Mmoja kati ya Watanzania waliokuwa hawajulikani walipo Nchini Israel, yabainika amefariki Dunia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa masikitiko na huzuni imetangaza kifo cha Clemence Felix Mtenga, Kijana Mtanzania ambaye ni miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa Mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo tangu yaliyopotokea mapigano October 07, 2023 nchini Israel na katika maeneo ya Wapalestina hususani Gaza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara haijasema chanzo cha kifo chake na Mji ambao amefia lakini imesema Clemence alikuwa ni miongoni mwa Vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo kuijulisha Familia na inaendelea kuwasiliana na Serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi zinakamilika kwa wakati.

Wizara imesema inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo “Wizara inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu

IMG-20231117-WA0449.jpg
 
Miongoni mwa mateka nchini Israel amekufa

Habari zaidi zinakuja

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa masikitiko na huzuni imetangaza kifo cha Clemence Felix Mtenga, Kijana Mtanzania ambaye ni miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa Mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo tangu yaliyopotokea mapigano October 07, 2023 nchini Israel na katika maeneo ya Wapalestina hususani Gaza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara haijasema chanzo cha kifo chake na Mji ambao amefia lakini imesema Clemence alikuwa ni miongoni mwa Vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo kuijulisha Familia na inaendelea kuwasiliana na Serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi zinakamilika kwa wakati.

Wizara imesema inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo “Wizara inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu” #MillardAyoUPDATES
 
Wizara ya Mambo ya Nje na USHIRIANO wa Kimataifa.
Hivi serikali yetu haitoi security alert kwa wananchi wa Tanzania hasa inapotokea migogoro kama hii ya kivita, kuzuia wananchi wasiende kwenye nchi zenye machafuko ambapo kuna terrorist attack, kidnapping na vita? hili suala inabidi tuliangalie kwa umakini.
 
Hivi wakati Yaser Arafat akiwa Kiongozi wa Palestine,Hamas walikuwa wanamuunga mkono au hapana?

Nauliza hivi Kwa sababu Nina hakika Serikali yetu ingepitia Iran ambako tuna mahusiano mazuri wao Iran wangewatafuta Washirika wao Hammas wangeqaachia Vijana Wetu.
 
Back
Top Bottom