Pre GE2025 Mna uhakika CHADEMA ikishika dola italeta utofauti wowote?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Nilikuwa nawaza hapa kwamba CCM ndio chanzo cha matatizo yote haya, lakini hapana wananchi wanaoikalia Tanzania ndio chanzo cha mfumo mbovu wa siasa zilizopo nchini.

Mohamed Kawaida, Tulia Akson nk. (Tunaowaona kama wajinga), wanaweza kuwa wapinzani wakubwa ikiwa Chadema ingekuwa madarakani, fikiria kuhusu Mchungaji Peter Msigwa.

Kenya kwa mfano, migogoro na lawama kwa viongozi haijawahi kuisha mbali na vyama tofauti tofauti kushika dola. Tofauti na kwetu Chama kimoja, lakini Kenya ni political stable kuliko Tanzania kwasababu ya wananchi wake.

Freeman Mbowe angekuwepo Nafasi aliyopo Samia, huenda Samia, au Majaliwa wangekuwa wapinzani pia.

Jitihada kubwa ingewekwa kwenye kuelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu na kuwaonyesha nguvu yao kwanza.

Nachokiona mimi ni kwamba Serikali itaendelea kufanya inachokitaka na kuendelea kuwepo, tutalia kwenye tweets online nk. baada ya siku tunarudi hatua tuliyotoka! Nini kifanyike?
 
itafanya nchi ichangamke zaidi hatuwezi ongozwa na chama kimoja toka uhuru tukitegemea mabadiliko hasa yakiuchumi ,kisiasa na kijamii ni uongo tutegemee ccm itubadilishe hatukatai wazee wa ccm vilikua vyuma kweli ila wamekuja tengeneza kizazi weak sana kuelewa siasa ni nini mwisho wa siku wanakuja tumia nguvu zaidi kuliko akili mfano kuna haja gani ya asilimia zaidi ya 95% bungeni kuwa chama tawala ungali hawasaidii kihoja na kimaslahiii (wote tunajua walivyoingia) kutofata katiba ungali katiba yetu ni mbovu, nk kimsingi kama taifa inabidi ifanyike overhaul ya maana madaraka yasiwe ya chama kimoja kinajisahau jumlisha mizaha isiokuwa na tija kwa taifa baada ya miaka 25 tutakuwa wapi?
 
Madini matupu haya👏. Hatuko tayari tena kutawaliwa na chama kimoja kwa shuruti. Hivi vikundi vya kuteka watu ni ili kufanya watu wawe waoga na watawaliwe na chama kimoja tu.
 
Tofauti lazima iwepo, japo kuna mambo yatabaki vilevile tu.

Mfano, tunaweza badili katiba, kuboresha sera mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kuimarisha utawala wa sheria.

Mambo ambayo naona yatasalia kama yalivyo ni uzembe kazini, ufisadi na kupendeleana n.k. Haya ni mambo ambayo watanzania wanakua nayo.
Kuyabadili ni suala la kijamii kuliko kisiasa.
 
Kwa akili yakomunaona umeanzisha uI wa maana sana. Hii Hali inayoendelea ya maisha ni wazi waliko madarakani wamelewa ni bora kuanza ngwe mpya !
Issue siyo kubadilisha Viongozi/ Wanasiasa Suala ni Kubadilisha Mindset za jamii (UELEWA).....Wanasiasa hawa lao moja....(KUTAFUNA NCHI). Walioko Upinzani walikuwa CCM, waliopo CCM walikuwa UPINZANI....Anayeitwa FISADI leo huko CCM, kesho atapokelewa UPINZANI....Anayeitwa KAMANDA leo huko UPINZANI kesho atakutwa majukwaani akiwananga MAKAMANDA wenzake. Mind your business....
 
Hivi unajua kuwa Kenya aimeendelea zaidi kuliko Tanzania kwasabb ya upana wa demokrasia yao.

Au hujui kuwa Kenya wako juu kiuchumi kuliko Tanzania? Kama jibu ni Ndiyo, basi jaribu kuangalia exchange rate ya fedha ya Tanzania na Kenya.
 
Nilikuwa nawaza hapa kwamba CCM ndio chanzo cha matatizo yote haya, lakini hapana wananchi wanaoikalia Tanzania ndio chanzo cha mfumo mbovu wa siasa zilizopo nchini.

Mohamed Kawaida , Tulia Akson nk. (Tunaowaona kama wajinga) , wanaweza kuwa wapinzani wakubwa ikiwa Chadema ingekuwa madarakani , fikiria kuhusu Mchungaji Peter Msigwa.

Kenya kwa mfano , migogoro na lawama kwa viongozi haijawahi kuisha mbali na vyama tofauti tofauti kushika dola. tofauti na kwetu Chama kimoja , lakini Kenya ni political stable kuliko Tanzania kwasababu ya wananchi wake.

Freeman Mbowe angekuwepo Nafasi aliyopo Samia , huenda Samia, au Majaliwa wangekuwa wapinzani pia.

Jitihada kubwa ingewekwa kwenye kuelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu na kuwaonyesha nguvu yao kwanza,
Nachokiona mimi ni kwamba Serikali itaendelea kufanya inachokitaka na kuendelea kuwepo , tutalia kwenye tweets online nk. baada ya siku tunarudi hatua tuliyotoka!. nini kifanyike?.
Wakati TANU inapewa nchi ilikuwa na historia gani?
 
Never as Mbowe yuko pale kwani jamaa kakaa kihasara sana kutaka kuifilisi nchi na kuvuruga mustakabali wa hali ya siasa!
 
Jambo muhimu ni hoja ya CHADEMA kutaka kuleta Katiba mpya itakayobadili mfumo mzima wa utawala na uendeshaji serikali. Kupunguza mamlaka ya Rais, kurejesha mamlaka ya mihimili yote, kuimarisha taasisi, kuimarisha utawala wa sheria na kuimarisha mfumo mzima wa demokrasia ya vyama vingi.

Hapo, Rais atakuwa chini ya Katiba na sheria, nchi itaongozwa na utawala wa sheria, kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki na haki za binadamu zitaheshimiwa. Kwa maana hiyo, ile jeuri ya Rais au chama tawala kumiliki mfumo wa uchaguzi na kusisitiza kwamba kwao "ushindi ni lazima" haitakuwepo na utendaji wa serikali ukiwa ovyo wananchi wataweza kuiondoa serikali iliyopo kwa kura. Ile hofu kwamba CHADEMA wakiingia madarakani na watataka nao kukaa milele kwa kutumia dola haitakuwepo. Wakiboronga, wananchi wataweza kuirejesha CCM au chama kingine madarakani. Hapo ndipo ubora au unafuu wa vyama vyote vya siasa utakapodhihirika tofauti na ramli zinazoendelea sasa.

Hii ni ndoto ya Al Nacha? Ndivyo inavyoonekana katika mazingira ya sasa. LAKINI ndilo jambo linalopasa kupiganiwa na Watanzania wote kwa nguvu zote kama tunathamini mustakabali bora wa taifa hili. Ama sivyo tutaendelea na hii safari yetu ya kuelekea kuzimu huku tukichekelea kama mazuzu. Hakuna short-cut.
 
Hivi unajua kuwa Kenya aimeendelea zaidi kuliko Tanzania kwasabb ya upana wa demokrasia yao.

Au hujui kuwa Kenya wako juu kiuchumi kuliko Tanzania? Kama jibu ni Ndiyo, basi jaribu kuangalia exchange rate ya fedha ya Tanzania na Kenya.
Nafahamu hilo na ndio nilichomaanisha kwenye uzi wangu
 
Nilikuwa nawaza hapa kwamba CCM ndio chanzo cha matatizo yote haya, lakini hapana wananchi wanaoikalia Tanzania ndio chanzo cha mfumo mbovu wa siasa zilizopo nchini.

Mohamed Kawaida , Tulia Akson nk. (Tunaowaona kama wajinga) , wanaweza kuwa wapinzani wakubwa ikiwa Chadema ingekuwa madarakani , fikiria kuhusu Mchungaji Peter Msigwa.

Kenya kwa mfano , migogoro na lawama kwa viongozi haijawahi kuisha mbali na vyama tofauti tofauti kushika dola. tofauti na kwetu Chama kimoja , lakini Kenya ni political stable kuliko Tanzania kwasababu ya wananchi wake.

Freeman Mbowe angekuwepo Nafasi aliyopo Samia , huenda Samia, au Majaliwa wangekuwa wapinzani pia.

Jitihada kubwa ingewekwa kwenye kuelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu na kuwaonyesha nguvu yao kwanza,
Nachokiona mimi ni kwamba Serikali itaendelea kufanya inachokitaka na kuendelea kuwepo , tutalia kwenye tweets online nk. baada ya siku tunarudi hatua tuliyotoka!. nini kifanyike?.
Chakadomoz ni saccos

Wapi SACCOS imeongoza nchi?
 
Kama wao wenyewe kama chama kimeshindwa kujiendeleza na kujitofauyisha, hiyo tofauti ya kutuletea sisi wataitoa wapi?
Demokrasia imekufa, pesa hazijulikani zinaenda wapi, rushwa kwenye chaguzi ndio mwendo mdundo, sasa hiyo tofauti itatoka wapi?
 
Back
Top Bottom