TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

TANZIA Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Tashrif, Hamoud Said Al Habsy afariki dunia

Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo (zaidi ya abiria 70 walikufa) likitoka Tanga kwenda Dar mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff.
Mmh wengine ndio tulikua tunazaliwa
 
Taarifa zilizotufikia leo asubuh ni kuwa mmiliki wa Kampuni za usafirishaji abiria ya Tashrif Hamoud Said amefariki Dunia

Innalillah wainna ilayhi raajiuun

=====

Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga ambae ni mmiliki wa mabasi ya Tashiriif, Hamoud Said Al Habsy amefariki dunia asubuhi ya leo Aprili 12, 2023 baada ya kudondoka ghafla wakati akitekeleza ibada ya swala ya Alfajir, mjukuu wa marehemu, Hamoud Salim Amri Said amethibitisha.

Mwili wa marehemu Hamoud ambae amezoeleka kwa jina la mzee Tashriif, unatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Alasir kwenye makaburi ya Mzalendo kata ya Mwanzange.

Azam news

View attachment 2585301
RIP
 
Taarifa zilizotufikia leo asubuh ni kuwa mmiliki wa Kampuni za usafirishaji abiria ya Tashrif Hamoud Said amefariki Dunia

Innalillah wainna ilayhi raajiuun

=====

Mfanyabiashara maarufu jijini Tanga ambae ni mmiliki wa mabasi ya Tashiriif, Hamoud Said Al Habsy amefariki dunia asubuhi ya leo Aprili 12, 2023 baada ya kudondoka ghafla wakati akitekeleza ibada ya swala ya Alfajir, mjukuu wa marehemu, Hamoud Salim Amri Said amethibitisha.

Mwili wa marehemu Hamoud ambae amezoeleka kwa jina la mzee Tashriif, unatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Alasir kwenye makaburi ya Mzalendo kata ya Mwanzange.

Azam news

View attachment 2585301
Apumzike kwa amani,mchango wake katika sekta ya usafirishaji ni "REMARKABLE AND AKNOWLEDGED....kwa wazawa wa Tanga nafikiri wanaelewa hili...Anaekufa ni mtu taasisi ama biashara haifi,tunawatakia kheri walioachwa kusimamia waendeleE LEGACY kwa weledi Ili TASHIRIF ziwe na maendeleo endelevu
 

Bado tunaikumbuka ajali ya basi lake la "No Challenge" lililotumbukia mtoni likijaribu kuvuka daraja lililofunikwa na maji wakati wa mvua na kuua abiria karibu wote waliokuwemo (zaidi ya abiria 70 walikufa) likitoka Tanga kwenda Dar mmiliki akaona abadilishe jina la no challenge na kuyaita Tashriff.
Duh! Umenikusha mbali sana ,kwa kuwa nilikuwa mdogo mi nilijua ni basi la simba mtoto ndo lilipata ajali leo ndo najua sio simba mtoto ni la tashriff.
 
R.I.P tajiri.

Inaishi raskazone/share unaenda zikwa mwanzange.

Kifo hakibagui.
 
Arusha neno Bilionea hupewa mtu yeyote anayehama hama grocery au baa na kila anakopita ananywesha watu kuanzia wahudumu.Kuna taasisi moja ilifanya utafiti kuhusu walevi wa Arusha na tabia zao za kuhama kama njia mojawapo isambazayo ukimwi Arusha

Walevi Arusha waweza hama grocery su baa ndani ya saa mbili aweza kupitia grocery au bar zaidi ya tano .Anakunywa hapa anahama anaenda kwingine

Sasa jiji la Arusha mtu kama huyo humwita Bilionea
Arusha ukiacha kula bangi na kuanza kuvuta fegi wewe ni bilionea
 
Ukifikiria kifo muda mwingine unajionea maisha hayana maana shenzi kabisa. Yaani unahangaika kutafuta mali halafu inafika siku unaziacha zote unakwenda kupumzika kaburini peke yako ukiwa mpweke, ndugu zako, mke na watoto wanakuacha ulale peke yako.

Ndio maana mimi kwa kila ninachotafuta kwa jasho lazima nitenge 5% mpaka 10% ya kwangu peke yangu nikale bata nipoze moyo. Iwe mshahara, posho, hela ya dili au faida ya kitu fulani hata kama nimeuza kitu.

Yaani nikifa, kila nitakachokiacha duniani ujue 10% yangu nilishafaidi peke yangu kisha wenzangu huku nyuma ndio wajue wanafanyaje.

Haiwezekani nitafute kwa jasho halafu niwaachie 100%! Haiwezekani haiwezekani.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimeipenda Hiyo, kwa upande wa pili Uko sahihi mkuu
 
Apumzike kwa Amani!
Nachelea kukihusisha kifo chake na mfungo. Mfungo uzingatie umri, hali ya kiafya n.k. Waislamu wengi hupoteza maisha kipindi cha mfungo, kwani wanafanya mabadiliko ya vile mwili ulivyozoea kwa ghafla (abruptly), na pia kwa kiwango cha juu (severely). Kama kuna mushkeli ya kiafya, inakuwa ni sawa na kujiua mwenyewe.
Wala hujui nini kinaendelea kuhusu mfungo wa Ramadhani.

Wazee na wagonjwa wameruhusiwa kula kabisa wala haina shida, pamoja na akina mama waja wazito, waliojifungua au walioko kwenye siku zao. Na ikiwa hawezi kuzilipa (kufunga baada ya kupona ugonjwa wake) basi anaweza kulipa kwa kutoa sadaka kwa masikini (nadhani kilo moja kwa siku).

Kwa hivyo hicho kifo chake kimesababishwa na maradhi yake aliyokuwa anaugua na siyo funga.
 
Wa mwaka 47 watasaidia.
Baba wa aliyefariki ndio alikuwa anamiliki mabasi yaliyokuwa yanaitwa Shengena miaka mingi iliyopita. Alipofariki watoto wakagawana mabasi.
Mmoja akayaita ya kwake Air Shengena,
Mwingine Air bus na huyu aliyefariki akayaita ya kwake No challenge, baadaye Really no challenge.
Baada ya ajali ya msangazi ndio akabadili na kuwa Tashriff.
Hadithi za kwenye kahawa barabara ya 14 Ngamiani.
 
Mfano St Mary's schools

Vita ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji, Marehemu Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi​


VITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.

Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.

Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’

Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.

Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.

Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.

“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.

“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.

“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.

Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.

“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.

“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.

“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.

Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.

Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.

Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.

Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.

Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.

“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.

“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.

“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?

“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.

“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.

“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.

Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.

Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.

Source: Tanzania-Panorama
 
Back
Top Bottom