Nawapa pole sana wafiwa, Mungu awafariji.
yatupasa kumshukuru Mungu kwa uzima anaotupatia kila iitwapo leo, pia tukumbuke kuwa, uwe na mali, usiwe na mali, uwe maarufu usiwe maarufu, usiogope kifo, ogopa kumkosa Mungu maishani mwako kwasababu ukifa bila Mungu maishani huna kwa kwenda ukifa zaidi ya moto wa milele. maisha ya hapa duniani ni mafupi. Mpokee Yesu sasa na uishi maisha matakatifu ili upate uzima wa milele. Yesu alisema, yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi, kwa maana ya kuwa na uzima wa milele. kuna mkulima aliwahi kuazima shamba moja, akagundua kwenye lile shamba kuna lulu yenye thamani kubwa na mwenye shamba hakujua hilo, alienda akauza vyote alivyo navyo akalinunua lile shamba ili aipate ile lulu. ilipo hazina yako ndipu utakapokuwepo na moyo wako.
kiburi na ufahari wako wa hapa duniani utaishia hapahapa duniani. hata tajiri alipokuwa kuzimu alipomwona maskini lazaro ameketi pamoja na Ibrahim alifikiri bado ana ubavu wa kumtumatuma, ati amtume maskini huyo arudi duniani akawaambie ndugu zake wasifanye maovu wasijepata kile alichokuwa akipitia motoni, akaambiwa haiwezekani wapo hukuhuku duniani wanaofanya hiyo kazi wasiposikilizwa wataenda motoni vilevile. Mkumbuke Mungu siku za maisha yako, kabla haujaikosa nafsi hata ya kunyanyua ulimi tu uombe msamaha mbele zake, tubuni mkabatizwe kila mtu kwa Jina lake Yesu mpate ondoleo la dhambi nanyi mtapata kipawa cha Roho Mtakatifu, na huo ndio uzima wa milele kuanzia hapa duniani hata milele yote. kuishi na Mungu moyoni.
Achaneni na imani za ajabu zisizookoa, zenye mungu asiye na nguvu anayehitaji msaada wa wanadamu wampiganie au kumtetea, Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo ndiye anayetawala, zaidi yake hapana mwingine naye anazo nguvu za kutosha hahitaji msaada wa mwanadamu ampiganie. anajitosheleza peke yake. na ni kwa njia ya Yesu Kristo peke yake, utamwona Mungu na kupona ile hukumu ya milele, manabii wengine wooote ni upotevu na hawatakufanya umwone Mungu kwasababu hawakufa kwa ajili yako, walikufa kwa nafsi zao tu. Yesu Kristo alitoa uhai wake afanyike kafara la ukombozi wa maisha yako, kwa kifo chake alikufa ili kulipa deni lako ya kifo na adhabu za aina yote, alipata huzuni yooote to the extent ya kutoka jasho la damu ili sisi tusihuzukine, Mwenyewe Yesu alihuzunika ili sisi tusihuzunike, alibeba masikitiko yetu yote kwasababu alisikitika badala yetu, alijeruhiwa na kuchubuliwa, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
yeye amelipa kila kitu kukuwezesha wewe na mimi tusamehewe dhambi na kuupata uzima wa milele, lakini uchaguzi ni wa mtu binafsi, kuchagua uzima upote au kuwa na kiburi na kupotea milele. siku ya mwishi hakuna atakayekuwapo wa kumlaumi mwingine, kila mtu atajilaumu mwenyewe kwasababu deni looote la dhambi lililipwa, lakini watu wakachagua upotevu badala ya uzima, alishaweka mazingira yoote ya kumfanya mwanadamu apate uzima wa milele kuepuka jehanum lakini watu wanachagua mauti badala ya uzima, itakuwa juu yao wenyewe kujilaumu.
mwenye sikio na asikie maneno haya ambayo Roho anawaambia!
KAMA UNATAKA KUMPOKEA YESU LEO USAMEHEWE DHAMBI ZAKO, RUDIA SALA HII PAMOJA NAMI!
" EEh Bwana Yesu Kristo, nakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi, nimefanya dhambi kwa kunena, kwa kutenda na kwa kwa kuwaza na kwa kutokufanya yale yanayonipasa kufanya. dhambi ninazo zijua na zile nizisozijua. Ninaamini moyoni mwangu kwamba wewe ndiwe njia kweli na uzima, na ni kupitia wewe nitasamehewa dhambi zangu na kuupata uzima wa milele. Ninaomba unisamehe dhambi zangu, unioshe kwa Damu yako takatifu, uchukue dhambi zangu na magonjwa yangu na mizigo yangu yote, Niongoze nikufuate wewe katika Maisha yangu. Kwa Jina lako takatifu ninaomba, Amen!.
Mungu akusaidie, kwa Jina la Yesu.