Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

quote_icon.png
By The bold

Bibie ukituliaga unaandika vitu murua kabisa mpaka unanikosha roho!!!

1000likes

Ahsante, ukinisoma kwa utulivu utaendelea kupata faida kubwa sana, jitahid.
 
Tuelewesheni je Silvanus Mzeru = Mbena Malumbi?Mbena ninamfahamu kama TUSS mwenye hela sana!!!!!! Ni mtiifu sana kwa mfalme ktk masuala ya miradi. Sasa kama polisi wameshajipanga kulinda ile miradi ya marehemu bigwa tujiulize miradi ile ni ya umma au serikali? Serikali haifanyi tena biashara tangu ilupoamua kuwa na sera ya Privatisation!!!! Sasa ni miradi ya nani mpaka ikazingirwe baada ya the so called mmiliki kuuawa under the cover ya ujambazi??!! Tusuburi Single nyingine ya Kova.
 
namhitaji apa Yericko Nyerere

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?
 
Last edited by a moderator:
R.I.P Silvanus Mzeru!huyu ndugu kwa huku Morogoro alikua anajulikana zaidi kwa jina la Mbena Marumbi,ndie aliekua mwenye resort mpya zijulikanazo kwa jina la Chilakale!ukweli ni pigo kubwa kwa wadau wa Morogoro hasa wale wafanyakazi wa Chilakale Resorts!
 
Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.

duuuh akili za ccm ni laana tuuu......hazkutoshi weweee
 
May his soul rest in peace, tulimpenda na alitupenda, Pumzika kwa amani Silva
 
Umeona kitambulisho chake, au uliwahi kuingia ofisini kwake, au .....
umesikia kutoka kwa watu tu.

Ni TISS kati ya wale ambao nature ya kazi zao zina wa expose. Mbena= Mzeru anajulikana sana na kazi yake hiyo. Nikuulize swali rahisu. Hivi wale walinzi wa Rais au viongozi waandamizi wa serikali wanajificha? Hapana, ni rahisi kuwafahanu. Hivyo basi TISS staff wako aina tofauti na si rahisi kuwafahamu wote. Wachache ndiyo wabaofahamuka na wengi hatuwajui wako maofisini kila mkoa na wilaya na makao makuu wengine back na wengine front office katika ofisi zao. Wengine tuko nao maofisini na sehemu zit hadi washona viatu, hawa ni informers au wanakuwa maofisini kwa kazi maalum!!! du nisiwre msemaji wao!!!
 
wakuu,huyo alikua ofisa wa usalama wa taifa marehemu mzelu,yasemekana wabaya wake aliwastukia toka uwanja wa ndege alipokua anapokea mzigo,ni noma,alikua katika kitengo cha madawa ya kulevya,huyu jamaa alikua tajiri mno,ila inasemekana wakubwa walikua wanawekeza kwake,maeneo ya chanika jamaa kajenga sio mchezo,acha kabisa,ana bar kubwa tu na mahali ambapo hua analaza magari,chanika kwa mbele,alikua na wafanyakazi wengi tu na jamaa alikua na utata katika kulipa mshahara,kuna majumba/maghorofa kayajenga ndanindani mpaka mtu unashangaa na yamezungushiwa fensi kubwa sana,inasemekana katika briefcase aliyoporwa kulikua na hela nyingi pamoja na sembe,hapa ndio tunapata shaka na usalama wa taifa,badala ya kufanya kazi za usalama wa taifa,wanafanya kazi ya kufanya deals chafu na wakubwa,na hii habari najua itapotezwa kimyakimya.
 
Back
Top Bottom