TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

Averos

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Posts
993
Reaction score
703
Taarifa zilizotufikia leo asubuh ni kuwa mmiliki wa Kampuni za usafirishaji abiria ya Tashrif Hamoud Said amefariki Dunia

Innalillah wainna ilayhi raajiuun

=====

Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga ambae ni mmiliki wa mabasi ya Tashiriif, Hamoud Said Al Habsy amefariki dunia asubuhi ya leo Aprili 12, 2023 baada ya kudondoka ghafla wakati akitekeleza ibada ya swala ya Alfajir, mjukuu wa marehemu, Hamoud Salim Amri Said amethibitisha.

Mwili wa marehemu Hamoud ambae amezoeleka kwa jina la mzee Tashriif, unatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Alasir kwenye makaburi ya Mzalendo kata ya Mwanzange.

Azam news

Screenshots_2023-04-12-13-33-21.png
 
Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo (zaidi ya abiria 70 walikufa) likitoka Tanga kwenda Dar mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff.
 
Bila shaka Kuna urithi
Pole kwa wafiwa

Ngozi nyeupe hiyo huwa hawana shida kabisa akifa watoto wanaendesha biashara bila Shida

Angekufa mswahili saa hii hata maiti wangekuwa hawahangaiki nayo wanajadili mirathi na kutembezeana vipigo na kuficha mali kila.mtu akificha anachoweza

Hqpo bado ndugu waswahili nao utakuta mbio kuja kudandia mirathi
Weupe hawana Shida mzee ASAS wa ASAS group of Companies alifariki lakini cheki kampuni inakwenda bila shida

Watoto wanaiendesha vizuri

Afe mswahili watagombania mirathi hadi sufuria na vijiko na nguo zake hadi za ndani
 
Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo likitoka Dar kwenda Tanga mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff
Mto Msangazi, nilikuwepo pale that day. One of our staff made great efforts to swim and she saved some lives. It was a very sad moment! One of our RAAWU chairperson perished in the drown!
 
Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo likitoka Dar kwenda Tanga mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff
Hii Tashreef mbona iko miaka mingi sana nyuma kabla ya ajali au nimekosea?
 
Back
Top Bottom