Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, ameshiriki Mkutano wa Saba wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano wa Ulinzi na Usalama kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji (Joint Permanent Commission for Defence and Security – JPCDS), uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umefungwa leo, tarehe 7 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyasaho, katika Ukumbi wa The Aga Khan Diamond Jubilee.
Mkutano huo umejikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika masuala ya ulinzi na usalama.
Katika mkutano huo, Mhe. Mmuya ameshiriki pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Lucy Kabyemera, na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bw. Hamdouny Mansoor.