TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

No Challenge wakati ule linapata ajali hawakubadili jina na kuliita Shengena au Air Bus! ule mziki ulifatana na ajali ya moto Shauri Tanga Sec school kama sijakosea.
Nafikiri lililopata ajali lilikuwa Shengena, ndio wakabadili na kuita Tashrif.
 
Wala usijali. Yote tushafundishwa hayo. Hakuna kitu kipya ambacho utatufundisha. Uislam umetufundisha kila kitu.

Mbali na hapo, mzee kafa kifo kizuri sana. Kaanguka akitekeleza Swala ya Alfajiri. Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan tena katika siku ambazo unapatikana katika moja wapo usiku wa Laylatul Qadr. Allah amsamehe na amrehemu. Hujui tu kwa Waislam mwisho mwema ni kitu kikubwa mno kwao.

Allah anipe mwisho mwema
Hakuna jipya chini ya jua!
 
Zaidi ya 70, unashangaa nini bongo hii +,?

gazeti la mwananchi:

Mwaka 1998, basi la No Challenge la mkoani Tanga lilipata ajali iliyosababisha vifo vya abiria wapatao 70 kutokana na kile aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro kudai ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi hilo. Baadaye basi hilo lilibadilishwa jina na kuitwa Tashrif lakini nalo lilisababisha vifo vya watu 27 katika ajali iliyotokea Korogwe.


https://www.jamiiforums.com/threads...usafiri-tanzania.1941892/page-5#post-41165046
Ajali haikusababishwa na mwendo mkali, bali ubishi wa dereva kulipitisha kwenye mkondo wa maji, likasombwa.
 
Wala hujui nini kinaendelea kuhusu mfungo wa Ramadhani.

Wazee na wagonjwa wameruhusiwa kula kabisa wala haina shida, pamoja na akina mama waja wazito, waliojifungua au walioko kwenye siku zao. Na ikiwa hawezi kuzilipa (kufunga baada ya kupona ugonjwa wake) basi anaweza kulipa kwa kutoa sadaka kwa masikini (nadhani kilo moja kwa siku).

Kwa hivyo hicho kifo chake kimesababishwa na maradhi yake aliyokuwa anaugua na siyo funga.
Inaeleweka hiyo, ila kuna wasiofuata ushauri huo.
 
Ajali haikusababishwa na mwendo mkali, bali ubishi wa dereva kulipitisha kwenye mkondo wa maji, likasombwa.
Upo sahihi hili gazette lilichanganya habari
 
Back
Top Bottom