TANZIA Mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) afariki

TANZIA Mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) afariki

Chibudee

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
1,775
Reaction score
2,404
Mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) na mkazi wa Usangi mkoani Kilimanjaro amekutwa amefariki dunia kwenye moja ya chumba cha wageni mtaa wa Dar es Salaam mjini Moshi.

Wakazi wa Arusha, Moshi, Same, Usangi nina uhakika mnayajua vyema mabasi haya.

Allah Ampunguzie Adhabu Ya Kaburi Inshallah.


Higer_KLQ_6129Q_bus.JPG


=====

Mmiliki mabasi ya Sahara akutwa amekufa kwenye nyumba ya wageni

Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi Mkoani Kilimanjaro, amekutwa amekufa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.

BY Janeth Joseph,

Moshi. Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi Mkoani Kilimanjaro, amekutwa amekufa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Januari 5, 2020, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani, lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu puani na mdomoni akakimbia.

“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.

Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa kwa uchunguzi.

Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.
 
Umeona Sehemu Nimesema Kwasababu Alikuwa Na Bus Acha Ku Panic Mkuu Relax Mwaka Bado Mpya Huu Hio Nidua Anayo Weza Ombewa Mtu Yyt Wewe Au Mm
Mungu ampunguzie adhabu?, Kwa sababu alikuwa na mabasi, acha kuingilia kazi za Mungu, kazi za Mungu hazina makosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom