Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Watu waliokuwa wanatumia pikipiki wamempiga risasi mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari na kumpora begi na kisha kutokomea na pikipiki yao.
Mtu huyo amepigwa risasi na kufariki papo hapo.
inauma sana
Natamani pikipiki zitolewe kabisa mjini na zikionekana zipigwe risasi
wafanyabiashara ni wagumu mno hapo alikuwa anabania sh laki moja tu ya kuwapa police wamsindikize bank imecost maisha yake lakini ndio kanda maalum hiyo mungu amlaze mahali pema peponi Amen
 
Tatizo ni siyo pkpk,tatizo ni watumia pkpk...ni sawa na kazi ya mikono ikishirikiana na viungo vingine ni kutimiza majukumu sahihi,lakin wengine wanatumia ktk kutimiza malengo mabaya...!vitabu vya dini vimeruhusu adhabu ya kifo kwa kila auwaye kwa kusudio,lkn wanaodai haki za binadam mpk na ushoga,wameckilizwa mno kiasi cha hukumu ya kifo kutokuwa na mashiko,hii inatosha kuwafanya watu wasio ogopa mungu kuuwa kwasababu hakuna sheria wanayo iogopa
 
inasikitisha kwa kweli.ila kama walikuwa na hela nyingi si wangeomba ulinzi?tatizo ni kwamba hawataki pesa zao zijulikane
 
Naomba Ujambazi utangazwe ni janga la kitaifa. Kila kukicha majambaz. Hv ni nani anawapa taarifa kuwa mtu fln ana fungu la hela? Tafakari chukua hatua
 
Sasa huyo naye akili zake sio sawa sawa...utatembeaje na pesa nyingi usiku tena bila ulinzi. Au ndio katoka kufanya ufisadi. Matatizo mengine ni ya kujitakia. Sasa hivi maisha magumu sana watu wananusa pesa.
 
Matukio ya unyang’anyi wa fedha kwa kutumia silaha wakati wa mchana kwa sasa katika jiji la Dar es salaam yamekuwa ni mengi sana. Kinachowafanya watu hawa kutumia usafiri wa pikipiki ni kutafuta wepesi wa kukimbia na kupenya hata vichochoroni kwa urahisi ili wasiweze kukamatwa. Lakini pia wakitambua kabisa kwa kitendo cha kuwa na silaha wananchi wa kawaida hawawezi kuthubutu kufanya ufuatiliaji wa aina yyte ile kwa kuhofia kipigwa risasi. Kwa kweli siwezi kuwatupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio haya ingawa ni wajibu wao na kazi yao kuhakikisha usalama wa raia na mali zao vyote vinalindwa. Sababu kwa idadi ya polisi waliopo katika jiji letu ni ndogo sana hawawezi hata kidogo kuweza kuwepo kila mahali matukio hayo yanapotokea. Lakini pia hili ni tatizo la kitaifa kwamba hatuna vifaa vya kutosha vya kiusalama kuweza kudhibiti matukio kama haya hasa kutokana na miundombinu ya jiji la Dar es salaam. Kikubwa ni sisi wananchi kuonesha nia ya dhati kupambana na matukio haya kwa kuwapa ushirikiano Polisi kwa namna moja au nyingine kuhakikisha tunawadhibiti watu hawa. Kwa sababu watu wanaofanya matukio haya tunawajua na tunaishi nao mitaani ila watu tumekuwa tukiwaficha.
 
JK aliingia kukiwa na kasi kubwa ya Ujambaz na anaondoka kukiwa kasi kubwa zaid ya ujambaz na mauaj,,,,,ndio maana tunasema kwa sasa Tanzania si kuwekeza kwenye mavifaru tuuu,tuwekeze kwenye teknolojia jamani,hawa majambaz wanachukua pesa kwenye main roads,,,why hakuna kamera za kiusalama????
 
polisi siwapend na sitawapenda,,,

watu kama nyie huwa nawafananisha na mtoto wa miaka 5 ambaye anazira kula chakula kwavile kachapwa na baba yake au anasema kabisa baba simpendi. Lakin siku kama hana hela ya kununua icecream anaenda kuomba tena kwa baba yule yule..... Ww unaongea hapa lakin siku ukitiwa ngeu lazma uende polis kufungua kes au kuchikua pf3 au ukiibiwa unakuwa wa kwanza kujichekesha polis huko huko. Uwapende au usiwapende lakin utaenda tu kuwalilia msaada
 
kwenye shida ndio mnawakumbuka polisi?? Lakn hao ndio tunawau,tunawaita njaa kali,tunawaita mbwa tunawadharau kama hatujui wapo kwa ajili ya nn..... Mm naomba polis walegeze kamba ili ijujlikane mwanaume ni nani na mwanamke ni nan?? Viva majambaz pigen kaz mjin hakuna kizuiz polis wamekata tamaa na mambo wanayofanyiwa na serikali na wananchi. Wapo kwenye mgomo wa kimya

hawajui kazi usiwatetee...!
 
Watu waliokuwa wanatumia pikipiki wamempiga risasi mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari na kumpora begi na kisha kutokomea na pikipiki yao.
Mtu huyo amepigwa risasi na kufariki papo hapo.
inauma sana
Natamani pikipiki zitolewe kabisa mjini na zikionekana zipigwe risasi

mitaa ya airport katika mkoa gani.!?
 
Back
Top Bottom