Mmewahi kukumbana na uchawi wa kusahaulishwa

Mmewahi kukumbana na uchawi wa kusahaulishwa

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Yani jamaa anakuroga usahau au uwe unahairisha kila ukitaka kuchukua hatua.

Nilikutana na mganga flani akawa ananipa story yaani hata kama mtu anakesi ya kuua anaweza kumfanya hata Mahakama au ndugu wanaomshtaki wasifuatilie kesi.

Nimesikia kuna maeneo pwani ukilima Shamba ukikaribia kuvuna unapgwa juju hii unachukia Shamba hadi jamaa wamalize kuvuna na hadi wanaliuza ila kila ukitaka kwenda unasahau. Hii nilidokezewa na Dalali mmoja nikisubiri bus Bagamoyo stand.

Wafanya biashara nao nasikia huwa wanawaroga wale jamaa wa Mikopo ili wasifuatilie Mikopo waliokopa.

Kuna madalali wanakuuzia Kiwanja au Nyumba unalipa alafu wanakuloga usiende kisha wanauza tena.

Wakuu hii kitu imekaaje. Imenifanya niliona nasitasita kwenye kitu najilazimisha nikiogopa jamaa wasijekuwa wamefanya yao.
 
Kuna jamaa alikuwa na biashara ya pamoja na rafikiye. Watu wa familia yake walikuwa wanajua hili. Siku jamaa alipokufa, ndugu mmoja akajaribu kuwashauri wenzake kuwa marehemu ana biashara na rafikiye. Hakika hakuna aliyekumbuka hadi leo rafiki wa marehemu alikuwa nani.

Sijasimuliwa, nilihusika kama mwanafamilia na tumepoteza mazima.
 
mbona kama vile wewe unakumbuka kuna rafikiye na marehemu
 
Kuna jamaa alikuwa na biashara ya pamoja na rafikiye. Watu wa familia yake walikuwa wanajua hili. Siku jamaa alipokufa, ndugu mmoja akajaribu kuwashauri wenzake kuwa marehemu ana biashara na rafikiye. Hakika hakuna aliyekumbuka hadi leo rafiki wa marehemu alikuwa nani.

Sijasimuliwa, nilihusika kama mwanafamilia na tumepoteza mazima.
Hata mambo yapo mkuu
 
Kesi ya mauaji hustakiwi na ndugu wa marehemu unashtakiwa na jamuhuri mzee ustegemee hiyo dawa kufanya kaz labda umwage pesa huko mahakamani
Kwetu uziguani hata kesi iwe vipi ukitaka unashinda tu hapo faili la kesi yako linapotezwa au linaungua moto hii hata mahakimu na majaji wanajua kwamba ukikutana na Mzigua uwezekano wa kufungwa ni asilimia 2% tu..tembea uone
 
Back
Top Bottom