Ukifikiria kifo muda mwingine unajionea maisha hayana maana shenzi kabisa. Yaani unahangaika kutafuta mali halafu inafika siku unaziacha zote unakwenda kupumzika kaburini peke yako ukiwa mpweke, ndugu zako, mke na watoto wanakuacha ulale peke yako.
Ndio maana mimi kwa kila ninachotafuta kwa jasho lazima nitenge 5% mpaka 10% ya kwangu peke yangu nikale bata nipoze moyo. Iwe mshahara, posho, hela ya dili au faida ya kitu fulani hata kama nimeuza kitu.
Yaani nikifa, kila nitakachokiacha duniani ujue 10% yangu nilishafaidi peke yangu kisha wenzangu huku nyuma ndio wajue wanafanyaje.
Haiwezekani nitafute kwa jasho halafu niwaachie 100%! Haiwezekani haiwezekani.