TANZIA Mmiliki wa Mabasi Ya Tavavili Afariki Dunia

TANZIA Mmiliki wa Mabasi Ya Tavavili Afariki Dunia

Marehemu baba yangu aliniasa nisije miliki chombo cha abiria nitakufa kwa Bp na sukari na niliona jinsi alivyokuwa akipambana na madereva hadi nilipomshauri auze zile gari ilikuwa majanga mara hiki mara kile mzee PB, sukari da! Rip baba yangu
Ukiingia kwenye biashara yoyote bila uwezo na mikakati lazima upate wakati mgumu. Wewe unaona mtu anamiliki magari, hufanyi utafiti, huna uwezo, huna mikakati unakimbilia kuiga ukidhani mwenzako anafaidi, kwa nini usipate stress? Inaelekea baba yako hakujiandaa na akadhani biashara ya magari iko hivyo kwa wote.
 
Hakuna tajiri nimewahi kusikia ana afya imara, yaani ni kisukari,ugonjwa WA moyo n.k, WHY??
Are you kidding me? Huku ndiko tunaita kujiliwaza mwenyewe kwa sababu umeona uwezo huna. Sizitaki mbichi hizi.... Ndugu yangu ungejua mafukara wanavyosumbuliwa na kufa kwa magonjwa! Ni hivi: Fukara akifa siyo habari, na mtaa wa pili pengine hawatajua lolote. Lakini tajiri akiugua au kufariki, ni habari. Hivi unadhani huyu mwenye magari angekuwa mchuuzi wa nyanya chungu ungefahamu?
 
Hope msiba utakuwa Mbinga,tupeane update utakuwa sehemu gani.
 
Hakuna tajiri nimewahi kusikia ana afya imara, yaani ni kisukari,ugonjwa WA moyo n.k, WHY??
Wanakuwa na access ya vitu vyote hatarishi
Masikini anaweza akae mwaka hajanywa soda, ,tqjiri anaweza nunua kreti zima la soda .
Tajiri anawaza kufilisika , masikini hana cha kupoteza
 
images%20(6).jpg
 
Kisukari ni ugonjwa mbaya sana. Muda wowote ukiamua tu, unakuondoa. Yaani asubuhi ulikuwa mzima wa afya, jioni ikifika unaitwa marehemu.

Pumzika kwa amani tajiri yetu wa Tavavil
 
Marehemu baba yangu aliniasa nisije miliki chombo cha abiria nitakufa kwa Bp na sukari na niliona jinsi alivyokuwa akipambana na madereva hadi nilipomshauri auze zile gari ilikuwa majanga mara hiki mara kile mzee PB, sukari da! Rip baba yangu
Aisee hata mimi kuna wakati niliwahi kumiliki ka gari kamoja tu ka biashara! Nakumbuka moyo ulikuwa unaenda mbio muda wote! Kwa bahati mbaya sana nilipata dereva mwehu! Yaani ilikuwa ukiona namba yake tu akipiga, presha inapanda juu!

Wakati fulani bora kuwekeza tu kwenye real estates. Ingawa return yake ni ndogo, lakini walau unaishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom