Mmoja kati ya Watanzania waliokuwa hawajulikani walipo Nchini Israel, yabainika amefariki Dunia

Mmoja kati ya Watanzania waliokuwa hawajulikani walipo Nchini Israel, yabainika amefariki Dunia

Wazo zuri sana ila watu wetu wa Diplomasia hawana akili kama zako. Wengi wanaenda kwenye Diplomasia sababu ya safari za nje tu. Inasikitisha mnoo

Mkuu ningependa iwe hivyo, lakini sidhani Hamas ilikuwa kwenye mood ya discussion, walikuwa kwenye kilele cha ushindi...na hawakutegemea response ya Israel itakuwaje......Israel ilichofanya imekuwa ni juu ya kiwango walichofikiri.
 
Miongoni mwa mateka nchini Israel amekufa

Habari zaidi zinakuja

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa masikitiko na huzuni imetangaza kifo cha Clemence Felix Mtenga, Kijana Mtanzania ambaye ni miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa Mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo tangu yaliyopotokea mapigano October 07, 2023 nchini Israel na katika maeneo ya Wapalestina hususani Gaza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara haijasema chanzo cha kifo chake na Mji ambao amefia lakini imesema Clemence alikuwa ni miongoni mwa Vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo kuijulisha Familia na inaendelea kuwasiliana na Serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi zinakamilika kwa wakati.

Wizara imesema inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo “Wizara inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu” #MillardAyoUPDATES
Mateka huyo alitekwa na nani?
 
Mkuu ningependa iwe hivyo, lakini sidhani Hamas ilikuwa kwenye mood ya discussion, walikuwa kwenye kilele cha ushindi...na hawakutegemea response ya Israel itakuwaje......Israel ilichofanya imekuwa ni juu ya kiwango walichofikiri.
Yes, Hamas hawakufanya tathmini ya athari na hiyo ndio tatizo la kufanya maamuzi kwa kukurupuka na unapokuwa mtu uliyekata tamaa. Ila ninaamini kwa wazo lako hapo juu lingetumika na best negotiator lingefanya kazi vizuri tu.
 
Wazo zuri sana ila watu wetu wa Diplomasia hawana akili kama zako. Wengi wanaenda kwenye Diplomasia sababu ya safari za nje tu. Inasikitisha mnoo
Kabisa, hata tungepiga mayowe tu na vishindo kama vya wakoma, hata tungemwita balozi wa palestina, tungepeleka delegation iran, naimani kabisa kijana wetu pamoja na wengine wangetoka salama, kama kile kibibi kiliwasifia hamas kuwa ni watu wema kikaachiwa sie hiyo mbinu ilitushinda kweli? Vijana walikuwa 260 wamebaki 258 hata hatujui wanaendeleaje? Wanaendelea na shule au ndo wako kwenye mahandaki au wamevalishwa combat
 
Kusema tuu amefariki bila kutoa maelezo ya amefariki vipi haitoshi.

Tuliambiwa wamechukuliwa mateka Sasa mbona hamjatueleza kifo chake kimesababishwa na nini?

Semeni oparesheni ya Kisengerema ya Israel imemuua Kijana Wetu.
Na aliyemteka Mtanzania mwenzetu tumfanyeje?Mbona hata rangi yetu haifanani na Waisrael.Mbona Hamas walishindwa kutambua kuwa huyu ni mwafrika na siyo mzungu?
 
Haijalishi lakini kumfanya binadamu mwenzako kuwa daraja la pili kama Israel inavyo wachulia wapalestina katika dunia ya sasa ni uovu ulio vuka mipaka.

Nani kamfanya mwenziye daraja la pili.....Narudia tena soma Charter ya Hamas mkuu....Utajua Mhayahudi ni daraja la ngapi....Hamas wamefuata exactly kama Quran ilivyosema....Hivi ni nani katawala Gaza toka 2005? Umeme na maji vyote ni kutoka Israeli....Huko ndio kuwa daraja la pili?
 
Na aliyemteka Mtanzania mwenzetu tumfanyeje?Mbona hata rangi yetu haifanani na Waisrael.Mbona Hamas walishindwa kutambua kuwa huyu ni mwafrika na siyo mzungu?
Ilikuwa ni swala la kuzungumza nae angemwachia maana Target sio Mtanzania na kwenye ambush hakuna kuulizana ID hiyo ni ya baadae sana.
 
