Mna maoni gani kuhusu hili suala la uvamizi wa Al-Shababu hapa Palma?

Mkimaliza kubishana nitawaambia kitu kwa nini vita haziishi Congo
 
Kuwa tyr kuna kampuni za kizungu(mabeberu) zinachimba ndio sababu ya kutokuoa na conflict of interest?

Unajifanya hujui nini kilifanya vita isiishe upesi Cabinda? Hujui kuwa ni baada ya vita baridi ndio Savimbi mabeberu walimtosa? Acha porojo zako.
so beberu ni nani!!!????
 
Mkimaliza kubishana nitawaambia kitu kwa nini vita haziishi Congo
Pitia huku then niambie kuna tofauti gani kati ya mabeberu kuchimba madini kukiwa na vita ila washindwe kukiwa na amani!!!

 
Ambacho sijaelewa mbona wakati wa amani wanapewa mikataba ya kinyonyaji kabisa kuchimba rasilimali ssa wategemee vikundi vya magaidi Ili iweje.

Mfano hapo msumbiji wana mikataba halali kabisa ya kuvumbua na kuchimba gesi ssa hapo gaidi wamhitaji wa nini?

Tanzania hapa zaidi ya miaka 20 wanaochimba ni mabeberu tena mikataba ya kijizi kabisa ssa walihitaji magaidi hapa TZ ili tuwape hyo mikataba?

Unaweza tusaidia hta jina la nchi moja ambalo madini yake hayachimbwi na beberu kwa sababu tu ina amani.

Na mimi ntakutajia list ya nchi zaidi ya 20 ambazo zinatwangana kwa miaka mingi sasa na hakuna madini.
 
Hujaelewa point ya msingi, nchi ya Africa ikiwa na raisi puppet kwao hutaona vita ya moja kwa moja unless ameanza kupingana nao, nchi kama Tanzania walichokifanya ni kuwatengenezea viongozi wa juu urahisi wa kuficha fedha zao nje, mfano Switzerland ambazo zinaongeza mzunguko kwao hivyo inakuwa rahisi hata wao kujichotea mali hapa bila bugudha kutokana na kuwa na siri za viongozi...

Sio lazima vita, inaweza ikawa blackmail na vitu kama hivyo, hujawahi sikia kisa cha mwanamfalme mmoja na issue ya Tembo, madawa ya kulevya, kunyongwa na umiliki wa bandari? Beberu ni beberu, awe mchina, mzungu, muafrika na wengineo.

Hakuna nchi isiyo na kitu chochote ardhini, kumbuka hata makinikia tuliambiwa ni vumbi tu. Tunahitaji kuwekeza sana kwenye elimu kuweza kupambanua yaliyomo na manufaa yake, mzungu huko katutangulia kufanya research nyingi sana duniani tena kwa ushirika wa wazawa wa eneo husika.
 
Bro Hichi kitu ndivyo kilivyo Wanasema WAJINGA NDIO WALIWAO Unajua yule kagame ndio alipindua leo tunaiona Ruanda inavopaa yalikuwa mambo kama haya hapa lkn akatokea kidume akasema nitakula nao kenge hawa, naam akapatia .
 
Eeenh, wewe kweli ni chizi. Cocaine na Alfganistan wapi na wapi?

Halafu mtu apigane vita kwa sababu ya mirungi?

YEHODAYA, ukiendelea hivi utazeekea JF bila ya kupata uteuzi wa aina yoyote hata kama huyo jamaa atakaa madarakani miaka 50!
Yaani Marekani akapigane vita Afghanistan miaka 10,atumie zaidi ya 2trillion USD kwa sababu ya mirungi na cocaine wakati anaweza kuingiza pure cocaine kutoka Mexico na Colombia bila kutumia nguvu. πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ .Hesabu za kijinga sana
 
Nchi tajiri kama Tanzania inakosaje capital ya kuwekeza kwenye uchimbaji madini?
 
Nasikia kiongozi wa hao jamaa ni mtanzania na kwa sasa anatafutwa na police wa Tanzania,akivuka mpaka kuja kwa waganga wake,wanamdaka na kumpoteza
 
Nchi tajiri kama Tanzania inakosaje capital ya kuwekeza kwenye uchimbaji madini?
Swali zuri ila ni swali la kuwauliza wanasiasa,watoe majibu sahihi...
 
Mtanzania yoyote anaechimba dhahabu 70% yake 30%mapato na hii ni kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ila kwenye iyo 30% SIO yote huenda serekalini ss sijui unajaribu kusema nn??
 
Awewe beberu,mchina au mhindi,Hakuna anayhetaka kufanya biashara sehemu yenye vita wakati anaweza ku loby viongozi wajinga wajinga wa Africa na akapewa umiliki wa rasilimali hata kwa 90% na kuchimba kiulaini kabisa..
 
Mtanzania yoyote anaechimba dhahabu 70% yake 30%mapato na hii ni kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ila kwenye iyo 30% SIO yote huenda serekalini ss sijui unajaribu kusema nn??
Wachimbaji wadogo wanachangia 6-10% ya mapato yote ya madini meaning ni kama tone la damu baharini!!

Hoja ni kwamba bado mabeberu wanafaidika na dhahabu zetu whether kuna vita ama lah kwahiyo napinga hoja kwamba ili wanufaike na madini eti ni lazima watumie magaidi.

Hyo pesa ya kufadhili magaidi si bora watumie kuhonga serikali ili wapate mikataba inayo wa favor.
 
Mtu mweusi siku zote hutoa kisingizio hafifu kuoanisha laana yake na mafanikio ya mzungu jambo ambalo linasababisha aendelee kuwa mtumwa siku zote duniani.

Je kwa nini hao wanaoitwa magaidi wawe ni wa kutoka imani moja tu na kama wanatumiwa kwa nini iwe ni wao tu kwa nini wasikatae kutumiwa na wale wanaoamini kwamba ni makafiri??

Siku zote siikubali hii porojo ya kusema haya matukio yanachochewa na wazungu wakati wahanga wakubwa wa huu uovu ni hao hao wazungu. Je huko Kibiti walikoanzia kwenyewe kulikuwa na rasilimali gani. Matatizo ya waafrika yanasababishwa na waafrika wenyewe, huo ndio ukweli.
 
Hapo ni kupigania pesa za ges, watakua wamerushana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…