Hakuna ajuaye kesho.
Mdakuzi njoo ujibu hili swali, yule wa kwako ataweza?
 
Riziki itapatikana tu kwani hutokea na tumeyaona haya
Mwanzo ni mgumu ila huwa wanayakubali na maisha yanaenda
Mke anaweza kuolewa tena na maisha yakasonga
Kwa mwanaume pia ni hivyo anaweza kuoa wa kumlelea watoto na hata akamzalia wengine
Maisha ni fumbo huwezi kujua ya kesho
Mkuu umejibu kisiasa sana.
Ni vyema ukaamini hayo lakini ukiwa katika process ya kujiandaa na yajayo.

Mi naamini hata Mungu hujidhihirisha pale kwenye juhudi binafsi.
 
Back
Top Bottom