RIP,,,ila huwa siwaamini sana watu weupe especially Israel walivyokua wabaguzi isijekuwa wametelekeza
 
WAkulaaniwa ni Israel au hao wafilisti waliosababisha vita hiyo na kuwateka watoto wetu kisha kuwaua, ?
 
Na aliyemteka Mtanzania mwenzetu tumfanyeje?Mbona hata rangi yetu haifanani na Waisrael.Mbona Hamas walishindwa kutambua kuwa huyu ni mwafrika na siyo mzungu?

Mkuu nimekwambia walikuwa kwe state ya euphoria...high excitement......Wamepige selfie na maiti...Wamepiga simu nyumba kwa mama zao na familia zao.....Hamas wamewafundisha kuumua Myahudi kuna thawabu ya aina yake.....Hawakuwa kwenye akili timamu mpka Israeli ilipoaanza mashambulizi.
 
Wazo zuri sana ila watu wetu wa Diplomasia hawana akili kama zako. Wengi wanaenda kwenye Diplomasia sababu ya safari za nje tu. Inasikitisha mnoo
Wangetumia mbinu ya kuzungumza na Iran wangefaulu lakini kutegemea Mzayuni directly wakati ni adui isingewezekana
 
Timu Hamas mlivyoenda kuishambulia Israel kwa sababu zenu za kishamba hamkujua kuwa kuna Raia wa Tanzania huko wasiokuwa na hatia?Na bado mmetuulia kijana wetu na bado unatoa laana kwa mtu ambaye hakuhusika pumbavu.
Israel mkoloni lazima ashambuliwe.Mateka walishikikiwa Ili mazungumzo yafanyike Sasa kuua mateka wanakofanya Israel Kwa kisingizio Cha kuwatafuta ndio wamefaulu?

Upumbavu wameua Kijana Wetu na nyie punguani mnashangilia.

Hamas wako sahihi maana wanapigania ardhi Yao.
 
RIP,,,ila huwa siwaamini sana watu weupe especially Israel walivyokua wabaguzi isijekuwa wametelekeza

Mkuu unasoma historia......Kuna kiwango cha ubaguzi kama ambavyo Wayahudi wametia ulimwenguni.....Unajua maana ya Neno Getto.......ni sehemu za watu waliochoka, maskini......wanaobagulia....hayo ndio yalikuwa makazi ya Wayahudi ulaya.....ndio chanzo na neno hilo.....Soma historia mkuu.
 
Waisrael na Wapalestina Weusi wpao wengi tu mbona. Usikariri
Lakini sura zao na sisi ni tofauti,Mnigeria na Mtanzani ni Waafrika lakini kwa sura ni tofauti.
Israel mkoloni lazima ashambuliwe.Mateka walishikikiwa Ili mazungumzo yafanyike Sasa kuua mateka wanakofanya Israel Kwa kisingizio Cha kuwatafuta ndio wamefaulu?

Upumbavu wameua Kijana Wetu na nyie punguani mnashangilia.

Hamas wako sahihi maana wanapigania ardhi Yao.
Wewe ni mpumbavu na muuaji huwezi nishawishi kwa lolote.
 
Israel mkoloni lazima ashambuliwe.Mateka walishikikiwa Ili mazungumzo yafanyike Sasa kuua mateka wanakofanya Israel Kwa kisingizio Cha kuwatafuta ndio wamefaulu?

Upumbavu wameua Kijana Wetu na nyie punguani mnashangilia.

Hamas wako sahihi maana wanapigania ardhi Yao.

Nani kashambulia Mkuu....Ulidhani Israel itaingia mkenge wa majadiliano kama kila wakati inavyofanya...? Kwanza kuna uhakika hao mateka bado wapo.....Kwanza ni kuwafundisha adabu.....halafu Israel itaangalia kama wateka wapo.....Kwa taarifa za Hamas, mpaka leo wamekufa Wapelestina 12,000. Hamas haikufikira hayo.....na bado.....hatujui nini kitaendelea...Hata Iran na Waarabu wenzao hawajui la kufanya.
 
Wangetumia mbinu ya kuzungumza na Iran wangefaulu lakini kutegemea Mzayuni directly wakati ni adui isingewezekana
Kuna mtanzania alitekwa congo akajiongeza akawa ndio mpishi mkuu kufua nguo za makamanda akawa anatengeneza madikodiko ya kufa mtu, nyani anamtengeneza supu huwezi amini, mwisho wa siku walimwachia akasalimie familia, hadi leo anapigiana simu na washakaji, sasa sie tulishindwa kweli kujiongeza
 
Back
Top Bottom