Mme wako akifa Utaweza kuimudu familia?

Mme wako akifa Utaweza kuimudu familia?

Binadamu ana tabia ya kubadilika kulingana na mazingira..
 
Mume kufa umeenda mbali mno.

Jiweke mbali au niseme jitoe akili siku tatu tu, uone maajabu yatakayofanyika humo ndani.

Kufa hautajua matokeo, research will not be accomplished.
 
Hata nikidondoka leo, waifu atapambania watoto wake tu, kuna wanawake wanapambania watoto wao ili hali baba wa hao watoto wako hai, hao wanawake wanaitwa Singo mamazi, kwahiyo mwanaume akifa maisha yanaenda tu kama mwanamke sio mzembe
Point
 
We jamaa maswali gani hayo unauliza,jua fika Wanawake wote hata kama anakupenda kama kupe-wish yao ni wewe Mwanaume utangulie kufa.
Wenzio wanaolewa tayari wana plan kichwani.
 
Mke wangu nilikutana nae kwenye genge lake nikiwa kama mteja. Alikua ndio amemaliza chuo. Nilipenda maamuzi yake ya kuchagua kuwa mjasiriamali badala ya kusubiria ajira. Huu ni mwaka wa pili niko nae. Nashukuru Mungu nilimuamisha pale alipokua na genge lake na nikamjengea genge lingine maeneo hayo hayo. Mwaka huu Mungu mkubwa nimemchukulia Frem pambeni ya genge lake na kumfungulia duka so ana biashara 2, genge na duka na zote zipo sehemu moja.
Malengo yangu ni kumfanya awe mfanyabiashara mzuri. Note that mimi sina nidhamu ya fedha na kwenye biashara ni mbovu sana. Kwa kuwa nimepata mwanamke ambae anaweza biashara nimechagua kuwekeza kwake ili na yeye aweze hudumia familia yake lakini pia hata kama leo nikitwalia kwenye Ulimwengu huu basi awe na pakusimamia.
Note that kuhusu nyumba hajui habari ya kodi ya nyumba. Nilishajenga kibanda lakini pia eneo letu lina nafasi kubwa ya ufugaji wa kuku na tayari ameanza hii biashara ya kufuga kuku wa kienyeji.

God bless my family
 
Back
Top Bottom