BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mtu mmoja kati ya watu 8 waliokamatwa, wakituhumiwa kuiba mali za waliofariki katika ajali iliyotokea Korogwe mkoani Tanga, ikihusisha gari la mizigo aina ya Fuso na gari la abiria aina ya Coaster, lililokuwa likisafirisha mwili kwa ajili ya maziko wilayani Rombo na kusababisha vifo vya watu 20, amekutwa amejinyonga katika mahabusu ya polisi iliyopo Jijini Tanga.
Mkuu wa Mkoa huo, Omari Mgumba ,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akibainisha kuwa, mtuhumiwa huyo ni yule ambaye wakati wa upekuzi nyumbani kwake alikutwa na baadhi ya vitu ikiwemo simu, begi na nguo zinazoshukiwa kuibiwa kwenye eneo la ajali vikiwa na damu.
ITV