Mmiliki na Dereva wa gari yenye usajili T 546 DGV wachukuliwe hatua kali za Kisheria

Hako kajamaa kaache kwanza, kataenda kuwekwa sehemu kwa musa pombe ikiisha kichwani ndio katajibu maswali.
 
watu wa Dar bna yaan mtu anasababisha ajali kwa uzembe na bado anakua na ujasiri wa kuwamwagia pombe? aje ajaribu huku mikoani aone nini tutamfanya

ihiiiiiiii (in magufuli voice)
 
Habari wakuu,

Hali yangu kiafya siyo njema sana, nikiwa natoka kutibiwa kwenye mojawapo ya hospitali humu jijini Dsm nimekutana na jambo baya linalosikitisha sana.

Dereva mmoja mwenye gari iliyo na usajiri wa T 546 DGV (Mimi sio mtaalamu sana wa magari, sijaweza kugundua upesi ni gari aina gani) ametaka kusababisha msiba mkubwa kwa Taifa kwenye kona ya kwanza iliyo na mteremko wa kasi wa Barabara inayoelekea Saranga kutokea Kimara Temboni.

Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhimili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Bila gari ile kugonga nguzo mojawapo ya fremu zile na kusimama mtaroni ni dhahiri kuwa eneo hilo kwa leo lingeshuhudia mauaji makubwa yanayoweza kuepukika.

Kibaya zaidi, katika hali ile ya taharuki huku manusura wakiwa na wenge kubwa la kusalimika, dereva anaanza kumwagia watu pombe zilizobaki kwenye gari huku akiwafukuza wasitoe msaada.

Najua baadae trafiki mtafika hapo. Chukueni hatua kali dhidi ya kijana huyo mwenye tabia ya hovyo isiyoelezeka.

View attachment 2644467
View attachment 2644469View attachment 2644470View attachment 2644471
Picha ya Mwisho: Kijana aliyevaa suruali ya khaki na shati jeusi mikono mirefu ndiye dereva.

Uhai ukipotea haurudi. Usiendeshe gari ukiwa umelewa.
Wangetia kiberiti hiyo gari pombe zingemwishia
 
Kama hamjampa kichapo wote ni wajinga,nilishaapa ukinigonga ukiwa umelewa kabla ya yote lazima nikushugulikie labda uje na kauli nitayokuelewa na siku hiyo niwe nimeamka na malaika wa huruma iliyopitiliza.
Haiwezekan starehe zako zikasababisha matatizo kwangu.
 
Huyo likely ni mjeda au TISS. Ndo zao hizo. Hudhani wako invincible. Kuna mahali nilikaa kwa muda karibu na kambi ya jeshi matukio haya yalikuwa ya kawaida tu. Walikuwa wanaparamia nguzo za umeme kila leo halafu wakitoka wanaacha gari hapo wanatembea kwenda kambini kwa miguu. No discipline whatsoever!
 
Angepigwa tu ndo mkaiita traffic vijana wa dar duuh,poleni lakini huyo inaonekana Mali ya mjomba hata uchungu hana ,mwenye gari ungemjua tu so huyo mpumbavu
 
Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhimili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Ni makosa kuendesha gari ukiwa huna utimamu wa kiakili, afya na ukiwa na kilevi...

Lakini Dar es Salaam ina changamoto kubwa ya watu kufanya biashara ndani ya hifadhi ya barabara, tena wengine hufanya juu ya lami kabisa wakigusa mistari ya mipaka ya lami...

Ningekuwa polisi hapo ni kukamata wote ,dereva mzembe na wote waliokuwa ndani ya hifadhi ya barabara kwa kuhatarisha maisha yao...
 
Wanaume wa Dar machoko sana... Kama mmeshindwaje kumtia hata makofi mjinga huyo
 
Habari wakuu,

Hali yangu kiafya siyo njema sana, nikiwa natoka kutibiwa kwenye mojawapo ya hospitali humu jijini Dsm nimekutana na jambo baya linalosikitisha sana.

Dereva mmoja mwenye gari iliyo na usajiri wa T 546 DGV (Mimi sio mtaalamu sana wa magari, sijaweza kugundua upesi ni gari aina gani) ametaka kusababisha msiba mkubwa kwa Taifa kwenye kona ya kwanza iliyo na mteremko wa kasi wa Barabara inayoelekea Saranga kutokea Kimara Temboni.

Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhimili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Bila gari ile kugonga nguzo mojawapo ya fremu zile na kusimama mtaroni ni dhahiri kuwa eneo hilo kwa leo lingeshuhudia mauaji makubwa yanayoweza kuepukika.

Kibaya zaidi, katika hali ile ya taharuki huku manusura wakiwa na wenge kubwa la kusalimika, dereva anaanza kumwagia watu pombe zilizobaki kwenye gari huku akiwafukuza wasitoe msaada.

Najua baadae trafiki mtafika hapo. Chukueni hatua kali dhidi ya kijana huyo mwenye tabia ya hovyo isiyoelezeka.

View attachment 2644467
View attachment 2644469View attachment 2644470View attachment 2644471
Picha ya Mwisho: Kijana aliyevaa suruali ya khaki na shati jeusi mikono mirefu ndiye dereva.

Uhai ukipotea haurudi. Usiendeshe gari ukiwa umelewa.
Si huyo hapo sasa. Kamateni mumpe kichapo mpaka pombe iishe.
 
Back
Top Bottom